Mtumiaji:Kipala/Archive 2
Karibu Wikipedia ya Kiswahili! --Chamdarae 00:03, 16 Desemba 2005 (UTC)
Uhusiano na wanablogu
Kipala, nina swali kidogo kwa vile nadhani wewe pia sio mwanablogu nami nisivyokuwa mmoja. Nimegundua blogu za wenzetu siku hizi tu. Kumbe, kuna mawasiliano mengi (hata na waandishi wa habari kama wale wa New York Times aliyoirejea Guaka katika blogu yake, au ombi la Amgine hapo juu n.k.). Sasa, sijui wanavyofaulu kuwasiliana kiasi ambacho huwasiliana nacho. Mimi napendelea kuendeleza wikipedia ya Kiswahili tu (ili wengine wapate ujuzi). Sawa, bila kutangaza hakuna ujuzi pia. Hata hivyo nimesikitika (au hata kuhuzunika?) kusoma kuhusu tumaini lao la kwamba Waswahili wamefikisha makala zaidi ya elfu moja wakati ni wasio Waswahili kama wewe waliochapa kazi. Je, tumaini limejengwa kichangani? Nitakuwa nimechoka kuchangia wikiwiki hii nikiendelea kusikia mipango na ndoto hizo. Labda utaweza kunionyesha picha kamili inayoleta tumaini kwelikweli. Asante, na kila la kheri, --Oliver Stegen 18:50, 22 Novemba 2006 (UTC)
- Sijawahi kushiriki na wanablogu wa Kiswahili hadi sasa. Nimesoma kidogo hapa na pala lakini ni kitu kingine tofauti na wikipedia. Ni kweli ya kwamba si Waswahili wengi mtandaoni lakini hata hivyo sitegemei ya kwamba kila Mswhili mtandaoni anajali hali ya Mswahili mwingine. (Mimi nilingia wakati wikipedia ilikuwa na makala 140!!)
- Halafu kuhusu wikipedia ni kitu kingine. Nadhani ni kweli si Waswahili wenyewe wa Afrika waliopanusha wikipedia hii hadi tuliko. Karibu yote iliandiwka na Waswahili (Watanzania/Wakenya) walio nje ya Afrika na Wazungu wapenda Kiswahili. Walioandika mengi hadi sasa ni sisi ambao tunaweza kuitwa "Waswahili wa Hiari" (kwa Kijerumani walitumia neno kama "Beutegermanen").
- Binafsi kwa kazi yangu ya wikipedia naona pande mbili. Upande moja ni furaha yangu: napenda kuandika Kiswahili na kupanusha ujuzi wangu wa lugha kwa kuandika (kazi hii yote ya kuangalia kamusi, sarufi, kutafuta maneno - eti mimi ni Mluteri na mzee wetu alianza kwa kutafsiri!!). Pia nina furaha ya elimu: Nisingejua mengi kuhusu visiwa vya Karibi kama nisingeandika makala hizi zote za kijiografia...
- Upande mwingine kwangu ni (au: ilikuwa? Hivyo ndivyo nilivyoanza) wajibu. Napenda kutoa shukrani zangu kwa Afrika kwa kuchangia kamusi hiyo ya wikipedia. Naamini ya kwamba wikipedia ni nafasi ya pekee kwa Kiswahili kupata kamusi elezo. Sioni kamwe kamusi ya kuchapichwa kwenye karatasi. HII NI TOFAUTI NA WIKI-KIIINGEREZA, KIJERUMANI n.k. Pia naona ya kwamba saa ya kamusi hii kutumiwa inakuja (haikufika bado)
- Maswali mengine ni: a) je, nani anaandika? b) Nani anasoma? c) Na je Waswahili wenyewe wanaonaje hawa Wazungu wanaoiandika ? hapa naona: a) kwa sasa ni wachache mno; Waswahili wa Afrika wenyewe ni wachache mno siwaoni karibuni. b) kwa sasa sidhani ni wengi wanaosoma. Lakini naamini saa inakuja. Mitambo inazidi kupatikana - na polepole watajua kamusi. Kuna faida ya kuandika kabla ya mitambo haikufika: wikipedia itakuwa tayari zaidi itakapohitajika. c) je wenyeji watapenda akina Oliver na Kipala waliandika mengi?? Labda hapana. Halafu? Si kitu. Kazi iko. Kama tumefanya kazi nzuri - basi (wazo la Kiluteri pia??)
- Na wanablogu? Dunia tofauti. Unaonaje? --Kipala 00:30, 23 Novemba 2006 (UTC)
- Asante, Kipala, kwa kunigusa nafsini! (Au ambavyo tungesema katika lugha yetu "Du hast mir aus der Seele gesprochen".) Mara nyingi siwezi kuniambia neno lifaalo. Pia, nimeanguka mtegoni mwa kuona wivu (nani asingependa kutajwa gazetini?). Asante kwa kunionyesha njia bora; nimeshaanza kutubu :-)
- Sasa nikueleze kuwa nami pia ni Mluteri (na kurithi hamu ya mzee wetu ya kutafsiri). Basi, nitaendelea kupanda miti yangu ya tufaha (ee, kamusi ya TUKI kweli inasema tufaha) bila kuangalia matendo ya wengine sana ila kuyafurahia ikiwezekana.
- Ka, ningependelea kukutana nawe na kujadiliana mambo hayo tukinywa na kula pamoja (hii pia ilikuwaga hamu ya mzee). Haya, ukifika mji wa Dresden, karibu sana! Ubarikiwe! --Oliver Stegen 10:07, 23 Novemba 2006 (UTC)
Thanks
- Thank you for the translation :-) Ev 02:21, 21 Desemba 2006 (UTC)
Merry Christmas!
Well you got one of your wishes! As you can see, changing the labels is easy, they are positioned by x and y coordinates. Codex Sinaiticus 17:46, 24 Desemba 2006 (UTC)
Wakabidhi wako wapi?
Kipala, nakutakia baraka za Mwaka Mpya. Je, unaelewa mambo ambayo yametokea katika wikipedia hii? Tangu Oktoba, wakabidhi ("administrators") hawakufanya kazi. Mabadilisho mengi yanafanyika na 'bots' tu, na majadiliano yamesinzia. Ukijua majibu kwa maswali yangu kuhusu Elinewinga au Tanganyika nitafurahi kupata habari kutoka kwako. Kila la kheri, --Oliver Stegen 09:30, 22 Januari 2007 (UTC)
- Salaam Oliver nadhani ni kweli wakabidhi wamepotea. Je unapenda kuwaandikia moja kwa moja? Kuhusu Elinewinga sina habari. Nilijaribu kutafuta Eli Newinga lakini sijafaulu. Tanganyika nimesahihisha sasa. Nisipokosei niliandika mwanzoni kabisa nilipoanza kuchangia. Eli Newinga - sijui.
- Naona kama wakabidhi hawawezi kurudi tujaribu kuwabadilisha. Wanaobaki kwa sasa si wengi. Lakini tusikate tamaa. Hata kama mimi mwenyewe napaswa kikazi kupunguza michango. --Kipala 20:55, 22 Januari 2007 (UTC)
- Nakushukuru, Kipala, kwa kazi yako ya kutenganisha makala zinazohusu Tanganyika.
- Elinewinga ni jina la Kichagga kama sikosei; nimegundua Marilyn Elinewinga na Helen Elinewinga na wengine mtandaoni lakini hakuna aliyekuwa mbunge wa wilaya ya Hai. Angalao hajatajwa mtandaoni. Basi.
- Ndesanjo ameshaniambia kwamba atarudi mwezi ujao. Sasa hivi anasumbuliwa na mambo mengi. Wale wengine sijui kama watarudi. Nami ningekuwa nisichukue masaa mengi hivyo ninavyofanya badala ya kuendesha masomo yangu ... :-( Haya, siyo rahisi kupunguza michango wakati tunaifurahia. --Oliver Stegen 21:17, 22 Januari 2007 (UTC)
Wakabidhi
Hello Kipala, I've nommed you to be an admin; I hope you don't mind. Sj 18:33, 1 Februari 2007 (UTC)
- I am not to keen and not sure thatI can keep presence up. But as things are - ok. Do we have to take this proposal of yours as an indicator that you yourself are on the way out? In that Case we should take in Oliver. --Kipala 19:31, 1 Februari 2007 (UTC)
Nimekufanya uwe mkabidhi. Una uwezo kufuta na kulinda makala, kuzuia wahuni, na kadhalika. Ona pia
- en:Wikipedia:Administrators' how-to guide (Kiingereza)
- de:Wikipedia:Administratoren (Kijerumani)
Kama una matatizo niulize. Hongera! Matt Crypto 18:51, 14 Februari 2007 (UTC)
- Asante! Nitauliza tu. --Kipala 20:24, 14 Februari 2007 (UTC)
Nitazingatia shauri lako
Habari mzee Kipala,
Upendo, nikupe hongera nyingi kwa jitihada zako katika kuhakikisha Kamusi elezi hii inakua na kupanuka kwa uwanja wa lugha ya Kiswahili. Nimependa kuwa mchangiaji mada na nitajitahidi kuweka makala nyingi nikianzia na maarifa ya dini. Kwa kweli nitaridhika sana na moyo wangu kuona nafasi hii ya kamusi elezi itajaa makala zenye kuchochea udadisi zaidi kuanza kwenye makala zenye hakika kwa jinsi zitavyowekwa. Nitazingatia ushauri ulionipa; kwanza naomba niendelee kujazia makala nilizozianza, kusudi baadaye nizitanabari(Adapt) katika fomati yenye kukubalika.
Tusonge mbele,
Mo X, DSM
Edits for Nigeria
It is somewhat confusing but I am enjoying learning. Thank you for your advice and corrections. --Mr Accountable 03:12, 25 Februari 2007 (UTC)
Nchi za Ulaya
--Oliver Stegen 13:18, 13 Machi 2007 (UTC)
Nchi za Afrika
Pia, sanduku la Chad limefupishwa. --Oliver Stegen 13:42, 13 Machi 2007 (UTC)
Nchi za Asia
Nchi za Asia bila makala kwa mji wake mkuu ni: Uturuki (lakini ni Istanbul tu). Haya, tuendelee ... --Oliver Stegen 15:11, 13 Machi 2007 (UTC)
Nchi za Amerika
Bila makala ya mji mkuu ni: -- Wasalaam, --Oliver Stegen 15:34, 13 Machi 2007 (UTC)
Nchi za Australia na Pasifiki
Kumbe - nimegundua hatujapata nchi hizo (ila Australia yenyewe na Papua Guinea Mpya). Haya, nitakungojea uzifanyie kazi New Zealand, Fiji, Samoa na kadhalika. Pole, Bwana! Tusisahau kuombeana, na ubarikiwe, --Oliver Stegen 15:39, 13 Machi 2007 (UTC)
Miji mikuu yenye makala fupi mno
Haya, nikaendelea kuchunguza miji mikuu nikagundua kuna mingine yenye makala ya sentensi moja tu. Nimeanza kutumia templeti yako ya "fupi" ili kuirejea miji hiyo. Katika Ulaya nimegundua Vilnius na London tu lakini nitaendelea. --Oliver Stegen 16:16, 13 Machi 2007 (UTC)
- Baadhi ya miji mikuu ya Kiafrika nimegundua mmoja tu uliye na makala fupi: Monrovia. --Oliver Stegen 11:50, 15 Machi 2007 (UTC)
- Miji mikuu ya Asia yenye makala fupi mno (yaani sentensi moja tu) ni ifuatayo: Kabul, Phnom Penh, Ulaanbaatar na Vientiane. Pia, nimeona makala za Jakarta na Taipei ziongezewe. Asante, --Oliver Stegen 12:23, 15 Machi 2007 (UTC)
- Asante sana umechapa kazi kweli. Najitahidi kwanza kumaliza nchi zote na masanduku halafu miji mikuu.--Kipala 14:58, 15 Machi 2007 (UTC)
- Miji mikuu ya Asia yenye makala fupi mno (yaani sentensi moja tu) ni ifuatayo: Kabul, Phnom Penh, Ulaanbaatar na Vientiane. Pia, nimeona makala za Jakarta na Taipei ziongezewe. Asante, --Oliver Stegen 12:23, 15 Machi 2007 (UTC)
Kiamu dialect
Hi, I am Botev from the Polish Wikipedia. I have seen that you have written in the article Lahaja za Kiswahili that the Kiamu dialect is spoken on the Lamu Island which is in Kenya. However my sources state that it is in fact a dialect of Rwanda. My sources may be wrong but still I would like to confirm this. Are you sure about the location of the Kiamu speakers? - My discussion page
- I am very sure about Lamu and Kiamu. No idea about your Rwandan Kiamu. Maybe a parallel name? What is your source? In Rwanda a dialect of what? --Kipala 10:18, 25 Machi 2007 (UTC)
- This a an academic book about languages of Africa. Kiamu is supposed to be a dialect of Swahili spoken in Rwanda. However, still there can be mistakes, so I will correct the corresponding article on the Polish Wikipedia. Thanks for your help. --Botev
- I just wrote the article on Lamu (mji). I did not mention it, but in local dialect town and Island are also called "Amu". Thats how "Kiamu" came about. Besides you can probably check in any publication on Swahili dialects, you will find Kiunguja, Kimvita and Kiamu as the three main dialect variations of Swahili. So either there is an error in your book, or people from Lamu made it to Rwanda, or it is just a parallel name form. --Kipala 17:58, 25 Machi 2007 (UTC)
- I am very sure about Lamu and Kiamu. No idea about your Rwandan Kiamu. Maybe a parallel name? What is your source? In Rwanda a dialect of what? --Kipala 10:18, 25 Machi 2007 (UTC)
Meaning of Zuhura in Arabic
Hi Kipala, Thank you very much for your kind message Your article about planets for Swahili wikipedia looks very nice and promosing . We all Wiki hope to see more and more article in Swahili and other non English language…
Regarding your question about the meaning of “ Zuhura”, The Following answer –in my opinion – may help you:
In Arabic language : Zahra (pl Zouhor) refers to flowers َزهرة- جمعها: زهور
But our case is: “ Zuh’ra” or “ Az’Zuhrah “ زُهـــره: Refers to
- Az’zuhrah ( zuhura) = Early evening and Early morning Star ( Venus )
Az’zuhrah ( zuhura) = Luminous, The Glorious white.
