Danieli Fasanella na wenzake

(Elekezwa kutoka Danieli Fasanella)

Danieli Fasanella na wenzake (walifia dini huko Ceuta, 10 Oktoba 1227) walikuwa Ndugu Wadogo wamisionari huko Moroko.[1] Wote walikuwa mapadri isipokuwa Donulus.

Kifodini cha Wat. Danieli na wenzake.

Walitangazwa watakatifu na Papa Leo X tarehe 22 Januari 1516.

Sikukuu yao inaadhimishwa kila tarehe 10 Oktoba[2][3].

Historia

hariri

Kifodini cha Berardo wa Carbio na wenzake kilichotokea Moroko mwaka 1219 kilifanya Wafransisko wengi watamani kufuata nyayo zao kwa kuhubiri Injili kwa wasio Wakristo.

Basi, mwaka 1227, uilofuata ule wa kifo cha mwanzilishi, Fransisko wa Asizi, watawa 6 wa kanda ya Toscana, Agnelus, Samueli, Donulus, Leo, Hugolino na Nikola wa Sassoferrato, walimuomba Elia wa Cortona, mkuu wa shirika, awaruhusu kwenda Moroko kuwahubiria Waislamu.

Kisha kukubaliwa, walikwenda Hispania, alipojiunga nao kama kiongozi Danieli Fasanella wa Belvedere, mkuu wa kanda ya Calabria.

Toka huko walivuka bahari na tarehe 20 Septemba walishukia Afrika, walipobaki siku chache katika kijiji kilichokaliwa hasa na wafanyabiashara Wakristo.

Halafu, Jumapili asubuhi, waliingia mjini Ceuta, wakaanza mara kuhubiri kwa kupinga Uislamu. Kwa sababu hiyo walipekelekwa kwa sultani ambaye, akiwadhani ni vichaa, aliagiza watiwe gerezani. Walibaki humo hadi Jumapili iliyofuata, ambapo sultani kwa mabembelezo na vitisho alijaribu kuwafanya wakane dini yao.

Aliposhindwa, aliagiza wauawe. Kila mmojawao alimkaribia Danieli ili kupata baraka yake na ruhusa ya kumfia Yesu. Wote, baada ya matusi na mateso, walikatwa kichwa[4].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Father Candide Chalippe (1 Juni 2007). The Life and Legends of Saint Francis of Assisi. Echo Library. ku. 164–. ISBN 978-1-4068-4456-6. Iliwekwa mnamo 8 Julai 2013.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Martyrologium Romanum
  3. https://catholicsaints.info/martyrs-of-ceuta/
  4. https://www.santiebeati.it/dettaglio/73850

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.