Ceuta (tamka: the-uta; kwa Kiarabu: سبتة sabta) ni mji wa Kihispania kwenye pwani ya Mediteranea ambao upande wa bara unazungukwa na eneo la Moroko. Ceuta iko karibu na mji wa Tetouan upande wa Moroko. Umbali na Hispania ni km 21 kuvuka mlango wa bahari wa Gibraltar.

Kisiwa cha Ceuta
Ceuta (Hispania)

Pamoja na mji wa Melilla ni sehemu ya Hispania na Umoja wa Ulaya kisiasa , lakini kijiografia ni sehemu ya Afrika. Moroko inadai ni sehemu ya eneo lake la kitaifa.

Watu hariri

Ceuta ina wakazi 75.276 katika eneo la km² 18.5. Karibu nusu ni Wazungu/Wakristo na nusu ya pili ni Waberber-Waarabu/Waislamu.

Historia hariri

Ceuta inaaminika iliundwa na Karthago katika karne ya 5 KK. Jina la Kigiriki la mji imekuwa "Επτά Αδελφοί" (hepta adelphoí - ndugu saba).

Tangu Waroma walipochukua utawala wa Afrika ya Kaskazini mji ulijulikana kwa jina la "Septem Fratres" (ndugu saba). Jina hili limeendelea hadi leo, mji ukiitwa "sabta" kwa Kiarabu au kwa matamshi ya Kihispania "Ceuta".

Kuanzia karne ya 5 BK mji ulitawaliwa na Wavandali.

Mwaka 710 Waarabu Waislamu walifika wakipita Ceuta kuvamia Hispania. Hadi karne ya 14 mji ulikuwa chini ya watawala Waislamu ama Waarabu au Waberberi. Kati ya Wakristo waliofia dini yao huko wanakumbukwa watakatifu Danieli mfiadini na wenzake (1226).

Mwaka 1415 Wareno waliteka Ceuta wakaitawala hadi mwaka 1668. Baada ya vita kati ya Ureno na Hispania mji ulikabidhiwa kwa mfalme wa Hispania.

Tangu mwaka 1668 Ceuta imekuwa sehemu ya Hispania. Ndani ya Hispania imekuwa Mji wa kujitawala (kwa Kihispania: ciudad autónoma) tangu 1995.


Nchi za Afrika  
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
  Makala hii kuhusu maeneo ya Hispania bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ceuta kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.