Reference : المنجد في اللغة و الأعلام: الطبعة 33 : دار المشرق لبنان
( 1992 ) ISBN:2-7214-2181-6
- Shukran ketir, ya ustadhi! --Kipala 21:34, 2 May 2007 (UTC)
Machafuko
Kipala, habari? Asante kwa kazi nzuri tena na tena! Nimeona ukigundua uharabu au machafuko kwenye makala fulani unayaondoa kwa kufuta neno hadi neno. Kwa vile u mkabidhi ungeweza kutumia "rollback" katika orodha ya Mabadilisho ya karibuni. Ni rahisi zaidi. Ila tusiitumie zaidi kuliko mara tatu kwa masaa 24. Kazi njema! --Oliver Stegen 20:30, 2 May 2007 (UTC)
- Rollback?? Kitu gani? Labda nitumie "screenshot". Asante --Kipala 21:30, 2 May 2007 (UTC)
- Samahani, nimekosea. "Rollback" haipo kwenye orodha ya Mabadilisho. Lakini ukifungua diff au historia ya makala fulani, badilisho la mwisho litakuwa na kitufe "rollback"; ukibofya hicho badilisho la mwisho litaondolewa na lile litangulialo litarudishwa. Rahisi tu! --Oliver Stegen 13:03, 3 May 2007 (UTC)
Byrialbot
Hello Kipala. Thank you for your message. I am doing what I can to get a botflag for Byrialbot. I first asked Matt Crypto because he is bureaucrat, but he has not been actice for several months. Then I asked at Wikipedia:Jumuia#Bot request for User:Byrialbot to get support from the local community so I afterwards can request the flag from a stewart at the Meta-Wiki. I have stopped the bot now at this wiki, but I kindly ask for support for my request at Jumuia so I will be able to get the flag. Thank you! Byrial 23:28, 6 Julai 2007 (UTC)
Nimekuelewa
Habari Ndugu Kipala, Katika mfumo wa langi mimi naona langi nzuri ni ile ya "Njano" ni rangi nzuri yenye kuvutia, pamoja na kuwa ni rangi nzuri ya njano bado kutakuwa na watu wengine wenye kutaka kuweka rangi tofauti na njano nk. hivyo basi kama inawezeka ni bora ile hiyari ya langi iendele kuwepo na utaendelea kuifanyia semi-protect unaionaje hiyo?. kuhsu makala kuanza na jina halisi la kuzaliwa ni vizuri, lakini sio tabu kwa wale ambao hawawajui wasanii majina yao halisi si itakuwa tabu kidogo kinamna flani au we unaonaje?, ni vizuri kiupande flani lakini ni tabu kwa wenye fikra chache za kufikiria anaemtafuta amtafute kwa jina halisi hali ya kuwa alijui inakuwaje hii, makala nyingi za kingereza unapomtafuta msanii wa kimarekani mara nyingi uwa unaandika jina la kisanii mfano Dr Dre, Ice Cube, Snoop Doggy, Raekwon, Methodman, na wengine wengi tu unawapata kwa majina ya kisanii, sasa sija fahamu kwamba mwanzoni walifungua makala kwa majina yao halisi arafu baadae na kuzi #REDIRECT bado sijafahamu ila nahisi kitu kama hicho na kuazia sasa nitakuwa nafungua makala kwa jina halisi kisha wewe utakuwa unazisogeza au kuzi Redirect, kama uta muda wa kufanya hivyo au mwenyewe nikisha nizimaliza naziredirect kazi. kazi nakutakia siku njema na Ramadhani njema kwa huku kwetu Tanzania tumeshaanza kufunga mwezi mtukufu wa ramadhani. wako katika ujenzi wa Wikipedia --Muddyb Producer 07:28, 13 Septemba 2007 (UTC)
Ku-Redirect
Habari yako Mzee Kipala, Natumai upo okey sawa, kuhusu maswala ya Ku-Redirect ni kazi ndogo sana kwasababu nilishawahi Ku-Redirect baadhi ya kurasa kwa mfano hii hapa Jamhuri ya watu wa China, kwetu Tanzania mara nyingi huwa tunaita hivyo ikiwa Jamhuri yoyote ile uwa tunaita Jamhuri ya nchi fulani mfano kongo, Czech nk. kwa maana ya kwamba Ku-Redirect naweza sema huwa naona kama vile sio safi lakini haya nitajitahidi kufanya hivyo ili nisiwe Beyond na Format ya Wikipedia, nita fanya hivyo kwasababu nimesha amua kuwa mwana Wikipedia wa kweli, na kingine nilikuwa naomba kama kitawezekana kufanyika, nikuhusu sanduku la habari kwa wanasiasa manake naona hamna lakini wikipedia ya kingereza ipo ya kiswahili tu ndio hamna, hilo lilikuwa ombi sio lazima sana unaweza kufanya hivyo kama utaona kuna muhimu fulani manake sio lazima sana kama taarifa tayari zipo sema kuwa sanduku ni Uboreshaji wa hali ya juu sana.sina mengi wako katika Ujenzi wa Wikipedia --Muddyb Producer 06:00, 14 Septemba 2007 (UTC)
- Asante kwa mchango kuhusu Redirect ni kweli si vigumu. Kati majadiliano ya awali tumeelewana hivyo kati ya wanawiki: Tufuate kawaida ya kamusi kama hizi za TUKI au pia Kamusi Hai; pale ambako Kamusi zinatofautiana sana au hazieleweki tutumie maneno yanayoeleweka lakii tuongeze REDIRECT ili maumbo yote yapatikane kwa mtumiaji anayetafuta. Wakati mwingie tumetumia kurasa za maana (k.m. Uingereza). Mara nyingi tahajia ya Kiswahili si imara sana na watu wamezoea maumbo mbalimbali basi tuandike Kiswahili sanifu iwezekanavyo lakini tufungue mlango kupitia maumbo mbalimbali ya jina. Hivyo jinsi ulivyoandika sasa Joachim Kimario au Master Jay mtu anafika palepale.
- Ile redirect ya China nilibadilisha kwa sababu ilichanganya China mbili. Kwa majina ya nchi ni sawa kutumia majina ya nchi jinsi yalivyo kawaida. Sidhani ya kwamba mtu ataita Ujerumani au Ufaransa "Jamhuri ya..". Kongo ni tofauti kwa sababu ziko mbili.
- Habari ya sanduku nitaangalia. --Kipala 14:49, 14 Septemba 2007 (UTC)
Ushirika Umeongezeka
Shikamoo Ndugu Kipala, natumai upo sawa. nashukuru kwa ku-kubaliana namimi kuhusiana na ile sanduku la wanasiasa na nimeliona ni zuri tu na linafaa. kuna jambo kidogo nataka uniambie, kuna uwezekano wa kumueleza mtu habari yoyote kuhusu uchangiaji wa wikipedia ikiwa yeye haja Jiandikisha?, manake kwenye siku mbili hizi katika kurasa mpya nimeona makala kama Tabata na Kizulu ni mtu aliyeandika lakini anaonekana haja pata msaada wa kutosha kivipi yani, kwanza hajafungua Akaunti wakati kufungua Akaunti ya wikipedia ni dakika moja au isifike sasa hii mtu kuanza kuandika makala bila hata kujiandikisha inakuwa makusudi au hajui? manake IP Address yake inakuwa iko wazi kila mtu anaoinyona, arafu makala zake bado haziji toshelezi najua umeiona sema bado unamuacha huenda akabadilika kutokana na makala zenyewe zilivyo sasa basi nilikuwa na mpango wa kufungua makala iitwayo hivyo hivyo makala ambayo yenyewe itakuwa ina namna kuwa mwanawikipedia, masharti na kurasa ile ya Msaada wa kuanzisha makala hivyo nazani itakuwa rahisi kidogo na pia nilikuwa naomba ruhusa ya kuchukua hii logo ya wikipedia nikaitangaze kwenye tovuti yangu nilizotengeneza mimi hivyo nitakuwa nahirahishia kinamna fulani je hilo linakubalika. kumbuka hayo ni mambo mawili
- 1 Kuanzisha makala yenye kuitwa makala kwa kutoa masharti na taratibu za kuanzisha makala.
- 2 Kuchukua logo ya wikipedia na kuenda kuitangaza kwenye tovuti zote ambazo mimi nilitengeneza.
sina mengi ni hayo tu, Baadhi ya tovuti ni hizi hapa - Tovuti ya Filamu za Tanzania, Tovuti ya Muziki Tanzania, wako katika Ujenzi wa Wikipedia --Muddyb Producer 05:42, 15 Septemba 2007 (UTC)
- Ndugu Muddy, kumbe unashiriki sana mtandaoni na kuhariri kurasa hizi tovuti za filamu na muziki? Hongera! Ni wazo zuri kuweka kiungo cha wikipedia ya Kiswahili humo.
- Kuhusu watu wasiojiandikisha: mimi nakubaliana nawe lakini hapa tunagonga ukuta kwa wakati huu. Itikadi au sheria za kimsingi za wikipedia zinasisitiza kuwa watumiaji wasibanwe mno - tulijadiliana mwaka jana ona majadiliano kwenye ukurasa wa jumuiya. Matt kwa sasa ni "mkubwa" ingawa hatuna wakubwa wala wadogo lakini tumemchagua kuwa "bureaucrat" ya sw-wiki yaani amepewa madaraka ya kiwango cha juu kwa sasa ni yeye pekee yake.
- Kitu cha kufanya ni kusahihisha. Kama mtu amejiandikisha kwa kawaida naandika kwenye ukurasa wa "majadiliano" asipojibu nabadilisha tu. Kama hajajiandikisha sisiti kubadilisha nikiwa na muda. Katika wikipedia nyingine mara nyingi hawaulizi au kusubiri lakini pale ni watu maelfu wanaoandika sisi ni wachache. Tofauti ya ustaarabu ni kama jijini au mashambani - mashambani watu husalimiana na kuongea jijini wanasukumana tu - basi sisi ni washamba. Faida ya kuwa na wikipedia ndogo. -- Umeona ya kwamba nimesahihisha kidogo "Kizulu", hasa kuweka viungo vya "interwiki" yaani ya lugha mbalimbali na jamii (category).
- Kuhusu kutumia logo: yaliyomo yote ya wikipedia ni huru - maana yake wewe (na mtu yeyote) ni huru kuyachukua na kutumia atakavyo; hata kuyaweka katika kitabu na kuuza. Kinyume chake sisi waandishi wa wikipedia tunapaswa kuangalia kama kweli tuna haki kutumia picha fulani - mara nyingi picha hizi si huru zabanwa na sheria ya kunakili. Tovuti yako ya filamu ni huru kutumia picha zote za wikipedia - lakini wikipedia hatuko huru kutumia picha za tovuti nyingine bila kuchungulia hali ya haki za picha ile.
- Halafu naomba sema: Bado nashangaa sahihi yako kuonekana bila kiungo. Ukitazama kwenye dirisha la "hariri" utaona watu kuonekana hivyo: [[User:Byrial|Byrial]] 23:28, 6 Julai 2007 (UTC) lakini wewe hivi: Muddyb Producer 05:42, 15 Septemba 2007 (UTC). Hii inatakiwa kujitokeza ukibonyeza hapo juu kwenye dirisha la "hariri".
--Kipala 13:47, 15 Septemba 2007 (UTC)
Ahsante Ndugu Kipala
Shikamoo Mzee Kipala, Kwanza shukurani kwa kunifahamisha namna Wikipedia ilivyo Mwazoni sikufahamu kama wikipedia ni mtandao huru ila Wikipedia wao hawapo huru kwa mitandao mingine. Swala la logo ya Wikipedia kuiweka kwangu ni kazi ndogo sana, kwanza nina marafiki wengi mno wa kimtandao japokuwa wote ni wadogo kiumri lakini fikra zetu kimtandao ni za hali ya juu hivyo kama nitaweleza kuhusu Wikipedia utaona wengi tu wanamiminika kuchangia na kazi hiyo nitainza si muda mefu kutoka sasa ni kiasi cha kuwaambia tu jamani njoeni huku tufanye mavituzi na kwa jinsi ninavyoifahamu wikipedia ukichangia makala siku moja tu lazima kesho utarudi tena kama ilivyo nikuta mimi nilijaribu siku moja tu nikajiona kesho nakuja tena ndio mpaka leo. Angalia sababu zilizo pelekea mimi kuwa mwanawikipedia.
