Mzingo aktiki

(Elekezwa kutoka Arctic Circle)

Mzingo aktiki (kwa Kiingereza: Arctic circle) ni mstari wa kudhaniwa kwenye uso wa Dunia kwa latitudo ya 66° 33' 49 hivi[1]. Umbali wake na ncha ya kaskazini ni takriban kilomita 2,600.

Mstari wa mzingo aktiki kwenye ramani ya Dunia.
Mzingo aktiki kwenye ramani ya Aktiki.

Kinyume chake ni mzingo antaktiki upande wa kaskazini ya Dunia.

Ufafanuzi wa mzingo aktiki

hariri

Mzingo aktiki unafafanuliwa na latitudo ambako Jua linaanza kuonekana kwa saa 24 mfululizo kwenye solistasi ya Juni, mnamo tarehe 21 au 22. Latitudo yake unabadilika kidogo mara kwa mara pamoja na kucheza kwa mhimili wa mzunguko wa Dunia.

Maana ya mzingo aktiki

hariri

Maana kwenye siku ya solistasi ya Juni (mnamo 21 Juni), Jua halitui tena chini ya upeo wa macho ndani ya mzingo aktiki hata saa za usiku wa manane. Kadiri latitudo inavyopungua, yaani tukielekea zaidi kwenda kaskazini na kukaribia ncha, kipindi cha mchana kinarefuka hadi kufikia nusu mwaka nchani kabisa.

Kinyume chake, ndani ya mzingo aktiki kwenye siku ya solistasi ya Desemba (mnamo 21 Desemba), Jua halichomozi tena juu ya upeo. Hii haimaanishi giza kabisa wakati wa mchana lakini hakuna zaidi ila nuru ya mapambazuko saa 6 mchana. Kadiri tunavyokaribia ncha yaani kufika kaskazini, kipindi cha usiku na giza kabisa hurefuka hadi kufikia nusu mwaka nchani kabisa.

Jiografia

hariri

Mzingo aktiki una urefu wa kilomita 16,000 hivi. [2] Maeneo ndani yake ni takribani kilomita za mraba 20,000,000 ambayo sawa na asilimia 4 za uso wa Dunia. [3]

Mzingo Aktiki hupita kwenye sehemu zifuatazo: Bahari Aktiki, Rasi ya Skandinavia, Asia ya Kaskazini (Siberia), Amerika Kaskazini, na Greenland. Nchi nane huwa na maeneo ndani ya mzingo aktiki: Norwei, Uswidi, Ufini, Urusi, Marekani (Alaska), Kanada (Yukon, Northwest Territories, na Nunavut), Denmark (Greenland), na Iceland (kisiwa cha Grímsey).

Tabianchi

hariri

Tabianchi ndani ya mzingo aktiki kwa jumla ni baridi. Lakini pwani za Norwei si baridi sana kwa sababu zinapitiwa na maji ya Mkondo wa Ghuba unaopeleka maji ya vuguvugu kutoka ikweta hadi Norwei na Urusi kaskazini-magharibi ambako hayaruhusu maji ya bahari kuwa barafu wakati wa baridi kali. Hata ndani ya mzingo aktiki inawezekana kuwa na vipindi vya joto kabisa kwa muda mfupi; mfano mjini Norilsk (Krasnoyarsk Krai, Urusi) halijoto inaweza kupita sentigredi 30 kwenye mwezi wa Julai, lakini wakati wa Januari inaweza kushuka hadi sentigredi -50 (chini ya sifuri).

Wakazi

hariri

Kutokana na ukali wa tabianchi hakuna watu wengi wanaoishi ndani ya mzingo aktiki, kote duniani hawazidi milioni 4 kwa jumla. Kuna wakazi asilia waliowahi kuishi huko kwa miaka elfu kadhaa, kama vile Waeskimo au Waindio wa kaskazini. Siku hizi hao ni takriban asilimia 10 ya watu wote wanaoishi upande wa kaskazini wa mzingo aktiki[4] Takriban miaka 20,000 hadi 30,000 iliyopita makundi ya watu walihama kutoka Siberia wakivuka mlangobahari wa Bering na kuingia Amerika Kaskazini.

Miji mikubwa ndani ya mzingo aktiki iko katika Urusi, Norwei na Uswidi: Murmansk (wakazi 295,374), Norilsk (178,018), Tromsø (75,638), Vorkuta (58,133), na Kiruna (16,936).

Kwa upande wa Amerika hakuna miji mkubwa: Sisimiut (Greenland), ina wakazi wapatao 5,000 na Utqiagvik, Alaska ina wakazi 4,000.

