Historia ya Komori

Historia ya Komori inahusu funguvisiwa vya Bahari ya Hindi mkabala wa Afrika Mashariki ambavyo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Komori, mbali na kisiwa cha Mayotte.

Asili ya wakazi

hariri
 
Jahazi.
 
Sultani Said Ali bin Said Omar wa Ngazija (1897).

Visiwa vya Komori vimekaliwa na watu mbalimbali kutoka Afrika na Asia Kusini katika historia ndefu. Wanaakiolojia walitambua mabaki ya makazi ya watu kutoka karne ya 6 kwenye kisiwa cha Nzwani lakini haijulikani kama watu walitangulia kufika mapema bila kuacha mabaki ya kutambulika.

Waswahili wa kwanza walifika kama sehemu ya uenezi wa Wabantu tangu karne ya 9 BK.

Kipindi cha kwanza huitwa kipindi cha Dembeni (karne ya 9 - 10) ambako Waswahili walianzisha kijiji kimoja katika kila kisiwa.

Wakati wa karne ya 11 hadi ya 15 biashara iliongezeka na Madagaska pia na wafanyabiashara kutoka Uarabuni. Vijiji vidogo vikaongezeka na vijiji vya awali vikakua vikawa miji.

Kumbukumbu ya wenyeji hutaja mara nyingi majina ya Waarabu kutoka Yemen na Saba' kama mababu wa koo asilia lakini hakuna uhakika kama kumbukumbu hizo zinalingana na historia halisi.

Athira ya Kiarabu na ya Kiislamu ikaongezeka kutokana na biashara ya watumwa, dhahabu na pembe za ndovu kati ya Afrika ya Mashariki na nchi za Kiislamu.

Waarabu na Waajemi walijenga vituo kwa ajili ya biashara yao pamoja na misikiti na kueneza dini ya Uislamu kwenye visiwa.

Hata kama Komori si karibu sana na pwani, hata hivyo kutokana na mwendo wa upepo ni kituo muhimu cha jahazi kwenye safari kati ya Kilwa na Msumbiji iliyokuwa bandari kuu ya dhahabu ya Zimbabwe.

Ukoloni na uhuru

hariri

Baada ya kutawaliwa na Wafaransa kuanzia mwaka 1841 hadi 6 Julai 1975, Komori ilipata uhuru, lakini wakazi wa kisiwa cha Mayotte kwa wingi wa kura waliamua kubaki chini ya Ufaransa, uamuzi uliothibitishwa mwaka 2009.

Kufuatana na katiba ya uhuru ya mwaka 1975 Komori ilitangazwa kuwa jamhuri ya Kiislamu.

Serikali zilipinduliwa mara kwa mara na wanajeshi au na mamluki.

Katiba mpya ya mwaka 2001 imeondoa tabia ya kidini ya dola na iliunda utaratibu wa urais kuzunguka kati ya visiwa vitatu vikubwa.

Katika muundo huo rais wa jamhuri atateuliwa kila baada ya miaka minne kutoka kisiwa tofauti.

Katika uchaguzi ya mwaka 2002 rais Azali Assoumani alichaguliwa kutoka kisiwa cha Ngazidja (Komori Kuu).

Katika uchaguzi wa 2006 rais amechaguliwa kati ya wagombea kutoka kisiwa cha Anjouan. Wananchi wa Anjouan walipiga kura ya kwanza. Wagombea watatu wenye kura nyingi wameteuliwa na kusimamishwa mbele ya wapiga kura wa visiwa vyote watakaomchagua rais wa jamhuri.

Rais wa mwaka 2010 alitoka katika kisiwa cha Moheli, baadaye tena rais kutoka Ngazidja, n.k.

Katika uchaguzi wa 2010 Ikililou Dhoinine ndiye aliyepata kura nyingi.

  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Komori kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.