- Mwanzoni nilikuwa na tafuta habari mbalimbali kwenye mtandao wa yahoo, habari zinazohusu Waongozaji wa filamu na waigizaji wa kimarekani na Ulaya kwa ujumla, sasa nikiwa natafuta kila kurasa inayokuja lazima wikipedia iwepo kila kurasa lazima wikipedia iwepo sasa nikawa najiuliza hii wikipedia ni nini? na mtandao gani?, hebu ngoja nianze kuperuzi kwenye hii wikipedia habari ninazopata kwenye wikipedia ni tofauti na mtandao mwingine wowote ambao mimi tayari nimeshawahi kuitembelea ikabidi ni jiunge hiyo ilikuwa wikipedia ya Kiingereza nikawa nafanya utembezi kadha wa kadha kwakuwa nina uzoefu na mitandao kwangu ilikuwa rahisi sana kuweka makala katika wikipedia, baadae nikapata wikipedia hii ya Kiswahili ndo nikaamua kuwa Mwanwikipedia wa Kiswahili kabisa kwakuwa kiswahili ni Lugha yangu hivyo itakuwa rahisi sana kuweka makala. kwani bwana kipala hushangae maelekezo unatoa kidogo lakini mimi ukija unakuta nishaweka na wala sirudii naendlea mbele tu, nadhani umenielewa vizuri tu wapi nilikotokea hivyo najua mambo kuhusu wikipedia ila bado nahitaji msaada wako zaidi. Wako katika Ujenzi wa Wikipedia --Muddyb Blast Producer 10:24, 17 Septemba 2007 (UTC)
Template Mwanasiasa
Habari Ndugu Kipala, Ile templeti ya mwansiasa inaonekana kama kuna tatizo hivi manake maandishi ya kichwa cha habari cha templeti hayaja pendeza kama yalivyo yale ya Templeti ya Msanii, hii inakuwaje sijafahamu kwanini imekuwa vile inabidi ufanye follow up kisha ukinge hiyo templeti kama ulivyo ikinga ile ya Wasaniii. ni hayo sina Mengi wako katika Ujenzi wa Wikipedia --Muddyb Blast Producer 14:19, 19 Septemba 2007 (UTC)
- Asante Nd Muddy, Naombe uweke kiungo wa mfano, sijaelewa vizuri ni nini unachomaanisha na ni nini unachopendelea. Sema tu nitaangalia.--Kipala 12:58, 19 Septemba 2007 (UTC)
Habari Ndugu Kipala, Jaribu kutazama utaona mwanzo wa sanduku huwa jina linaanza sasa katika hii templeti ya mwanasiasa cha kwanza kutokea ni yale maandishi yaliyo andikwa Mwanasiasa. yale maansishi pale hayastahili kuwepo kwa fikra zangu na kimtazamo pia, kwa maana ya kwamba hayaja leta sura nzuri hebu angalia makala ya shenazi ile templeti ya wasanii juu ya picha kuna jina tu hamna sijui huyu mwanamuziki au nini, vile ndo inavyotakiwa iwe kama ilivyo jengwa mwanzo, mwanzoni haikuwa vile inaonekana kuna mtu katia mkono wake au ulikuwa huja ikinga na ndiomaana ikaja kuwa vile, kifupi maandishi yanaingiliana kati ya maandishi yaliyondikwa mwanasiasa na jina la mwanasiasa. sina mengi ni hayo tu wako katika ujenzi wa Wikipedia --Muddyb Blast Producer 08:36, 20 Septemba 2007 (UTC)
Sijapata Jibu
Habari Ndugu Kipala, Ndugu yangu kipala mbona kimya kingi hivyo?, sijapata hata jibu kuhusiana na ile templeti ya mwanasiasa, marekebisho yake kidoogo ambayo simakubwa kama kuanza upya, sasa naona kimya kingi au ndo kazi nyingi!!!. nilikuwa naomba marekebisho kidoogo tu ya ile templeti ya mwanasiasa maelekezo soma majadiliano ya juu utaelewa nini kimesibu pale. bado nina ombi lingine, kuhusu hili ombi utafanya taratiibu wala halina haraka sana kwani hata kazi yake pia itakuwa taratiibu. ni kuhusu sanduku la habari la filamu, nimetembelea en-wiki kuangalia baadhi ya filamu habari zake yaani Over View naona kila filamu ina sanduku la habari lenye kukuelezea kuhusu filamu nzima, imetoka lini, imesambazwa na nani, mtayarishaji nani, nyota wa filamu nani nk. sasa ile ni safi kwanini na sisi wana sw-wiki tusiweke?. ninaomba ufany hilo mkubwa pindi tu uapatapo muda ila tuendelee kujadiliana juu ya hili na sio kukaa kimya bwana mkubwa. wako katika ujenzi wa wikipedia --Muddyb Blast Producer 05:39, 24 Septemba 2007 (UTC)
- Nd Muddy nisamehe nikiwa kimya kazi tu; templeti kwangu si kazi rahisi. Nilisita kubadiisha mara moja kwa sababu sijaridhika na templeti hii kwa ujumla. Nilijaribu kutumia mfano wa en:wiki lakini wale wamejengaa kitu kinachonishinda. Yaani sikutaka kuunda templeti nyingi mno lakini templeti ya siasa lazima iwe na nafasi mbalimbali. Kwa mfano Mbunge, rais au waziri asiye mbunge, kiongozi wa chama asiyeshika cheo cha kidola n.k. En:wiki waliunganisha kila kitu katika templeti moja ila tu hii siwezi ni kubwa mno. Hebu naomba usubiri mpaka nitakapokuwa tena na masaa mawili matatu kujaribujaribu.--Kipala 09:02, 24 Septemba 2007 (UTC)
Habari Ndugu Kipala, Ni sawa ukipata muda utafanya hivyo maana ni muhimu sana au unaonaje?. kisha kuna kitu kimenishangaza, ikiwa sisi wanawikipedia hatufurahii kumuona mtu anaweka makala au kutoa majadiliano bila ya Ku-login, vipi ndugu kipala wewe kutoa majadiliano bila hata ya kuingia, au ndo mawazo mengi?. wakati naingia kwenye ukurasa wa majadiliano niliona IP Address yako inaonekana yaani umejibu bila ya Ku-ingia, lakinini nimerekebisha. wako katika Ujenzi wa Wikipedia --Muddyb Blast Producer 16:56, 24 Septemba 2007 (UTC)
- Kumbe Nd Muddy mambo hutokea. Kwa kawaida naandika kutoka kwangu ambako mashine inashughulika kazi ya kujiandikisha bila mimi kugonga kitu. Leo nilikuwa nje nikatumia mashine ya mtu nikapita tu mara moja kwenye wiki kumbe nikaandika bila kuniandikisha. Basi lakini umenitambua asante. --Kipala 14:42, 24 Septemba 2007 (UTC)
Habari Ndugu Kipala, Sijakuelewa umemaanisha nini kuweka Category ya sanduku la habari, nimeangalia sijaelewa na hamna hata kimoja nilichokitaka vipi?. au ndio moja kati ya mfano, lakini ipo tofauti kidoogo majadiliano yetu ile kategori ya Sanduku la Habari, naomba nifahamishe. kisha naomba upitie Makala Hii Angelina Jolie kwa marekebisho nakuomba tafadhali kisha unipe taarifa wapi umefikia. wako katika Ujenzi wa Wikipedia --Muddyb Blast Producer 12:33, 25 Septemba 2007 (UTC)
- Ndugu Muddy hujambo, kuhusu jamii ile (category) nilikusanya tu masanduku mbalimbali yaliyopo tayari baada ya kuona si rahisi kukumbuka masanduku yote tuliyotengeneza hadi sasa. Yaani kuangalia sanduku kunanisaidia wakati wa kutunga nyingine. Pia ni vizuri kutosahau wakati wa kuandika makala (mfano: nilikuwa nimesahau ya kwamba nimeshatengeneza sanduku la "ziwa). Kwa hiyo jamii hii haikusababishwa kutokana na ombi lako.
- Kuhusu Angela Jolie: Nisaidie niangalie nini hasa. Niliona kosa moja ilikuwa ya interwiki (wikiquote imeonekana kama kiungo cha makala). Niangale nini tena? Ndimi wako --Kipala 13:02, 25 Septemba 2007 (UTC)
Habari Ndugu Kipala, Ni kuhusu makala ya jolie: makala ya jolie ilichukua kama muda wa masaa yasiyopunguwa sita kuweka makala nzima, kwamaana ya kwamba siku ya kwanza niliweka maelezo ya juu tu, siku ya pili ndio nikaweka maelezo yoote ambayo ndio nilichukua huo muda wa masaa sita na zaidi, hivyo makala lazima uwe umekosea baadhi ya maneno kuandika kutokana sija pumzika toka asubuhi saa tatu nilivyo anza mpaka saa tisa nipo naandika makala moja tu. sasa ile kuna makosa ya kiandishi sema ndugu kipala hujaona we soma kisha utaona, mimi nimeona baadhi najua ilikuwa uchovu ila kwasasa nairekebisha. Ahsante kwa ushirikiano wako mzee, tuendelee hivi hivi kuwekana sawa. wako katika ujenzi wa Wikipedia --Muddyb Blast Producer 05:51, 26 Septemba 2007 (UTC)
Ahsante kwa Pongezi
Habari Ndugu Kipala, Naam nimeona pongezi na hizi zote ni jitihahda za wanawikipedia wote, hivyo tupeane hongera kwa kufikia makala 6,000. Kinachotakiwa kufanya ni ushirikiano zaidi ili tuweze kufikia Elfu nyingine hivyo tuombeane kheri na maisha mema ili tuweze kufikia tena elfu 7,000. sina mengi ni hayo tu. wako katika ujenzi wa Wikipedia --Muddyb Blast Producer 05:49, 27 Septemba 2007 (UTC)
Asante
Asante sana ndugu Kipala kunikaribisha. Nitajaribu kuchanga na kujadili hoja zangu. Lakini kiswahili yangu si halisi. Asante tena. Muhammad Mahdi Karim 11:36, 28 Septemba 2007 (UTC)
Featured pictures
Habari ndugu, nilikuwa nafikiria, kwanini sisi hapa sw.wiki hatuna featured pictures? Muhammad Mahdi Karim 16:19, 28 Septemba 2007 (UTC)
- Asante kwa swali lakini nimeshakuambia hapa tuko mashambani. Sijui "Featured picture" ni kitu gani? Tueleze halafu weka mfano mmoja tayari! --Kipala 18:38, 28 Septemba 2007 (UTC)
- Featured Pictures ni picha nzuri sana zilizopo katika wikipedia. Picha hizi zinawekwa mwanzoni mwa wikipedia. mf picha hii imetolewa commons.
Muhammad Mahdi Karim 17:11, 29 Septemba 2007 (UTC)
- Asante, nikielewa vema ni kitu kama "picha bora" au "picha maalum" iliyopigiwa kura na wanawikipedia na kuonyeshwa kama kielelezo, sivyo? Sawa ukipenda kuanzisha hii basi ni jaribio. Lakini usikate tamaa kama si rahisi kupata watu wa kuipigia kura kwa sababu tuko wachache sana. Kimsingi tungekuwa na nafasi kwenye ukurasa wa mwanzo. Ila tu - tuko wachache sana. Mimi mwenyewe huwa nabadilisha "makala maalumu" wakati mwingine. Je, ungependa wewe kuchukua kazi ya kuhariri na kubadiliosha "makala maalumu" kila baada ya juma moja? Ningeshukuru kama mtu mwingine anachukua kazi hii. --Kipala 17:26, 29 Septemba 2007 (UTC)
- Umeelewa vizuri. Mimi ningependa kusaidia lakini lugha na kazi yangu inanibana. Naomba unieleze vizuri nini kufanya; nitafikiria... Muhammad Mahdi Karim 19:16, 29 Septemba 2007 (UTC)
- Safi sana. Basi tujaribu. Usiogope lugha. Sisi wengine ni Wajerumani au Waingereza, Waswahili kadhaa hadi sasa wana matatizo kuandika Kiswahili sanifu kwa hiyo tusione aibu, tusaidiane tu. HAya ukitaka kujaribu:
- fungua ukurasa wa mwanzo-kuhariri na takriban baada ya theluthi ya urefu wa maandishi utaona <h3 style="font-size:150%"><em style="color:orange;font-style:normal">•</em>'''Makala maalum: [[St. George's (Grenada)]]'''</h3>. Hapa utaanza kubadilisha.
- Umeelewa vizuri. Mimi ningependa kusaidia lakini lugha na kazi yangu inanibana. Naomba unieleze vizuri nini kufanya; nitafikiria... Muhammad Mahdi Karim 19:16, 29 Septemba 2007 (UTC)
- Kwanza chagua makala ya kufaa yenye picha nzuri. Ni vizuri kubadilishabadilisha vichwa au categories. Nimeweka uzito kwa mada za Kiafrika lakini si kila safari maana sisi ni jicho la Uswahilini kutazama dunia yote. Halafu chagua sehemu fupi ya mwanzo. Isizidi mistari jinsi iliovyo sasa. Badala ya "St. George's (Grenada)" unaingiza kichwa cha makala mpya ndani ya mabano. Unakili pia jina la picha na kuiweka baada ya "image:" badala ya jina lililopo (sasa: "StGeorgesGrenada2000.jpg"). Huwa mimi naweka hapa mistari 4-6 si zaidi kutoka mwanzo wa makala iliyochaguliwa. Ni sawa kufupisha kidogo ukiona sawa ili habari za kuvutia ziwe mbele.
- Halafu bonyeza chini kwanza kwa "Mandhari ya badilisho" (=preview) na angalia. Angalia kama picha ni sawa si ndogo wala kubwa mno. Ukubwa wa picha utabadilisha kwa kuandika namba tofauti mbele ya "px" (kwa sasa: |thumb|250px|; mara nyingi 180 px zatosha lakini hii hutegemea na picha yenyewe), sahihisha kama lazima halafu gonga "Weka ukurasa". tayari. --Kipala 20:03, 29 Septemba 2007 (UTC)
- Sawa. Sasa nikuulize katika lugha ya kiingereza kama nimeelewa vizuri.
- What I will have to do will be to change the article at the main page every week. Right? Muhammad Mahdi Karim 08:31, 30 Septemba 2007 (UTC)
Templeti ya Filamu
Habari Ndugu Kipala, Nimeomba templeti ya filamu kisha kipala ukanijibu kwa maelezo ya kuwa kuunda sanduku si kitu kidogo sana, ni suala la kukaa na kutulia. sasa basi kama utapata mda inabidi ujitahidi ili tuweze kusogea maana hao wana en-wiki walianza taratibu mpaka wamefika, arafu ninaswali jingine kuhusu hiki chumba cha kuandikia (Sand Box): Katika en-wiki kuna ile alama ya kuwekea break (br /), lakini kwenye sw-wiki hamna ile vipi?, kwani hamna uwezekano kabisa wakuweza kuwa nayo ile, lakini ili pia ni ombi kama itakuwa ngumu basi hata hivyo haitumiki sana lakini kuna usemi wa kiswahili usemao "Akiba Haiozi". ni hayo tu wako katuika ujenzi wa wikipedia --Muddyb Blast Producer 05:29, 29 Septemba 2007 (UTC)
- Habari Ndugu Muddy, sijaelewa vizuri unamaanisha nini. Mimi kuhariri templeti ni kweli swali la muda sina maarifa makubwa sana. Kama unaweza kueleza vizuri unachotaka ni rahisi zaidi. Itasaidia ukiweka kiungo ndani ya swali lako ya kunielekeza moja kwa moja kwa mfano unaoongelea. Hii pia kwa swali kuhusu ile "break" katika en:wiki. Sina uhakika ni nini. Labda rudia swali ukiweka kiungo moja kwa moja pale ulipoona kitu kile. Asante --Kipala 16:47, 29 Septemba 2007 (UTC)
Templeti Zinazohitajika
Umeona hayo Maandishi ya juu ya jina la mlengwa (Mwanasiasa wa Tanzania), hayatakiwi pale yaondoshe ili kuweka templeti iwe na sura nzuri kisha pandisha juu jina la mlengwa. Angali templeti ya msanii utaona jina tu hamna kusema huyu mwanamuziki nk. kwasababu ile templeti yenyewe inajieleza hivyo mtu anapo soma anelewa kama huyu ni nani. ombi langu kubwa ni hayo maandishi ya juu yaondoke iwe kama templeti ya msanii kuwa juu hamna kingine zaidi ya jina tu. hata zile templeti za kiingereza zipo hivyo hivyo juu hamna kingine zaidi ya jina tu taarifa zaidi utapata kupitia maandishi yaliyopo chini katika templeti. natumai utaelewa nini nililenga. jambo lingine kuhusu ile alama ya break: ile alama ya break kwenye en-wiki ipo kama alama ya ENTER, yaani kuna kama mshale unashuka chini, jaribu kuangalia kwenye en-wiki ndio utaelewa zaidi maana nikiweka hapa na yenyewe itashusha. sina mengi ila sidhani kama umenilewa maana sisi ni waswahili lakini kiswahili hatujui kama usemavyo ndugu kipala. kama ujanielewa nitakufahamisha zaidi. wako katika ujenzi wa wikipedia --Muddyb Blast Producer 05:18, 1 Oktoba 2007 (UTC)
- Haya Nd. Muddy mstari huu nimeondoa lakini sijaridhika bado na muundo wa templeti hii. Sijui nafasi nitapata lini.
- Ile alama ya break bado sijaelewa vizuri bado. Ningeomba nipe mfano wa ukurasa pamoja na anwani yake au nakili ile sehemu kutoka ukurasa wa "hariri" humo. Ukitaka kuionyesha tu kuna mbinu kuandika kabla <nowiki> na nyuma yake </nowiki> itaonyesha tu bila kutekeleza amri. Kuna mbinu ninayojua ni kutumia amri ya <br> inayoweka "break" na kusababisha mstari mpya mmoja (tazama kwenye "hariri" jinsi nilivyoweka nowiki kabla na nyuma ili kuzuia break isitekelezwe ionyeshwe tu.)