Sehemu kwenye Mzingo Aktiki

hariri

Kuanzia meridiani ya sifuri na kuelekea mashariki, mzingo aktiki unapita hapa:

Majiranukta Nchi, mkoa au bahari Maelezo
66°34′N 0°0′E / 66.567°N 0.000°E / 66.567; 0.000 (Prime Meridian)  Atlantiki Bahari ya Norwei
66°34′N 12°3′E / 66.567°N 12.050°E / 66.567; 12.050 (Nordland, Norwei) Kigezo:NOR Visiwa vya Træna, Nordland
66°34′N 12°18′E / 66.567°N 12.300°E / 66.567; 12.300 (Bahari ya Norwei) Atlantiki Trænfjorden, Bahari ya Norwei
66°34′N 12°29′E / 66.567°N 12.483°E / 66.567; 12.483 (Nordland, Norwei) Kigezo:NOR Visiwa vya Nesøya, Nordland
66°34′N 12°41′E / 66.567°N 12.683°E / 66.567; 12.683 (Bahari ya Norwei) Atlantiki Nesøyfjorden, Bahari ya Norwei
66°34′N 12°49′E / 66.567°N 12.817°E / 66.567; 12.817 (Nordland, Norwei) Kigezo:NOR Visiwa vya Storseløya, Nordland
66°34′N 12°52′E / 66.567°N 12.867°E / 66.567; 12.867 (Bahari ya Norwei) Atlantiki Kvarøyfjorden, Bahari ya Norwei
66°34′N 12°57′E / 66.567°N 12.950°E / 66.567; 12.950 (Nordland, Norwei) Kigezo:NOR Visiwa vya Rangsundøya, Nordland
66°34′N 13°3′E / 66.567°N 13.050°E / 66.567; 13.050 (Bahari ya Norwei) Atlantiki Værangfjorden, Bahari ya Norwei
66°34′N 13°12′E / 66.567°N 13.200°E / 66.567; 13.200 (Nordland, Norwei) Kigezo:NOR Nordland
66°34′N 15°33′E / 66.567°N 15.550°E / 66.567; 15.550 (Norrbottens län, Uswidi)   Uswidi Norrbottens län (Mikoa ya Lapland (Uswidi)na Norrbotten)
66°34′N 23°51′E / 66.567°N 23.850°E / 66.567; 23.850 (Lapland, Ufini)   Finland Lapland
66°34′N 29°28′E / 66.567°N 29.467°E / 66.567; 29.467 (Karelia, Urusi)   Urusi Karelia
66°34′N 31°36′E / 66.567°N 31.600°E / 66.567; 31.600 (Murmansk, Urusi) Murmansk Oblast
66°34′N 32°37′E / 66.567°N 32.617°E / 66.567; 32.617 (Karelia, Urusi) Karelia
66°34′N 33°10′E / 66.567°N 33.167°E / 66.567; 33.167 (Murmansk, Urusi) Murmansk Oblast
66°34′N 33°25′E / 66.567°N 33.417°E / 66.567; 33.417 (Kandalaksha Gulf, Bahari Nyeupe) Bahari Aktiki Kandalaksha Gulf, Bahari Nyeupe, Bahari ya Barents
66°34′N 34°28′E / 66.567°N 34.467°E / 66.567; 34.467 (Murmansk Oblast, Urusi)   Urusi Rasi ya Kola, Murmansk Oblast — for about km 7 (mi 4.3)
66°34′N 34°38′E / 66.567°N 34.633°E / 66.567; 34.633 (Kandalaksha Gulf, Bahari Nyeupe) Bahari Aktiki Kandalaksha Gulf, Bahari Nyeupe, Bahari ya Barents
66°34′N 35°0′E / 66.567°N 35.000°E / 66.567; 35.000 (Murmansk Oblast, Rasi ya Kola, Urusi)   Urusi Rasi ya Kola, Murmansk Oblast
66°34′N 40°42′E / 66.567°N 40.700°E / 66.567; 40.700 (Bahari Nyeupe) Bahari Aktiki Bahari Nyeupe, Bahari ya Barents
66°34′N 44°23′E / 66.567°N 44.383°E / 66.567; 44.383 (Nenets Autonomous Okrug, Urusi)   Urusi Nenets Autonomous Okrug
66°34′N 50°51′E / 66.567°N 50.850°E / 66.567; 50.850 (Komi Republic, Urusi) Komi Republic
66°34′N 63°48′E / 66.567°N 63.800°E / 66.567; 63.800 (Yamalo-Nenets Autonomous Okrug, Urusi) Yamalo-Nenets Autonomous Okrug
66°34′N 71°5′E / 66.567°N 71.083°E / 66.567; 71.083 (Ghuba ya Ob) Bahari Aktiki Ghuba ya Ob, Bahari ya Kara
66°34′N 72°27′E / 66.567°N 72.450°E / 66.567; 72.450 (Yamalo-Nenets Autonomous Okrug, Urusi)   Urusi Yamalo-Nenets Autonomous Okrug
