Fransisko Caracciolo

Fransisko Caracciolo (kwa jina la awali Ascanio Pisquizio; Villa Santa Maria, Chieti, leo katika mkoa wa Abruzzo nchini Italia, 13 Oktoba 1563 - Agnone, Isernia, mkoa wa Molise, 4 Juni 1608) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki ambaye, pamoja na Yohane Augustino Adorno, alianzisha shirika la Wakleri Watawa Wadogo, akisukumwa na upendo wake mkubwa kwa Mungu na kwa jirani.[1]

Mt. Fransisko Caracciolo akifagia.

Fransisko alitangazwa mwenye heri na Papa Klementi XIV tarehe 4 Juni 1769, halafu mtakatifu na Papa Pius VII tarehe 24 Mei 1807.[2]

Sikukuu yake huadhimisha tarehe ya kifo chake, 4 Juni[3].

Maisha hariri

Tangu ujana wake alijulikana kwa uadilifu na heshima[4].

Aliamua kutawa alipokuwa na umri wa miaka 22, kisha kupatwa na maradhi ya ngozi yaliyodhaniwa kuwa ukoma, ugonjwa usiotibika wakati huo. Hapo aliweka nadhiri ya kumtumikia Mungu na watu maisha yake yote kama atapona.

Basi, jinsi alivyopona haraka ilitafsiriwa kuwa muujiza.[5] Kwa vyovyote, alijitahidi mara moja kutimiza ahadi yake, akaenda Napoli asomee upadri.

Mwaka 1587 alipewa upadrisho akajiunga na chama cha Bianchi della Giustizia (Weupe wa Haki), ambacho lengo lake lilikuwa kuandaa waliohukumiwa kufa waweze kufa kitakatifu.

Miaka 5 baada ya kuhamia Napoli (1588) alipata kimakosa barua ya Giovanni Agostino Adorno wa Genova iliyomualika jamaa yake fulani kuungana naye katika kuanzisha shirika jipya. Fransisko aliona kosa hilo liliingia katika maongozi ya Mungu aliyemtaka yeye aitikie mwaliko huo.

Hivyo alisaidia kuandika katiba ya shirika hilo ambalo lilikubaliwa na Papa Sisto V tarehe 1 Julai 1588, likathibitishwa na Papa Gregori XIV tarehe 8 Februari 1591, tena na Papa Klementi VIII tarehe 1 Juni 1592.[4]

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Paoli, Francesco. "St. Francis Caracciolo." The Catholic Encyclopedia. Vol. 6. New York: Robert Appleton Company, 1909. 23 Jan. 2013
  2. Capetola C.R.M., Fr. Nicholas, "History", Adorno Fathers
  3. Martyrologium Romanum
  4. 4.0 4.1 "Butler, Alban, "The Lives or the Fathers, Martyrs and Other Principal Saints", Vol. V, by the Rev. Alban Butler, Virtue and Company, Limited, London, 1954". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2016-06-03. 
  5. ibid.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.