- Natumaini hujakasirika kuhusu yale niliyoandika kuhusu lugha. Ninavyoona ni kweli balaa au angalau tatizo ya kwamba wasomi wengi Waswahili wamezoea ama kuandika kwa Kiingereza au kuwasiliana kwa mchanganyiko wa Kiswahili na Kiingereza hadi wanaona vigumu kujieleza kwa Kiswahili sanifu kuhusu mada mbalimbali. Nilikaa Kenya huko hali ya kiswahili ni ama kuhuzunika au heri kucheka tu. Katika wikipedia hii ni sisi Wajerumani tuliochangia mengi hadi sasa lakini kwetu lugha namna gani? Yaani hata kama tumezoea nidhamu kutazama tena na tena kamusi kuhusu tahajia lakini sentensi zangu mara nyingi ni sentensi za Kijerumani kabisa nikitumia maneno ya Kiswahili si sentensi za Kiswahili hata kidogo. Wenyeji kwa kawaida hawana neno sijui wananivumilia au hawajali? Au hawatambui kwa sababu wengi wao wamezoea aina za "sheng". Hii ilikuwa sababu nilijaribu kumpa mgeni wetu moyo asione aibu sisi sote hapa twatembea kwa mikongojo tu! Ila tu tunasonga mbele hata hivyo. Basi ni yale tu --Kipala 09:40, 1 Oktoba 2007 (UTC)
Salam Kipala, Hii ipo sawa na nimeridhika na majibu yako. yapo asahihi sana. kuhusu masuala ya break naona lengo ushalijua lilikuwa nini, hivyo hamna haja ya kuendelea kujadiliana kuhusu break nitatumia tu ile ya kuweka <br> najua itakubali kama nilivyokuwa nafanyanya zamani, sema mimi ni mtu wa pwani (Mamwinyi huwa hatupendi tabu) tunataka tubofye tu kisha br itokee yenyewe na sio kuandika. sian mengi ni hayo tu. ila wewe mwanasiasa sana ume ni Manipulate mpaka nimekubali kama ule ulikuwa mfano kuhusu lugha sanifu hivyo hata kinyongo kiliondoka kwa kucheka baada ya kusoma yale majadiliano. kila lakheri tufunge mikanda safari bado ndefu kama ya Indiana Jones (Harison Ford) katika safari zake za utafiti na uchunguzi wa kina hivyo tubadilike na tuendeleze wikipedia kila siku ya mungu. tukijaaliwa--Muddyb Blast Producer 13:07, 1 Oktoba 2007 (UTC)
Naomba Msaada
Hbari Ndugu Kipala, Naomba Unisadie maana ya maneno haya kwa kiswahili fasaha
- Telenovelas.
- TV Series.
Ni hayo tu ndio nataka maana halisi kwasababu nilijaribu kutafsiri Telenovelas nikashindwa, kwenye kamusi ya yake.edu hamna, ila TV Series naweza sema sikupenda maana yake bado naitilia shaka kwasababu kiingreza si lugha yangu ila nilijifunza sasa basi kwakuwa wewe mzungu ni rahisi kwako kuelezea maneno haya. naomba nisaidie ili kuweka kiswahili fasaha ili makala zieleweke. naomba hili unijibu haraka bosi, sina mengi. --Muddyb Producer 13:11, 2 Oktoba 2007 (UTC)
- Salaam Muddy, sasa unauliza swali gumu. Telenovela labda si kitu sana. Yaani hata kwa Kiingereza au Kijerumani neno la Kihispania "telenovela" latumiwa kwa sababu wakitaka kutaja aina hii ya pekee hakuna neno. Hapa nafikiri hata kwa Kiswahili ingekuwa sawa kusema "(TV-series)-aina ya telenovela". Ugumu kwangu ni "TV-series". Hapa sijui. Kitu kama "mfulizo wa filamu"? "riwaya-filamu"? Je kwenu TZ hakuna kawaida ya kutaja filamu hizi kwa Kiswahili? Yaani kama hadithi fulani yasimulizwa kwa filamu fupi zinazofuatana? Kimsingi ni hiyo tu. Ile "sabuni" (=soap) ni aina ya Kimarekani, Telenovela ni ileile kwa namna ya Amerika ya Kihispania, n.k. Nilipokaa TZ ilikuwa mashambani hapana TV; Kenya - sikumbuki kama waikuwa na neno lakini sijaangalia sana TV hasa sijakuwa na KBC. Labda fanya utafiti pale kwako. Kwa sasa sina mengi --Kipala 22:45, 2 Oktoba 2007 (UTC)
Salam Nd. Kipala, Si umeona sasa na umeamini ule usemi wa kiswahili usemao: Kwenye wengi kuna Mengi. angalia umeshanipa maana halisi ya neno Tv-series. hii ni riwaya, simulizi za hadithi fulani yenye kuendelea kila siku, na hata kama ikisha basi atakuja mwingine kuindeleza. mfumo mzima wa tamthilia au filamu yenye tabia yakuwa series basi hizi huwa hazina mwisho labda upite ubinafsi au wasipate mwingine wa kushikilia ile sehemu kama alivyoshikilia yule aliopita. mfano riwaya ya James Bond, huwezi kuwa katika series za james bond kama hujatokea katika jumuiya ya kifalme yaani UK. wengi nilowaona na kuwasoma katika en-wiki wanatokea Scottland au Uk. Telenovelas.
Hili neno toka mwanzoni nilikuwa nahisi kama mfumo flani wa tamthilia za kilatini sema nilikuwa natafuta uhakika tu midamu nimepata uhakika basi nitaindeleza kusema kama vile lilivyo, nadhani pia wataelewa kama nilivyoelewa mimi. Ahasante kwa msaada na nitaendelea kukuuliza pindi tu nipatapo shida.--Muddyb Blast Producer 06:26, 3 Oktoba 2007 (UTC)
Makala Kuhusu Ujerumani ya Nazi
Habari Nd. Kipala, Naomba uandiki makala hii (German for "Protective Squadron"), kwa kifupi SS au Schutzstaffel. Nilikuwa natafuta filamu fulani ya Kijerumani inaitwa Escape from Sobibor, Hapo ndipo nilipopata habari za kuhusu SS, kwa upande fulani imenifurahisha na nimeependa lakini kwa kutafsri itanichukua muda sana, kwakuwa tunae mtu anayetokea huko ujerumani (Bwana Kipala) wewe utaweza kuandika makala hii hata kwa ufupi ili tufahamu nini kilitokea wakati huo. Hili ni ombi tu unaweza kufanya hivyo mara tu upatapo mda, maana hii makala ni nzuri sana arafu tena hii ujerumani ya nazi ndio ipi?, nataka kuijua najua wewe yote utaelezea kama utaamua kuandika makala hii ya Schutzstaffel. sina mengi wako katika ujenzi wa wikipedia --Muddyb Blast Producer 13:43, 4 Oktoba 2007 (UTC)
Hongera Mzee Kipala kwa kazi Yako
Shikamoo Mzee Kipala, Ahsante kwa kuitikia ombi langu la wewe kuunda makala ya Schutzstaffel. Inaonyesha ni kiasi gani tunasikilizana na kuelewana. Chamsingi ni kukupa pongezi kwa kazi yako. Ile makala nimesoma na nimeelewa kule walipo pelekwa wale wayahudi wa kipoland, ni katika kambi ya mauiti safi sana. Japokuwa huja ni jibu kama ile makala umeandika au la, mpaka niliojaribu kutafuta ndio nikaona, Najua ulikuwa umechoka sana kwa kuandika makala ndefu kama ile ndicho kitu kilichopelekea wewe uache hata kunitaarifu kuhusiana na ile makala kwa hilo lawama hamna chamsingi makala midamu makala ipo hilo aligombwi. kazi njema nakutakia kila lakheri katika ujenzi wa wikipedia.--Muddyb Blast Producer 07:45, 5 Oktoba 2007 (UTC)
Template Filamu
Habari Nd. Kipala, Sijaelewa kidogo pale nini kinachotakiwa kulingana, kama ikiwa ni producer inabidi iandikwe (Imetayarishwa na), sizani kama lingine zaidi ya hilo ikiwa lile neno la producer au? unasemaje mkubwa wangu.--Muddyb Producer 13:15, 8 Oktoba 2007 (UTC)
Habari Nd. Kipala, Nimejaribu kuweka sawa zile HTML lakini inaonekana kama kwenye sehemu ya kwanza kuna kasolo, Kati ya jina na picha - maelezo ya picha hadi kuelekea kwenye ukubwa wa picha, Haya maelezo bado yanapishana kisha hamna kiungo cha kuwekea katika template ya mtumiajai. kwa habari zaidi fungua ile template kisha fananisha kati ya ile ya mtumiaji na kile chanzo cha template. Angalia hapa. --Muddyb Blast Producer 05:54, 9 Oktoba 2007 (UTC)
- Slaam, naomba angalia hapa --Kipala 06:49, 9 Oktoba 2007 (UTC)
Bado hali ni tete. ile template ya element ndio ya ajabu bora hata ile filamu, kwanza imenza na rangi kitu ambacho kimenivunja nguvu pili sijaielewa kiurahisi kama ile ya filamu, kwa msaada zaidi ili niweze kuunda template mwenyewe nzuri naomba ninakilie ile template ya msanii hapo nitaweza maana template ya msanii inafanana na ile ya filamu tu. sina mengi nisaidie hilo kwanza habari kamili hapa. --Muddyb Blast Producer 09:21, 9 Oktoba 2007 (UTC)
- Slaam, naomba angalia hapa --Kipala 06:49, 9 Oktoba 2007 (UTC)
Mwisho wa Maarifa Yangu
Haya bwana Kipala kwa juhudi zangu zote na maarifa niliotumia nimeweza kufikia hiyo sehemu unayoona, sema kuna kitu sijaelewa kabisaa yani, Vipi yale maandishi yanatokea pale kwenye ile templeti ya mtumiaji, kama maandishi nimefuta kinachotakiwa kuonekana ni maandishi ya mtumiaji na sio yale ya template sijui umenipata hebu angali hapo chini.
{{Filamu
| rangi =
| jina = Harusi ya Candy
| picha = Harusi ya Candy.jpg
| maelezo_ya_picha = Kasha la Filamu ya HYC
| Imeongozwa na = Tuesday Kihangala
| Imetayarishwa na = GMC Wasanii
| Imetungwa na = Tuesday Kihangala
| Nyota = Angel John, Tuesday
| Muziki na =
| Imehaririwa na =
| Imesambazwa na = GMC
| Imetoka Tar. =
| Muda = 130.dk
| Nchi = Tanzania
| Lugha = Kiswahili
| Bajeti ya filamu =
| Mapato ya filamu =
| Ilitanguliwa na =
| Ikafuatiwa na =
| Tovuti =
}}
--Muddyb Blast Producer 12:38, 9 Oktoba 2007 (UTC)
- Muddy, umeshafika! Naomba angalia kule --Kipala 12:51, 9 Oktoba 2007 (UTC)
- Kipala Upo? rudi nyumbani
Nimesha gundua kosa liko wapi sasa hii naomba ruhusa niifanye kesho manake leo hali mbaya. Kiasi bwana kipala useme kuunda template si kazi ndogo mhhh, hali mbaya basi kesho nitaiangalia wapi nemekosea. ukiwa unalolote la kusema sema mzee wangu usihofu kwani bado nipo kazini ila baada ya nusu saa nitaondoka maana huku dar es salaam ni hali ya baridi hivyo inabidi tuwahi majumbani kupumzika. Ahsante --Muddyb Blast Producer 14:06, 9 Oktoba 2007 (UTC)
- Sikuwa karibu na mitambo basi angalia haya. :
Harusi ya Candy | |
---|---|
| |
Imeongozwa na | {{{imeongozwa na}}} |
Imetungwa na | {{{imetungwa na}}} |
Imetaarishwa na | {{{imetaarishwa na}}} |
Nyota | Angel John, Tuesday |
Imehaririwa na | {{{imehaririwa na}}} |
Imesambazwa na | {{{imesambazwa na}}} |
Muda wake | 130.dk |
Imetolewa tar. | {{{imetolewa tar.}}} |
Nchi | Tanzania |
Lugha | Kiswahili |
Habari Nd. Kipala, Nimeona templeti umeshafanya marekebisho. Sasa ni kucheki tena wapi kunashindwa kuonekana maana kuna baadhi ya vitu vya jedwali dogo vipo lakini havifanyi kazi, Hivyo nitajaribu kuweka sawa au kama utaendelea kurekebisha sawa maana wewe ni mtalaam miaka mingi mimi bado mgeni ndio kwanza nina miezi miwili. Kazi njema baadae kidoogo nitarudi ila ukiweka ujumbe nitaupata maana sipo mbali na mitambo. --Muddyb Blast Producer 06:30, 10 Oktoba 2007 (UTC)
Masahihisho ya Makala
Habari Bwana Kipala, Unajua templeti ya filamu iliniweka mbali kidogo na masuala ya uandishi wa makala lakini kwa sasa nimejaribu hii ya Saida Karoli, Sasa naomba msaada wa kuipitia makala na kuangalia lugha na kiswahili chake kinaeweka? sina mengi ni hayo ndugu yangu ila usisahau kunijulisha juu ya hili katika kurasa ya majadiliano ya Saida ambapo ni hapa.--Muddyb Blast Producer 09:17, 10 Oktoba 2007 (UTC)
Kipala upo? rudi hapa.--Muddyb Blast Producer
08:45, 11 Oktoba 2007 (UTC)
Ahsante kwa masahihisho yako
Salam Nyingi Nd. Kipala, Ni baada ya kumaliza siku kuu hizi mbili tatu naona nimerudi tena uwanjani.
Katika moja kati ya makala nilizoandika kuhusu filamu za kimagharibi nime bahatika kuona masahihisho kadha wa kagha, Hii inaonyesha ni kiasi gani tupo pamoja katika ujenzi wa Wikipedia, Japokuwa Nd. Kipala uliacha kabisa masahihisho na kuniacha kijana wako peke yangu na andika makala bila wewe kuzipitia japokuwa nilikuwa nakuomba uzipitie na huzipitii. Kwakuwa kulikuwa na dhana ya mimi nishakomaa hivyo nina uwezo wa kuandika makala bila hata mzee kipala kuizpitia.