66°34′N 83°3′E / 66.567°N 83.050°E / 66.567; 83.050 (Krasnoyarsk Krai, Urusi) Krasnoyarsk Krai
66°34′N 106°18′E / 66.567°N 106.300°E / 66.567; 106.300 (Sakha Republic, Urusi) Sakha Republic
66°34′N 158°38′E / 66.567°N 158.633°E / 66.567; 158.633 (Chukotka Autonomous Okrug, Urusi) Chukotka Autonomous Okrug
66°34′N 171°1′W / 66.567°N 171.017°W / 66.567; -171.017 (Bahari ya Chukchi, Bahari Aktiki) Bahari Aktiki Bahari ya Chukchi
66°34′N 164°38′W / 66.567°N 164.633°W / 66.567; -164.633 (Seward Peninsula, Alaska, Marekani)   Marekani Seward Peninsula, Alaska
66°34′N 163°44′W / 66.567°N 163.733°W / 66.567; -163.733 (Kotzebue Sound, Bahari Aktiki) Bahari Aktiki Kotzebue Sound, Bahari ya Chukchi
66°34′N 161°56′W / 66.567°N 161.933°W / 66.567; -161.933 (Alaska, Marekani)   Marekani Alaska—ukipita katikaSelawik Lake
66°34′N 141°0′W / 66.567°N 141.000°W / 66.567; -141.000 (Yukon, Kanada)   Kanada Yukon
66°34′N 133°36′W / 66.567°N 133.600°W / 66.567; -133.600 (Northwest Territories, Kanada) Northwest Territories, ukipita katikaGreat Bear Lake
66°34′N 115°56′W / 66.567°N 115.933°W / 66.567; -115.933 (Nunavut, Kanada) Nunavut
66°34′N 82°59′W / 66.567°N 82.983°W / 66.567; -82.983 (Foxe Basin, Hudson Bay) Bahari Aktiki Foxe Basin
66°34′N 73°25′W / 66.567°N 73.417°W / 66.567; -73.417 (Baffin Island, Nunavut, Kanada)   Kanada Nunavut (Baffin Island), ukipita katikaNettilling Lake na Auyuittuq National Park (sign location)
66°34′N 61°24′W / 66.567°N 61.400°W / 66.567; -61.400 (Mlangobahari wa Davis, Atlantiki) Atlantiki Mlangobahari wa Davis
66°34′N 53°16′W / 66.567°N 53.267°W / 66.567; -53.267 (Greenland) Kigezo:GRL ukipita katikaKangerlussuaq Fjord na Schweizerland
66°34′N 34°9′W / 66.567°N 34.150°W / 66.567; -34.150 (Mlangobahari wa Denmark, Atlantiki) Atlantiki Mlangobahari wa Denmark
66°34′N 26°18′W / 66.567°N 26.300°W / 66.567; -26.300 (Greenland Sea) Greenland Sea
66°34′N 18°1′W / 66.567°N 18.017°W / 66.567; -18.017 (Grímsey, Iceland)   Iceland Island of Grímsey
66°34′N 17°59′W / 66.567°N 17.983°W / 66.567; -17.983 (Greenland Sea, Atlantiki) Atlantiki Greenland Sea
66°34′N 12°32′W / 66.567°N 12.533°W / 66.567; -12.533 (Bahari ya Norwei) Bahari ya Norwei
 
A sign along the Dalton Highway marking the location of the Arctic Circle in Alaska
 
Arctic Circle line in Rovaniemi, Ufini
 
Aurora Borealis above Arctic Circle sign along the Dempster Highway in Yukon at 66°33′55″N 136°18′26″W / 66.56528°N 136.30722°W / 66.56528; -136.30722 (Arctic Circle sign)

Tanbihi

hariri
  1. Obliquity of the Ecliptic, Nutation in Obliquity and Latitudes of the Arctic/Antarctic Circles, tovuti ya NeoProgrammics PHP Science Labs, Basic Astronomy and Science-Related Tools, iliangaliwa Septemba 2019
  2. Nuttall, Mark (2004). Encyclopedia of the Arctic Volumes 1, 2 and 3. Routledge. uk. 115. ISBN 978-1579584368. Iliwekwa mnamo 26 Julai 2016.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Marsh, William M.; Kaufman, Martin M. (2012). Physical Geography: Great Systems and Global Environments. Cambridge University Press. uk. 24. ISBN 978-0-521-76428-5.
  4. "Arctic Population". www.athropolis.com.