Kwenye makala za Spaghetti Western nimeona masahihisho yako na nimefurahi sana kitendo cha wewe kuweka sawa zile makala. Ahsante Sana. --Muddyb Blast Producer 12:33, 15 Oktoba 2007 (UTC)
- Pole na kazi nyingi. Naomba uangalie filamu za western na masahihisho kidogo kwenye Saida Karoli. --Kipala 21:44, 15 Oktoba 2007 (UTC)
Habari Nd. Kipala, Ahsante nimeona ile makala ya Filamu za western. Sasa kuna suala moja naomba tufanye kama inawezakana. Ni kuhusu ujenzi wa watu na washiriki wa filamu za western, Nimesha anza na Clint Eastwood, Lee van Cleef, Bud Spencer. Kinachotakiwa kufanya mimi na anzisha makala kisha wewe utakuwa unasahihisha kama ulivyo fanya hizi zilizopita je unasemaje muda huo unao? Na kama unao basi jahazi ndio hilo linaenda zake. --Muddyb Blast Producer 05:31, 16 Oktoba 2007 (UTC)
- Habari Muddy, Muda ni vigumu kidogo siku hizi. Najaribu lakini siwezi kuahidi kitu chochote. --Kipala 05:35, 16 Oktoba 2007 (UTC)
Naam Nd. Kipala, Nimeitikia wito kwani kwa hilo ni dogo sizani kama linasumbua nitafanya hivyo. Na kuhusu watu walioshriki kuigiza filamu za western vipi? Maana sijapata jibu bado kama sawa au? --Muddyb Blast Producer 06:17, 16 Oktoba 2007 (UTC)
- Muddy umechoka? Usome hapo juu ya swali lako la mwisho. --Kipala 07:08, 16 Oktoba 2007 (UTC)
Kicheko, Najua umejibu kifalsafa. Haina neno nitafanya hivyo. Ila ukipata muda inabidi ujitahidi kuzipitia makala hizi za western unasemaje?.--Muddyb Blast Producer 08:04, 16 Oktoba 2007 (UTC)
About AlleborgoBot
Hi! I had made a request for flag here a week ago, can you support my request to speed up the bot assign process? Anyway, now the bot is stopped. I'll restart only when the flag will be on. Goodbye. --AlleborgoBot 22:47, 18 Oktoba 2007 (UTC)
Namomba Msaada Kidoogo
Salam Nyiiingi Nd. Kipala, Ni baada ya mapumziko kidogo ya hapa na pale lakini nimerudo tena ila sijaanza na masuala ya uuundaji wa makala kwakuwa baadhi ya vitu navihitaji kisha sivipati hivyo nimeamua kuunda zana za kufanyia kazi ili niweze kufanikisha makala zinazohitaji hizo zana. Moja kati ya zana hizo ni hii Teplate Muigizaji bado naifanyia kazi ya kuitafsiri kitaratibu ili iweze kutumika, Endapo utapata muda wa kunisaidia kwa hili nitashukuru maana umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, Endapo pia utaona muda mdogo basi nitajitahidi kuiwezesha. Sina mengi wako katika ujenzi wa Wikipedia --Muddyb Blast Producer 14:24, 19 Oktoba 2007 (UTC)
- Salaam, naondoka kidogo kwangu. Labda nitapata nafasi Jumapili jioni. Nimeangalia templeti kwa kifupi. Ningeshauri kuifupisha - unataka kweli mahali pa kaburi ? --Kipala 14:44, 19 Oktoba 2007 (UTC)
Salam Nd. Kipala, Sizani kama kuna ulazima wa kuweka sehemu pamakaburi kwani siwengi wenye kufahamika wapi walizikiwa hivyo haina ulazima. Haya ndugu kapumzike ila kwa sisi watu wa afrika ya mashariki na afrika kusini tunalia kilio cha ndugu yetu rafiki yetu Lucky Dube ameuawa tarehe 18 Oktoba, 2007 na majaambazi, Hivyo hatunae tena. Ahsante nd. Kipala mungu akijalia utakuta mabadiliko. --Muddyb Blast Producer 05:09, 20 Oktoba 2007 (UTC)
Nataka kujua
Salam Nd. Kipala, Pole kwa mapumziko yako ya siku kadhaa ila tu nasema karibu. Kuna vitu huwa na kawaida ya kuviona lakini sikufanyia kazi kabisaa yaani. Ni kuhusu hizi alama mbili za katika sehemu ya sanduku la kuandikia:
- Haya ni mabadilisho madogo
- Simamia ukurasa huu
Hizi ni zanini hasa nahitaji kufahamu naomba nifahamishe. --Muddyb Blast Producer 06:27, 22 Oktoba 2007 (UTC)
- Salamu sana; hizo zinafanya kazi kama ifuatayo:
- "Mabadilisho madogo" yatarajiwa kurahisisha matumizi ya orodha la "mabadilisho ya karibuni" kwa sababu huku utaamua kama unataka kuona mabadiliko yote, au bila mabadilisho madogo, bila Bots n.k.
- Simamia ukurasa huu: ukitaka kufuatilia maendeleo ya ukurasa wowote unabonyeza hapo. Sasa ukurasa huu umeandikishwa katika orodha lako la "maangalizi". Ukibofya juu kwenye "maangalizi yangu" unapata orodha ya mabadiliko katika siku zilizopita kwenye kurasa zote ulizoandikisha humo. (inawezekana kurasa ulizoanzisha zimo hata hivyo bila kufanya kitu - sina uhakika). --Kipala 07:57, 22 Oktoba 2007 (UTC)
- Salamu sana; hizo zinafanya kazi kama ifuatayo:
Sija jaribu bado kwasababu sijaimalizia vizuri. Ile template inataka utulivu sana ili uweze kuifanya makini, Ila kama unataka tuifanyie kazi basi hata sasa hivi tunaweza kujaribu je upo tayari wa hilo?--Muddyb Blast Producer 11:19, 22 Oktoba 2007 (UTC)
Haya njoo hapa
It seems your quitely busy mr. kipala is it?--Muddyb Blast Producer 12:34, 22 Oktoba 2007 (UTC)
asante kwa picha ya Eisenhower
Asante, Kipala, kwa kuongeza picha kwenye makala ya Dwight D. Eisenhower. Nilitaka kuitafuta kwenye wiki commons, bahati mbaya nikakatika kutoka mtandao nikashindwa. Baada ya kuongezewa picha naona, makala siyo 'mbegu' tena. Ndiyo maana nilitoa mstari wa 'mbegu'. Wasalaam, --Oliver Stegen 13:04, 22 Oktoba 2007 (UTC)
Kipala upo? Tafadhali naomba angali hii na hii--Muddyb Blast Producer 14:42, 22 Oktoba 2007 (UTC)
Unaweza kuamini hii template nimeunda kwa dakika saba tu nikafanikiwa kuweka kila kitu na sijarudi nyuma. Kuna kitu sijafurahia kidoogo: Unajua lile jina halipo kati yaani kama limeshuka kidogo, Hebu jaribu kuangalia utaona kama limeshuka halijakaa kati je hilo nalo litakuwaje? Naomba nijibu hapa hapa kwako wala usijali--Muddyb Blast Producer 14:53, 22 Oktoba 2007 (UTC)
- Tuendelee kwa Angelina Jolie --Kipala 14:59, 22 Oktoba 2007 (UTC)
Tuendelee humu tafadhali.--Muddyb Blast Producer 15:15, 22 Oktoba 2007 (UTC)
Kipala upo? Tuendelee. --Muddyb Blast Producer 15:21, 22 Oktoba 2007 (UTC)
Angalia nimefaulu. Nilikuwa na comparison na ile template uliojenga template msanii muziki na hii hapa nika gundua katika ile sehemu ya jina {{{jina}}} arafu {{{jina}}} paliwekwa alama ya <br> badala ya | hivyo ikawa inashusha chini jina badala ya kuweka kati, Mimi nikafuta br nikaweka | nikaona mambo safi. Ahsante kwa msaada wako najua kitendo cha kuniachia mimi niunde Template kimeniofanya niweze kuzisoma HTML vizuri na kuzielewa kila lakheri.--Muddyb Blast Producer 15:38, 22 Oktoba 2007 (UTC)
Salam Nyingi Nd. Kipala, Kuna kasoro nimeziona katika hii Template Filamu, Kama vile inasogeza chini maandishi, Yaani haianzi sawa kama template zingine yenyewe kama inashuka na maelezo yote. Ili ujue hili angalia hii. Kisha ni jibu kuhusu hili tafadhali.--Muddyb 08:13, 23 Oktoba 2007 (UTC)
Salam nyingi Nd. Kipala, Mimi nilikosea kidoogo kukufahamisha kuhusu Template ipi iliyokuwa bado inanipa tabu. Ilikuwa kuhusu template ya Muigizaji ndio yenye kuleta tabu, Sema jana sijakuelewesha vizuri. Kuhusu template filamu nilkuwa bado naiweka sawa kidogokidogo sikuwa na haraka nayo sana kama hii ya muigizaji hivyo nilikuwa naisahihisha taratibu. Naomba nisamehe kwa usumbufu niliokupatia mzee wangu. Sasa kuna suala lile ambalo ndio nilikuwa nimelilenga haswaa, Ni kuhusu Template Muigizaji: kwanini inashuka chini kidogo? yaani hianzi juu maelezo yake, Template na maelezo yote yanashuka chini kidogo, Je hili pia unaweza kulichunguza japo kwa dakika kadhaa? Naomba unifahamishe juu ya hili.--Muddyb 05:56, 24 Oktoba 2007 (UTC)
Salama, Je upo? Kama upo naomba uje tuendelee--Muddyb 12:48, 24 Oktoba 2007 (UTC)
Twaweza Template talk:kuendelea mkubwa wangu. --Muddyb 14:15, 24 Oktoba 2007 (UTC)
Majibu ya Kiwamba Picha
Angalia majibu yako tafadhali. Sasa namimi umefika muda wa kwenda nyumbani kesho asubu nitakuja kufanya maarifa ila umeamini kama niko naelewa vitu vizuri kabisa. kisha ninaswali nataka nikuulize: Kwani Nd. Kipala ulishawahi kuwa mwalimu? na kama ulikuwa mwalimu basi ulikuwa unafundisha kwa lugha gani? Manake kila unapo nipa maelekezo huwa sirudi nyuma ni kwenda mebele tu, Kisha yale maelekezo yana andikwa vizuri kiasi kwamba usipoelewa basi hujue kuna mkono wa mtu. Ni jibu tafdhali maswali yote ya kwenye Template na hapa kwako. Samahani kwa maswali yasikuwa na msingi. --Muddyb 15:38, 24 Oktoba 2007 (UTC)
Habari Nd. Kipala, Ninaswali kidoogo sivibaya sana kufahmu vitu vinavyo husu Wikipedia. Hii Template:Swen inashughulika na nini? Nahitaji kufahamu kuhusu hii template. --Muddyb 07:26, 25 Oktoba 2007 (UTC)
- Sijui. Inaonekana kama kitu kisichokamilika. Kazi fulani kuhusu Swahili na English? --Kipala 08:10, 25 Oktoba 2007 (UTC)
Jamani, Maajabu gani haya. wewe ndiyo uliotengeneza ile template, Inaonekana hivyo kwa mujibu wa Wikipedia jumuia kwamba wewe uliumba template swen. lakini sikufamu lengo kuu hasa nini la kuiweka ile Template. Je unalolote la kusema juu huu ushaidi au ndio TOP SECRET?--Muddyb 08:20, 25 Oktoba 2007 (UTC)
- Sijatengeneza. Angalia historia ni Matt Crypto. Nadhani hasa kati ya templeti kuna maiti kadhaa ambazo hazikuzikwa kwa sababu tumejaribu-jaribu. Hii imewahi kutumiwa mara mbili tu - angalia "Viungo viungacho ukurasa huu" upande wa kushoto. Sioni faida yake. Nadhani Matt alicheza tu nayo kidogo. --Kipala 08:39, 25 Oktoba 2007 (UTC)
Samahani kidogo kuna swala nataka kufahamu, na wewe pia inabidi uulizie kuhusu hili. Ni kuhusu neno (Kinanda-Key Bord) Katika kumbukumbu zangu za kuangalia vipindi vya TV vinavyohusu Kompyuta kinachorushwa na televisheni ya Channel ten ya mjini Dar es salaam, Kipindi kinaitwa "RIGHT CLICK" wao huwa wanazungumzia vitu vyote vya kompyuta kwa kiswahili, Katika angalia yangu nikasikia Keybord jamaa yule ambaye ni mtangazaji kaitaja kama "Baobonye" (Key-bord) Mouse kaitaja "PUKU" je ipi sahihi Kinanda au Baobonye? --Muddyb 12:16, 25 Oktoba 2007 (UTC)
- Muddy nashukuru naona tutumie chako. Niko mbali hapa nategemea kamusi. Maneno ya kompyuta kuna orodha mbili za Chuo Kikuu DSM na pia cha Kadogo-kalaini (yaani microsoft) lakini haya yote ni nadharia na kutofautiana kati yao; kama watu wameanza kutumia lugha na kuamua tofauti na wataaamu wale basi tufuate kawaida ya watu. Nitasahihisha. --Kipala 12:52, 25 Oktoba 2007 (UTC)
Sawa yote kheri, Kwani hamna utofauti mkubwa saana, Lakini mie ndivyo nilivyosikia kutoka katika kikosi cha "The Right Click" walisema hivyo sasa sina uhakika saana kama wao ndio wanajua zaidi lakini siku zote wao Key bord huita "BAOBONYE" na mouse hita "PUKU" na vinginevyo vingi tu hutumia lugha yao kwa kiswahili. Sina mengi ahsante. --Muddyb 13:15, 25 Oktoba 2007 (UTC)
Ndugu, Tuendelee hapa --Muddyb 14:10, 25 Oktoba 2007 (UTC)
Huja ni jibu bado. Tafadhali jibia hapa--Mwanaharakati 15:00, 25 Oktoba 2007 (UTC)
Lugha ya Kompyuta
Salam Nyingi Nd. Kipala, Mhhh, ni kweli kunaulazima wa kuingiza Category:Lugha ya Kompyuta, Kwasababu mimi bado naifutlia hiyo lugha ili tuweze kuwa na lugha rasmi. Kwa upande fulani ikiwekea jamii ni vizuri iwe inajitgemea ili mwingine akitaka kujua atapitia katika hiyo jamii. je wewe unaonaje?--Mwanaharakati 06:30, 26 Oktoba 2007 (UTC)
- JAribu tu halafu tuone. Jamii peke yake haifai, lazima kuiingiza katika jamii ya juu. Lakini hata inawezekana kuiingiza katika jamii mbili za juu (komyuta na ?? Lugha??) -- Leo hutanikuta tena - (kipala) --62.154.201.129 08:20, 26 Oktoba 2007 (UTC)
Sijakuelewa jamii ya juu vipi yaani, Kuumba makala yenye kuzungumzia lugha ya Kompyuta au umemaanisha nini hapo--Mwanaharakati 11:31, 26 Oktoba 2007 (UTC)
Hamna kitakacho tokea kama utachukua picha kutoka en:wiki?.--Mwanaharakati 13:49, 26 Oktoba 2007 (UTC)
Kwenye Wikimedia-Commons mimi kule ni mwanachama ila sina kawaida sana ya kwenda kule kupakia picha. Mfano sasa hivi nimepakia picha ya babangida kule, pia nishawahi kupakia picha za remmy na wengine wengi tu. Sema huwa sipendi kwenda kule kwasababu bakuona mbali kisha sina mazoea saana. hebu angalia hii http://commons.wikimedia.org/wiki/Image:Babangida20.jpg arafu unimbie vipi. kisha tazama hizi
--Mwanaharakati 14:03, 26 Oktoba 2007 (UTC)
- Swali si kama unapakia commns au la. Mimi sifanyi kwa kawaida mara chache tu.
- Ila tu ukinakili picha kwenye ukuasa huu wa biafra watakuuliza: je haki za picha umepata wapi? Na hapa mimi naona siku moja atakuja mwingine atakayekuambia: picha hii eleza haki umepata wapi. Pasipo na maelezo basi watafuta.
- Mimi niliwahi kupakia picha aina ya tingatinga niliyonunua Dar ninayo nikapakia kwa makala ya de:wiki wakafuta kwa sababu sikuweza kusema ya kwamba mchoraji aliniruhusu kuionyesha mtandaoni kwa laiseni ya wikipedia (kwa sababu picha katika wikipedia inaweza kuchukuliwa na mtu yeyote na kutumiwa hata kibiashara - kwa kawaida mwenye haki ya picha ni yeye anayestahili asilimia yake katika faida kama mtu anauza au kuonyesha picha kwa faida...) --Kipala 15:02, 26 Oktoba 2007 (UTC)
Mhh jamani si hatari namna hiyo, Lakini picha za remmy niliweka wakauliza vipi, nikawajibu nimetoa maktaba ya nyumbani hawakusema kitu wakanyamza kimya na wakandelea kuicha mpaka leo hii. ila hii ya Babangida sijui kama itadumu!! si kitu sana. kinachotakiwa ni kufuata taratibu zote za wikipedia zinavyotakiwa kufuatwa. Nitafanya kama usemavyo kwani mie ni mwanawikipedia wa kweli niliye tayari kwa sharti lolote lile lenye kuhusu uendelezaji wa Wikipedia. Ahsante00Mwanaharakati 15:24, 26 Oktoba 2007 (UTC)
- Babangida yuko en:wiki si lazima kujitahidi penginepo. Vilevile wengine kadhaa.--Kipala 15:27, 26 Oktoba 2007 (UTC)
Haina tatizo hiyo tayari tumekwisha kubaliana There's no need to blame each other, let's think about something else apart with blaming or more instruction about the image. I really understood the sittuation so please let's talk about else things. Labda utanielewa maana kwa kiswahili nisha sema nitafanya kama wikipedia inavyosema but unaendelea kunipa vidonge tu Nd. vipi?--Mwanaharakati 16:31, 26 Oktoba 2007 (UTC)
- Nd Muddy sikutegemea kukulaumu. Habari ya picha nimetaja kwa sababu niliwahi kufanya kazi bure - kwa hiyo ujue unachofanya na usijisikie vibaya kama mtu anajitokeza anayeondoa picha. Menginevyo kuhusu kutazama wiki za lugha mbalimbali kwa picha: ni ushauri tu. Ni hayo tu hakuna fikra za siri. Halafu tufurahie kwa muda huu wikipedia yetu ndogo ambako tunaweza kuwasiliana kwa heshima. Tukikua sana na kuwa watu wengi ustaarabu utapungua tutaona vidonge kila siku. Hadi 10,000 nahisi itakuwa starehe --Kipala 16:46, 26 Oktoba 2007 (UTC)
Salam nyingi Nd. Kipala, Hamna neno ni kuelewana tu. Sasa naomba tusameheane juu ya haya yaliyotokea maana naona ushaandika "HESHIMA" hii ni misingi ya watu waoishio tofauti, wanatakiwa kuheshimiana hivyo ukiwa kama mkubwa wangu wa kazi pia kiumri nakuomba radhi kwa yote yalitokea. je umenisamehe? na kama umenisamehe nakuomba ufute hayo majadiliano ya juu yote yenye kuzungumzia mambo ya picha au waonaje?--Mwanaharakati 06:49, 27 Oktoba 2007 (UTC)
Salam, Umesusa?--Mwanaharakati 12:24, 27 Oktoba 2007 (UTC)
Help
- Hi! Can you translate this text onto Swahili?
- Almazán is a municipality located in the province of Soria, Castile and León, Spain.
- Thanks. --Jeneme 13:45, 28 Oktoba 2007 (UTC)
Salam nyingi Nd. Kipala, Sikuwa namaana ya kwamba nakimbia wikipedia la. Nilkuwa kidogo na kazi nje ya ofisi kama siku mbili hivi, Nilkuwa natengeneza muziki wa filamu ya "Msitu wa Majini". Niliteuliwa mimi kuwa ndio muundaji wa "Sound Track" hivyo sikuonekana kwenye mtandao kwa muda wa saa kadhaa tu. Kuhusu yale hayana neno kwani tumesha ya maliza pia nashukuru kwa message yako. Kila la kheri tupo pamoja na wiki yetu usijali.--Mwanaharakati 05:26, 29 Oktoba 2007 (UTC)
Salam, Ninaswali kidogo Nd. Kipala, japokuwa utakuwa umechoka na maswali yangu maana nimekuwa mtu wa kuuliza kila siku. Swali linahusu mie mwenyewe: Toka siku uliyonieleza namna ya makala inavyotakiwa iwe (Muundo wa Makala) vipi ninavyoandika, Upangaji wa makala zangu, Kueleweka n.k. je kuna badiliko lolote lile toka unielekeze. Hasa katika uandishi je taratibu za uhandishi zinafuatwa zinavyotakiwa? Tafadhali usisite kunieleza kasoro zangu nahitaji kujijua tafadhali. Siwezi kuwa nafanya kitu arafu sijui kama nakosea naomba msaada wako wa juu ya uandikaji wangu. Nieleze tafdhali.--Mwanaharakati 13:40, 29 Oktoba 2007 (UTC)
Samahani kidogo umeniacha mbali nini maana ya Tahajia? Spelling au Herufi? Maswali ya ziada:
- Kwani herufi kubwa haitakiwi baada ya koma?
- Kuhusu sentesi nikombioni kuweka sawa nalo. Ila kuwa na imani kama ulivyokuwa na vingene nitabadilika. Jibu maswali yangu tafadhali, kisha usisahau mie nimezaliwa Dar hivyo kiswahili cha hali ya juu siwezi hasa cha katika kamusi jitahidi kuandika lugha nyepesi kidogo.--Mwanaharakati 14:37, 29 Oktoba 2007 (UTC)
Salam Nd. Kipala, Kwa sasa niko najifunza namna ya kuandika sentesi nzuri katika makala za nchi mbali yaani nafungua kila nchi na kuanza kusoma. Katika nchi nilizofungua nakuzisoma na kuangalia historia ya kurasa kaandika naona mara escatbot siebot na wengine wengi tu bot, sasa hawa wakina bot ndio wakina nani?--Mwanaharakati 06:46, 30 Oktoba 2007 (UTC)
Ahsante sana.--Mwanaharakati 08:57, 30 Oktoba 2007 (UTC)
Sorry but I don't understand anything. Could you please talk in English????? --Jeneme 12:40, 11 Novemba 2007 (UTC)
- Sorry for you thats just the local language. Aqui la frase: Almazan ni mji mdogo wa mkoa wa Soria katika jimbo la Kastila-Leon la Hispania. --Kipala 15:17, 11 Novemba 2007 (UTC)
Ahsante
Ahsante sana kwa kunikaribisha. (en) but i know kiswahili little bit. --Suresh Kumar 05:49, 31 Oktoba 2007 (UTC)
Hatua ya Mwisho
Salam nyingi Nd. Kipala, Kama unakumbuka ile zana ya filamu ilyokuwa haijamaliziwa, mimi tayari nishamaliza lakini kuna baadhi ya vitu vimekosekana, vitu hivyo ni kama vifuatavyo:
- Kuna baadhi ya rangi hazitaki kuoneka mfano: Golden na khia hizi bwana haziji kabisaa, sasa sijafahamu ni nini kinachosababisha, labda zimetiwa kilema (Disabled) ili zisifanane za en:wiki au namna gani siujui nini hasa kimetokea.
- Kuna baadhi ya maelezo niliyatoa kutokana kila nikifanya jitahada ya kutaka jedwali dogo na kubwa kufanana lakini zikawa zinalumbana hali ya kuwa zote ni sawa, labda wewe ujaribu kuongeza baadhi ya hizo zilizobaki maana ni muhimu sana, zilizobaki ni: Bajeti ya filamu, Mapato ya filamu, Ilitanguliwa na, Ikafuatiwa na, Tovuti. Je unashauri lolote lile kuhusiana na hili?--Mwanaharakati 07:15, 31 Oktoba 2007 (UTC)
Salam Nd. Kipala, Ahsante kwa kunihamasisha juu ya Halima mdee, je hawa vipi? Ni kuhusu sentesi na msingi ya uhandishi halisia yaaani NUKTA na KOMA naomba unieleze ili niweze kufanya juhudi zaidi. Wahusika ni kama wafuatavyo:
Nd. Kipala kama usingesema kuwa nakosea katika uhandishi wa sentensi basi nisinge badilika, sasa sijui ingekuwaje. Tafadhali soma hizo makala kisha nifahamishe. Wako katika ujenzi wa Wikipedia.--Mwanaharakati 07:45, 1 Novemba 2007 (UTC)
- Hilo nalo neno. Mwanzoni sikuwanafikiria namna ya kuandika wake wote kwa ufupi, pia sikuwa nafikiria kuacha sehemu zisizo na ulazima wa kuweka kiougo cha huyo mzungumziwa. Tafsri inakuja kila unapokosea ndio marekebisho yanakuja. Ahsante kwa mchango wako.--Mwanaharakati 12:56, 1 Novemba 2007 (UTC)
Template Tuzo
Salam Nd. Kipala, kuna zana nyingine nimeiumba jana sasa nahitaji maridhiano baina ya mkabidhi na mtumiaji. Chochote kile kinachoumbwa ndani ya wikipedia basi si cha binafsi tena, kwani kikiundwa kuna watu watatumia!! sasa naomba uangalie maelezo yake kama yako sahihi basi sawa, ila usisahau kunijibu juu ya hili. Template tuzo--Mwanaharakati 06:22, 2 Novemba 2007 (UTC)
Sidhani kama nilikosea kuomba shauri lako. Unaweza kurekebisha ili iweze kuwa bora zaidi. Uko huru kuirekebisha sizani kama utakuwa unakosea. Weka sawa tu. kisha jibu hapa.--Mwanaharakati
Salam Nd. Kipala, leo ilikuwa siku ya kuendeleza na kuondosha ule uwekundu uliokuwa katika makala ya Spaghetti Western. Kwa siku ya leo nimejaribu kuzipunguza baadhi ya rangi nyekundu zlilkuwa zinaleta sura mbaya. Kesho nikipata muda tena, nitaendeleza watu waliobakia, lakini kwa leo mmhh, hatari makala sita, sio mchezo. Tuombeane uzima ili tuweze kumalizia nngwe ile iliyobakia. Ahsante, wako katika ujenzi wa Wikipedia.--Mwanaharakati 17:15, 2 Novemba 2007 (UTC)
, naomba uiandikie makala hii:Arsenic, nataka kuijua kwa undani zaidi. Kwakuwa wewe ndugu kipala ni mtaalamu wa masuala ya kemia, basi naomba nisaidie hili. Inapatikana katika en:wiki Arsenic, http://en.wikipedia.org/wiki/Arsenic . --Mwanaharakati 15:42, 3 Novemba 2007 (UTC)
Salam, Nd. Kipala, kuna baadhi ya maandishi huwa yanaandikwa kwa ufupi, ila sijafahamu yankuwa na maana gani, mafano: 1910 AD au 10 AD. Haya yana maana gani? Achia hayo kuna hizi KK nazo je?--Mwanaharakati 06:16, 5 Novemba 2007 (UTC)
Ucheki
Salam Nd. Kipala, kuna jambo kidogo nataka kushauri. Ni kuhusu makala ya nchi ya Ucheki, hii kwetu sisi hatuijui kama ucheki, wengi tunaijua kwa kuitaja kama "Jamhuri ya Czech" hivyo ndivyo tunavyoita watu wa Tanzania. Kuna siku nilipata tabu sana kuitafuta hii Czech, nikiangalia katika makala hamna, nikijaribu labda jamuri ya Czech nayo hamna, mpaka ikabidi niitafute katika yahoo sachi ndio nikaipata katika sw-wiki imeandikwa Ucheki. Nashauri hii makala iredirect-we katika Jamhuri ya Czech, hii itakuwa rahisi kwa watu wengine wasiofahamu hii Ucheki. Mimi binafsi tayari nimesha redirect jina la nchi kamili Czech, ila tu naomba samahani kwa kuto toa taarifa juu ya hili. Huu ni ushauri tu. wako katika ujenzi wa wikipedia.--Mwanaharakati 16:03, 6 Novemba 2007 (UTC)
- Muddy, sielewi ulikuwa na tatizo gani? Ulitafuta jina gani? Ukiandika "Czech" kwenye dirisha la "tafuta" unafikia mahali pake mara moja bila tatizo. Nakubali ya kwamba magazeti yanaweza kuandika mara nyingi "czech" lakini sijui watu wanaisoma na kutamka namna gani? Asiyejua atakosa au sivyo? Kwa sababu herufi za Kiswahili yana matamshi tofauti kuliko yale matamshi ya Kiingereza yaliyokuwa kawaida. Pendekezo la TUKI ni "Cheki au Jamhuri ya Cheki". "Ucheki" ilikuwa njia yangu ya kuifupisha. Nimeongeza tahajia ya "czeck" kwenye mwanzo wa makala pia kiungo kwa "Jamhuri ya Czech". Sijui kuna bado njia nyingine kutamka nchi hii? Kwa sasa ukitafuta Czech, Jamhuri ya Czech, Cheki, Jamhuri ya Cheki unafika kwenye makala ileile. --Kipala 16:52, 7 Novemba 2007 (UTC)
Salam, hapo itakuwa rahisi. Katika kumbukumbu zangu nakumbuka kwamba kila nchi mlioandika, mlikuwa mnaweka aina zote za utajaji wa nchi, ikiwemo kwa Kiingereza, Kiswahili hadi lugha ya nchi inavyoita. Si kitu, najua ulipitiwa tu na hili. Mengineyo:
- Nimeumba template mtu, hii unaweza kuingalia kama inafaa, kuanzia tahajia n.k.
- Naomba uangalie makala ya Steve Biko, maana huko ndiko nilikofanyia majaribio ya Template mpya. Kingine huyu mtu si mtu wa kawaida, ni mwanahistoria katika moja kati ya viongozi wakubwa wa Afrika, hivyo inabidi makala yake isiwe ya mchezo mchezo. Tafadhali naomba angalia makala hiyo kisha uniambie kipi cha kuweka sawa. Wako katika ujenzi wa wikipedia.--Mwanaharakati 05:33, 8 Novemba 2007 (UTC)
Template:Msanii muziki
Salam nyingi Nd. Kipala. Bwana Kipala Template:Msanii muziki imepatwa na mushkeli kidogo. Nashindwa kuelewa ni nini kilifanyika kabla ya kuhifadhi kurasa. Inaingiiliana na ile Template:Muigizaji (Kwenye jedwali dogo) Template:Msanii muziki, lakini jedwali dogo ni Template:Muigizaji, sasa hapo bado sijafahamu kwanini imekuwa vile. Naomba uangalie hili.
Mengineyo: arafu naomba hii Template:Msanii muziki uruhusu ile hiyari ya rangi (colour option) manake ile rangi moja haipendezi. Ni ombi unaweza kufanya hivyo pindi upatapo muda, ukiona muda huna basi fungua zile semi-protect kisha nijulishe mimi nitashughulikia mara moja. Kazi njema bosi. --Mwanaharakati 08:53, 13 Novemba 2007 (UTC)
Ahsante nimeona marekebisho yako. Kichekesho: Unajua ile tabia ya kuweka InterWiki katika makala, huwa na kawaida ya kumpa kipaumbele yule anaenisaidia katika ujenzi wa makala ninazojenga. Kila makala ambayo inataka InterWiki, basi nitaanza na Kiingereza pili wale jamaa wanaoita mtumiaje kwa lugha yao "Benutzer" kwakuwa wao ndio wanaonipa maarifa ya juu ya ujenzi wangu wa Wikipedia, huoni raha ilioje hiyo. Natumai utakuwa nafaraja nyingi. Siku njema.--Mwanaharakati 11:51, 14 Novemba 2007 (UTC)
Salam Nd. Kipala. Nimesha sogeza Template jiji kwenda Mji, je waonaje?--Mwanaharakati 04:41, 16 Novemba 2007 (UTC)
Barnstar
Salam Nd. Kipala, naomba unipe dondoo za hii Barnstar. Nataka kujua lengo kuu la kuweka Barnstar manake nimekuwa mtu wa kuona tu. Je katika Sw-wiki hamna hii Barnstar hebu nifahamishe nini lengo. --Mwanaharakati 12:40, 17 Novemba 2007 (UTC)
Jericho Rosales
Salaam ndugu Kipala. Ningekushukuru mno kama ungenisaidia kurekebisha makala hii ya Jericho Rosales katika templeti niliyotumia. Ndani ya hiyo templeti kuna maandishi yamejitokeza katika mabano. Sasa templeti ninaitaka katika kazi yangu ila maandishi yale siyahitaji pale. Nimeshindwa kufurukuta mzee. --Mwanaharakati2
Barnstar
Salam Nd. Kipala, nimekuelewa. Lakini waonaje na hapa sw:wiki tukianzisha utaratibu huo wa Barnstar kwa kutumia jina lingine lolote kama walivyofanya wenzetu wa Ujerumani, Ufaransa, Hispania n.k kwani itakuwa inaleta mostisha kidogo kwa wachangiaji au wewe waonaje?--Mwanaharakati 11:29, 19 Novemba 2007 (UTC)
Ahsante, wacha kwanza nitafute nembo ambayo itakuwa nzuri yenye kupendezesha wiki yetu, nikiipata au nikikosa nitakueleza nini kimeendelea juu ya hiyo nembo. Ukiona uifanye wewe ni kheri ila mie nitajaribu niwezavyo nikishindwa basi, ila jitahada zinatakiwa sana. Mengineyo:
Unajua toka nije sw:wiki, nahisi kama lugha yangu imebalika kidoogo, hata katika kuongea kwangu mtaani, kazini n.k. Ile tabia ya kuchukua makala kwa en:wiki au simple:wiki, na kuitafsri, imesababisha kupanuka kwa lugha ya Kiingereza, sasa nikisoma makala kwa Kiingereza naelewa mara moja kulikoni ilivyokuwa mwanzoni. Hii ni faida moja wapo hivyo katika wikipedia ni sehemu ya kupanua maarifa.
Japokuwa unajiona kama vile unafanya kazi ya bure, lakini ujue maarifa yanakuwa ya juu mno ni tofauti na kuanza kuchati na watu au kufungua tovuti zisizoeleweka. Kwakweli wikipedia imenisaidia kwa mengi na ndiomaana kila siku nipo lazima niingie japo kwa nusu saa au masaa matatu. Nd. Kipala, nashukuru kwa msaada wako kwa kipindi chote nilichokuwa nachangia makala hapa wikipedia.
Hujawahi kunidharau hata siku moja pale nikuombapo msaada wangu, hasa katika ujenzi wa template, badala yake ukanifundisha namna ya kujenga template ili niweze kufanya mwenyewe pindi tu nihitajipo template kwa kazi husika. Kitendo hicho kilipelekea mimi niwe na imani kubwa na wikipedia, nikawa najisikia faraja pale nichangiapo makala katika wikipedia. kusema kweli nimebadilika sana kupita kiasi, hivi ninavyo andika hivi sasa, mwanzo sikuwa hivi ila tu bwana Kipala juhudi zako zimepelekea mimi kuwa hivi. Nd. Kipala ahsante sana. --Mwanaharakati 13:30, 19 Novemba 2007 (UTC)
Naomba ufute hivi vitu
Salam Nd. Kipala. Naomba futa template hizi zifuatazo:
- Template:Wasanii
- Template:Tarehe ya kuzaliwa
- Template:InterWiki
- Template:Infobox Film
- Template:Image class
- Template:Daraja la picha
- Template:Wiktionarylang
Hayo yote yaliyojiri hapo juu, nilifanya mimi. Natunguliza kuomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.
--Mwanaharakati 15:18, 21 Novemba 2007 (UTC)
Salam Nd. Kipala. Maarifa yamepungua kidoogo. Lakini usinicheke. Kuna maneno kidogo yameniletea utata, nilijaribu kuyatafuta katika kamusi ya Yale, lakini sikufanikiwa kwa hilo. Sasa naomba msaada kwako huku nikiwa na matumani kibao yaliyojawa na furaha ndani yake. Maneno hayo ndugu yangu ni haya hapa:
Death and aftermath.
Sana sana hilo aftermath, death najua ila hilo aftermath ndio kizazaa kwangu. Nipe maana yote kwa ujumla. Sina mengi, wako katika ujenzi wa wikipedia.--Mwanaharakati 06:36, 23 Novemba 2007 (UTC)
Salam. Natumai hii makala umeiona, sijafanya hajizi kwa nd. huyu. Tayari nimesha mtumia E-mail afanye marekebisho juu ya kurasa hiyo. Maelezo hayo ni kama ifuatavyo hapo chini:
Salam nyingi Nd. Pheniuas Ndayishimiye.
Yah: kuweka makala Email ya steven kanumba katika Wikipedia.
Ndugu yangu Pheniuas, upo uwezekano wa kukusaidia juu ya hili tatizo lako kwakuwa mimi ni kijana ninayeishi Dar es Salaam. Lakini kuna jambo ulilofanya katika Wikipedia, kuweka lile ombi lako katika sehemu ya makala.
Kwa jinsi inavyotakiwa maelezo kama yale yanatakiwa yawe katika ukurasa wa mtumiaji (user page) na sio sehemu ya kuwekea makala. Hivyo kuna hatari ya kufutwa yale maelezo, labda uchukue hatua haraka iwezekanavyo ya kuondosha yale maelezo katika sehemu ya makala.
Nd. mpendwa Pheniuas unaombwa ufanye mabadiliko katika kurasa ile haraka iwezekanavyo kabla Wakabidhi hawaja chukua hatua yoyote ile dhidi ya makala ile. Ushauri:
- Unaushauriwa uwe mwanachama ili uweze kutambulika katika kazi zako.
- Ni vyema maelezo kama yale uwe unaweka katika ukurusa husika wa majadiliano wa katika huyo mtu unae mtaka, au kuweka sehemu ya mtumiaji (user page).
je upo tayari kwa hayo? Basi kama upo tayari hebu fungua hapa ili uweze kujisajili katika Wikipedia.
Natumai utakuwa nafuraha tele moyoni ukiona twasaidiana katika haya. Wako katika ujenzi wa Wikipedia Muddyb Blast Producer au Mwanaharakati wa Wikipedia.
Sidhani bwana Kipala kama nitakuwa nimekosea juu ya hil. Endapo utaona nimekosea basi nisamehe kwa hili. Wako katika ujenzi wa Wikipedia. --Mwanaharakati 06:13, 24 Novemba 2007 (UTC)
About Soria (Spain)
Can you make a category called "Municipalities of Soria" please? --Jeneme 14:17, 25 Novemba 2007 (UTC)
Salam nyingi Nd. Kipala. Samahani naomba ufute hizi kurasa zilizoingia kwa bahati mbaya. Nilikuwa nataka ku-redirect jina la Benjamin William Mkapa kwenda Benjamin Mkapa. Ili nilazimu kufanya hivyo kutokana na makala ya aliyekuwa makamu wa rais wa Tanzania, Nd. Omar Ali Juma, hivyo nikajikuta naingiza kurasa ikiambatana na NUKTA, naomba uondoshe hii kurasa.
--Mwanaharakati 10:38, 28 Novemba 2007 (UTC)
Vielen Dank für deine Unterstützung an meinem Artikel über den Ort Breinigerberg. Falls du noch irgendwelche Ideen hast, wie man ihn verbessern könnte - ich freue mich über Anregungen. Gruß --BBKurt 00:03, 1 Desemba 2007 (UTC)
Salam. Nimeona Nd. Kipala ila tu nashukuru kwa kunikumbusha tena na tena. Leo nimemuakia mama yake Jane Fonda na Peter Fonda, hivyo nishamaliza kumuelezea. Kazi njema.--Mwanaharakati 13:11, 1 Desemba 2007 (UTC)
Christiaan Barnard
Haya maelezo yako sawa? Maana kama naona hii ni sehemu ya Jamii kwa Kijerumani au nimeelewa vabaya? Maneno yenyewe haya hapa:
Kategorien: Mann | Südafrikaner | Chirurg | Geboren 1922 | Gestorben 2001 | Mediziner (20. Jahrhundert)
Tazama kwa umakini labda mie sijaelwa vizuri ni nini kinaendelea.--Mwanaharakati 13:27, 1 Desemba 2007 (UTC)
Bamba
Katika swala la lugha kuna kuwa na utata kidogo. Ni vyema panapo andikwa maneno ambayo wengine hawato fahamu, pakawekewa mabano kwa Kiingereza, ili iweze kurahisisha. Kwa maana ya kwamba! Si wote wanaojua Kiswahili sanifu! Mfano neno Bamba lina maana gani? Mimi sikuelewa ila tu nahisi itakuwa Delta kwa Kiingereza (ila sina uhakika kwa hilo na ndio maana nikaona bora tuwe tunaweka mabano kwa Kiingereza ili kurahisha) kwani hata baadhi ya wazungu hawajui haya maneno, hivyo ukiweka mabano na wao pia wanapatakujua. Hii ni faida kwa wote watakao soma makala za wiki kwa Kiswahili. Ushauri wangu unaonaje? Si kwa maneno yote ni baadhi ya maneno ambayo yataonekana kama yana utata fulani hivi. Ahsante.--Mwanaharakati 05:06, 3 Desemba 2007 (UTC)
Naona itakuwa bora kinamna fulani. Ni vema kuweka maneno mawili mawili ili kurahisisha. Ni kweli si wengi wanao soma habari za katika mtandao wanajua Kiingereza, vile vile si wengi wanaojua Kiswahili cha ndani kama fikra zilizopo. Ila naamini wengi tunaotembela mtandao kidogo tuna uhauweni wa Kiingereza. Si kitu, ni bora kuweka njia mbele ili tukuze Kiswahili chetu. Pia vile vile kurahisisha kunako takikana ili kupata mawasiliano rahisi je waonaje?--Mwanaharakati 13:43, 3 Desemba 2007 (UTC)
Lubumbashi
Kipala, Salam. Naomba uendeleze hii makala Lubumbashi. Kuna mtu aliiweka lakini hakuandika chochote zaidi ya kujitambilisha mwenye kama yeye ni nani. Mie nikaona nifute maelezo yake na kuanza kuweka mji wa Lubumbashi (Kongo) kama unavyojua tena ndugu yako katika jiografia mimi sio mzuri sana kama katika masuala mengine (muziki na filamu). Hivyo ndugu yangu naomba uendelee kama utapata muda. Sina uwezo mkubwa wa kuindeleza zaidi ya hapo nilipokia, na hiyo ilikuwa ni kuweka sawa mambo. Arafu kwani hamna uwezekano wa kuzuiya watu wasio jiandikisha kuchangia makala? --Mwanaharakati 15:55, 3 Desemba 2007 (UTC)
Unbelievable things
Salam Nd. Kipala. Imefanya vizuri sana (hongera - sema hatuna tuzo ninge kupa tuzo). Sasa hapa naona tumeelwana kuhusu swala la lugha. Umefanya vizuri sana kutoa mifano, maana kila unapo taja neno umeweka na neno (yaani kitu fulani- hapa natumai kila kitu kitakuwa sawa) vifuatavyo ni chuki binafsi na si kingine maana kila kitu swafi. Ukizungumzia mifano iliyoelweka basi hii imefunga dimba. Sitegemei kurekebisha chochote pale maana kila kitu kipo sawa. Tukaze mwendo wandugu!! Ila kwa hii we acha tu.--Mwanaharakati 16:33, 4 Desemba 2007 (UTC)
Wiki za Afrika
Kipala, Salam. Katika siku mbili hizi nilikuwa nafanya matembezi katika baadhi ya wikipedia za nchi tofauti za kiafrika, nikakuta nyingi bado hawana mambo mengi mno. Hapo awali wakati naanza kuingia sw:wiki, ule ukurasa wa mwanzo uliandikwa: Karibu katika wikipedia ya Kiswahili, hii ni kamusi elezo ya pili kwa ukubwa afrika, baada ya wikipedia ya afrikaans.
Hilo kwa kweli nilibisha, niliona kama tunajikweza, kumbe hiyo ni kweli kabisaa. Ukiangalia wikipedia ya rw:wiki ndio kwanza wana makala 104, ukiangalia kg:wiki hata ile kurasa ya mwanzo hawana, wala yule mkabidhi wao nae hamna kitu, sio kama majungu, mimi huwa na kawaida ya kuangalia sehemu ya kurasa mpya ndipo nikakuta makala fupi iliyo andikwa na mkabidhi wa kg:wiki (bwana ???) hata akuweka (Stub- Jamii) wala nini. Mhhh, Nd. zangu, sisi tupo mbali mno kuliko nilivyokuwa nafikiria.
Nilijua hilo baada ya kufanya utembezi katika wiki zingine za kiafrika. Pongezi ina stahili kuwepo kwa wanawikipedia wote wa Kiswahili, na tuwape pole wenzetu wasio na hata msaada wa kuweza kuchangiwa. Katika kg:wiki mchangiaji ni mmoja tu, ni yule mkabidhi wao hamna tena mwingine, sisi hapa wapo watu wengi sana, japokuwa wana changia siku moja moja, lakini bado wapo, wenzetu wa kg:wiki hamna hata wa kuchangia hata wa siku moja, je hatu stahili hongera?--Mwanaharakati 15:41, 7 Desemba 2007 (UTC)
Idioma-bot
Hi. Ooops, I confuse users and last time wrote to Matt Crypto instead writing to you (http://en.wikipedia.org/wiki/User_talk:Matt_Crypto#Idioma-bot_on_sw_wiki). Now I stopped my bot work and go to ask for bot flag to your bureaucrat. Regards, lt:User:Hugo.arg 21:26, 11 Desemba 2007 (UTC)
Kipala, salam. Ahsante kwa jibu lako. Lakini sijakupata kidoogo katika sentensi ya mwisho: Humjuimwalimu anayependa kujaribu kitu pamoja na wanafunzi wake? Hiyo ndiyo nafasi ninayosubiri. Naomba nifafanulie huu msemo umemaanisha nini?--Mwanaharakati 13:05, 12 Desemba 2007 (UTC)
Halo halo, naona kwa kwetu itakuwa kama ndoto. Si kitu, ni kumshukuru mungu kwamba baadhi ya watu tupo tuliojitolea kuindeleza lugha yetu katika mtandao huu wa wikipedia. Pia tunaomba mungu watokee wengine watakao pata muda wa kufanya hivi tunavyofanya sie tuliopo. Vile vile Tanzania bado tupo nyuma kidogo katika kutoa msaada wa kitu chochote (a. ni bora mtu afungue mitandao ya ngono, muziki, mpira n.k kulikoni kuja kuchangia makala katika wikipedia- hamna faida. b) wengi wanafikiria mnao pata faida ni nyinyi na wala si yeye labda mgao upite kote kote tena kwa vihakikio kwamba atalipwa. c) si wote tuliokuwa tunapenda kuperuzi masuala ya maisha ya watu au kitu fulani katika mtandao, na hata hao wenye kuperuzi vile vile wanakasumba ya kutopenda kutoa msaada hata wa dakika 5. Ni hayo tu sina mengi ila naamini mambo yatakuwa sawa, kwani hata mimi nyie hamja nitegemea kama nitakuja kuisadia wikipedia. Na pia ndugu zangu nawaomba tupeane kheri katika maisha kwani watu tulio na fikra kama zetu ni wachache sana Tanzania, hivyo na waomba mvumilie kila kitu kitakuwa sawa. Nilijaribu kumvuta mmoja (SideMontero) na akaweza kufanya mawili matatu katika wikipedia, lakini bado anaonekana haja sadiki ki-sawa-sawa. Si kazi ndogo kumfanya achangie makala bila hata ya malipo, sisi wengine ni watu wa kupenda wazungu wasio wabagua Waafrika, mfano:Kipala, Oliver, Marcos na wengine wengi tu mlio tuvutia hapa sw:wiki, au waonaje?--Mwanaharakati 14:21, 12 Desemba 2007 (UTC)
kama ndoto niko na wewe. Tuombe mungu labda mambo yatakuwa sawa. Na maisha ya siku hizi hamna hiyo kitu ya kusema eti nitalipwa akhera (thubutu ???? anaweza hivyo - maisha magumu) ila kwa imani tunayo ya kwamba watakuja wengine. --Mwanaharakati 15:18, 12 Desemba 2007 (UTC)
Sw:wiki katika dirisha la tafuta la nje
Salam nyingi sana Nd. Kipala. Kuna pendekezo nimeona litakuwa bora kwa wiki yetu pia ikiwa na suala kama hilo. Ni katika dirisha la tafuta kutoka mtandao mwingine mfano yahoo au google. Wiki yetu inaonyesha:
Wanaweka jina kisha wanaandika: Ibrahim Lipumba- Wikipedia, the free encyclopedia, ya kwetu, Ibrahim Lipumba - Wikipedia. Je hamna uwezekano wa kuiweka kama ya wenzetu? Maana ya kwetu inaonekana ya kienyeji mno ilhali ufahamu wa kuifanya iwe ya kimataifa upo kwanini tusiweke? Naomba jibu lako, na kama hujaelewa nitakufahamisha zaidi.--Mwanaharakati 11:39, 13 Desemba 2007 (UTC)
Nimemanisha hata kwa Kiswahili, wala sikuwa na haja iwekwe kwa Kiingereza. Mfano tafuta makala ya Scarlet Ortiz, katika yahoo, itakuja kwa wikipedia ya Kihispania huku wakiwa wameandika kama wenzetu lakini kwa lugha yao. Ila nimekuelewa kama hili haliwezakni mpaka Matt, na sio hilo tu kuna mengi kwetu hayaonekani. Ila hamna neno kama vipi Matt aambiwe tu, maana haiwezekani sisi tuwe nyuma kwa kila kitu.--Mwanaharakati 13:17, 13 Desemba 2007 (UTC)
Mengineyo: Viungo viungacho ukurasa huu, hii iandikwe:
Viungo viungavyo ukurasa huu au Viungo vinavyounga ukurasa huu.
Basi ni hayo tu niliojirisha katika chumba chako.--Mwanaharakati 13:57, 13 Desemba 2007 (UTC)
Kipala, salam. Nd. Kipala, kuna habari (haihusiani na wikipedia) nataka kukuelezea lakini nisinge penda habari hiyo iwe katika ukurasa huu wa majadiliano. Habari kamili naomba unilize kwa kupitia (muddybtz@yahoo.com) hapo nitakueleza kila kitu. Naomba ni jibu kama inawezekana.--Mwanaharakati 08:24, 15 Desemba 2007 (UTC)
Kipala, salam. Nimepata ule ujumbe wako ulionitumia katika barua pepe yangu, na vile vile umenijibu!! Safi sana. Ahsante na kila lakheri.--Mwanaharakati 13:39, 17 Desemba 2007 (UTC)
Mangosuthu Buthelezi
Kipala, salam. Naomba angalia hii: Mangosuthu Buthelezi. Kisha ufanye marekebisho kama yatakuwa yanahitajika!! Basi kila lakheri na usisahau kuelezea mabadiliko katika ukurasa wake wa majadiliano!! --Mwanaharakati 06:29, 22 Desemba 2007 (UTC)
Kheri ya Christmas na mwaka mpya
Nd. Kipla, salam nyingi kutoka Dar es Salaam, Tanzania. Ninapenda kukutakia kheri ya Christmas na mwaka mpya!! Japokuwa hujatakia mimi Eid Elhadji njema!! Kwa upande wangu ni salama tu, bado naendesha gurudumu hili la wikipedia. Kila la lakheri nd. Kipala.--Mwanaharakati 07:29, 24 Desemba 2007 (UTC)
Salam. Ndio nimekubali!! Lakini mie sina ujuzi sana wa dini yetu! Labda wewe kama utailezea sawa! Ila nitajaribu kusaidia mawili matatu ninayoyajua. Basi tuendeleee.--Mwanaharakati 05:37, 27 Desemba 2007 (UTC)
Hapo mara ya kwanza nilipo andika ujumbe huo wa juu, sikuwa nimefanya patrol katika ile sehemu ya kurasa mpya!! Ghafla naangalia kule, naikuta kurasa ulioniahidi kwamba utaiweka kama kitubio!! Ahsante kwa makala ile. Na hamna chochote cha kukielezea tena pale. Kazi njema.--Mwanaharakati 05:42, 27 Desemba 2007 (UTC)
Kipala, salam. Naomba angali makala hii: Magnificent Seven. Kisha uniambie nimefikia wapi hadi sasa!! Uandikaji, tafsri, sarufi na tahajia. Naomba nieleze tafadhwali. Basi ni mimi Nd. wako.--Mwanaharakati 14:36, 28 Desemba 2007 (UTC)
Airport - Uwanja wa ndege
Kipala, salam. Zamani ulikuwa unaitwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam. Siku hizi unaitwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. Hamna jina lingine zaidi ya hilo!! Ukisema kiwanja cha ndege sawa, ukisema uwanja wa ndege sawa wala hamna tofauti yoyote itakayopelekea hapo kuonekana lugha sio sahihi, kwani lengo ni lile lile tu. Habari zaidi: huja ni jibu swali langu la juu badala yake unaniswalika swali wewe. Ndugu mambo mengi au umepitiwa?--Mwanaharakati 10:38, 29 Desemba 2007 (UTC)
Si vibaya. Lakini hebu fanya tuone kwanza, kisha nitakwambia kama sawa au sisawa. Majadiliano ya hamie hapa--Mwanaharakati 12:15, 29 Desemba 2007 (UTC)
Kipala upo?--Mwanaharakati 13:27, 29 Desemba 2007 (UTC)
Ningependa zaidi unifahamishe wapi panapotwakiwa marebisho ili niweze kufanya kwasasa!!--Mwanaharakati 13:51, 29 Desemba 2007 (UTC)
Yale maelezo mazuri na yanapendeza pia yanafaa kuwepo katika eneo lile la makala husika. Lakini umetwanga maji kwenye KINU (ni bora ungebadilisha kabisa kisha maelezo yaje baadae). Kulikuwa hamna haja ya kuyaweka katika ukurasa wa majadiliano. Hapa tupo kwa ajili ya kufikisha swala katika jamii zetu kwa usahihi na kwa urahisi zaidi. Ni vyema tukiwa tunaafkiana kwa kila jambo. Lile lako limepita unaweza kuyaweka kwasasa. Tupo pamoja nafkiri, basi kama tupo pamoja, naomba tupa huo mchi na uache kutwanga maji katika KINU na kuanza kuiweka sawa ile makala kama muda upo, au unaonaje?--Mwanaharakati 14:54, 29 Desemba 2007 (UTC)
Muda umefika
Salam niyngi kutoka Dar es Salaam, Tanzania. Ndugu Kipala, ni muda sasa nimekuwa nachangia katika wiki hii ya Kiswahili, takriban miezi kama minne hadi sasa. Ingawaje nyie mnamika katika michango yenu. Muda umefika wa mimi kwenda shule!! Hivyo michango yangu itakuwa imepungua karibuni asilimia themanini za michangoi ya awali. Sababu zinazopelekea mie kuto changia sana kama awali ni kama ifuatavyo:
- Mwanzoni nilikuwa nikiingia kazini saa moja nanusu mpaka saa tatu na nusu asubuhi, huwa nafanya kazi ya wikipedia. Kuanzia hapo ni kazi ya kampuni hadi saa kumi na mbili na nusu narudi tena katika wikipedia hadi saa tatu usiku au saa mbili na nusu usiku.
- Kwa mwaka mpya nitaingia kazini saa moja na nusu na kutoka saa kumi jioni ili niweze kwenda shule. Hivyo itanilazimu kufanya kazi kama punda ili niweze kuruhusiwa kwenda shule!!
Katika wikipedia nitakuwa naingia kama kawaida japo kwa juma moja au kufanya patrol dhidi ya maharamia. Nitajitahidi ni malize nngwe zangu nilizo bakisha hadi hapo tarehe tano nitapoanza shule. Ndugu zangu wote wa wikipedia na washukuru kwa muda wote tuliokuwa pamoja katika kuijenga wiki hii!! Vile vile naomba mnitakie kheri katika kazi na shule pia nipate mafanikio mepesi ya kuelewa nifundishwacho!! Vile vile niweze kumudu sehemu zote za kazi, masomo na wikipedia pia. Kila lakheri na tuombeane kheri na bwana anipe nafuu ya kazi ili niweze kuweka michango yangu mikubwa hapa!!--Mwanaharakati 12:47, 31 Desemba 2007 (UTC)
Kipala, salam. Kwanza habari za mwaka mpya, maana naona leo siku ya pili toka mwaka huu uanze.
Naanza kwa kusema kwamba wikipedia kuikimbia au kuiacha itakuwa ngumu!! Nitakuwa kama kawaida lakini si kama mwanzoni nilivyokuwa nafanya kwa kuweza kuitumikia wikipedia kwa muda wa masaa yasiyopungua mawili na kuendelea. Nitafanya kazi zangu kwanza, kisha wikipedia inafuata!! Na muda wote ukinitumia msg kwa wikipedia naweza kukujibu!! Kwani nitakuwa hewani saa zote ila tu sitokuwa nachangia mara kwa mara. Kazini nitakuwa natoka mapema, hivyo sitegemei sana kama muda utatosha. Lakini kwakuwa hili bado jipya kwangu sitoweza kusema lolote kwa sasa hadi hapo nitakapo tulia. Ila naamini nitakuwepo kama kawaida japo kwa siku makala moja au waonaje?--Mwanaharakati 06:55, 2 Januari 2008 (UTC)
Swali la kiufundi
Salam, Kipala. Kuna jambo nimeona katika en:wiki. Katika ukurasa wa majadiliano wa kwao unapomaliza kuandika inatokea sehemu mbili, moja ya kurasa ya mtumiaji na pili ya ukurasa wa majadiliano ya mtumiaji aliokuachia ujumbe. Angalia: [[User:Muddyb Blast Producer|Muddyb Blast Producer]] ([[User talk:Muddyb Blast Producer|talk]]) au hii: http://en.wikipedia.org/wiki/User_talk:Belovedfreak#Thank_you_for_welcome-me kwa habari zaidi. Naona hii hii inarahisha mambo. Je hamna uwezekano nasisi tuwe kama wao?--Mwanaharakati 14:52, 3 Januari 2008 (UTC)
- Muddy, unisamehe lakini sijaelewa unamaanisha nini. Sioni jambo kwenye ukurasa uliotaja. Kitu gani inatokea sehemu bili, na sehemu mbili gani? --Kipala 16:24, 3 Januari 2008 (UTC)
Salam. Kikawaida unaponaliza kuandika jadilio lako si ni lazima uweke sahihi ya kuonyesha kama wewe ndio ulioandika!! Kwa wenzetu zinakuja sehemu mbili:
1. Jina la mwandikaji tar. na muda aliondika.
2. Sehemu ya majadiliano ya mtu aliyeacha ujumbe katika kurasa yako. Angalia mfano: (talk).
Kama nilivyoandika kwa mkono, lakini hiyo inatakiwa ije automatic kama en:wiki inavyokuja na sio kuandika kwa mkono. Je umeelewa?--Mwanaharakati 06:05, 5 Januari 2008 (UTC)
- Nikikuelewa vema iko hata hapa kwetu. Ukitazama dirisha hili la "Kuhariri" unaona alama ndogo juu yake. Ukibonyeza alama ya tatu kutoka upande wa kulia unapata alama za --~~~~. Alama hizi zinatafsiriwa na programu kuwa sahihi na tarehe mara ukihifadho maandiko yako. --62.154.201.129 09:26, 5 Januari 2008 (UTC)
Pole kwa kunijibu bila ya kuingia!! Pili hujanielewa. Nazungumzia tukio la pili mbali na la kwanza. Narudia tena: unapoweka hizo alama mbili za dash-dash kisha ~~~~, hizi zinataja jina la mtu aliyeacha ujumbe katika kurasa yako ama sivyo? Natumai ndivyo. Sasa tunakuja katika swala la pili: hapa kwetu unapoweka zile alama zinataja kurasa ya mtumiaji aliyeacha ujumbe katika kurasa yako bila ya kurasa yake ya majadiliano kuonekana, wakati ile ya en:wiki ukiweka hizo alama zinataja mambo mwaili kwa wakati mmoja (user page na user talk page) umeelewa?--Mwanaharakati 10:22, 5 Januari 2008 (UTC)
- Nafikiri ni muundo tofauti huko en:wiki. Tuone - nimecheza kwenye nafasi "mapemndekezo yangu - itatokea nini? --[[User_talk:Kipala]] 11:32, 5 Januari 2008 (UTC)
- Basi nimecheza upya - tuone! --User_talk:Kipala 11:34, 5 Januari 2008 (UTC)
- Nafikiri ni muundo tofauti huko en:wiki. Tuone - nimecheza kwenye nafasi "mapemndekezo yangu - itatokea nini? --[[User_talk:Kipala]] 11:32, 5 Januari 2008 (UTC)
Umekulupuka. Ile sio nikiname wala nini. Inakuja yenyewe na sio kuandika nickname au kujiandikia mwenyewe user talk page kwa mkono. Tuombe masaada kwani nasisi vilevile ni watu wa wikipedia na tuna stahili zana zote za kiufundi vinginevyo itakuwa maonevu. Ile inarahisisha mno. Vilevile hapa kwetu kunahitaji mabadliko mengi mno (nitakutumia katika e-mail- mabadiliko hayo) ili tuweze kuwa na kiwango cha juu.--Mwanaharakati 12:04, 5 Januari 2008 (UTC)
- Muddy, nimejifunza Afrika njia za panya na njia za juakali wanavyosema Kenya. Anyway jaribu tu njia isiyonyooka. --User_talk:Kipala 12:24, 5 Januari 2008 (UTC)
Ukisema njia isiyonyooka unamaanisha mimi sipo sawa na hoja yangu ninayokueleza. Haya!!--Mwanaharakati 13:23, 5 Januari 2008 (UTC)
- Haya mwalimu unasema kweli, nisamehe! Nimemaanisha kinyume chake --User_talk:Kipala 16:47, 5 Januari 2008 (UTC)
Hi Kipala
How are you? I'm new to this so I don't know if you received my message, here below. Hope all is well Kipala! :) I would like to ask if you could help me translate a short version of this article for the .sw Wikipedia? I would be more than happy if you could help me summarize a short stub-translation so that it could later help for future development. Do you think the .sw version of this article would be possible however short or long you could make it? I would be very grateful if you could help me with this. I’m looking forward to hear from you. Thanks so much and Happy New Year 2008! -Blianca Chica 03:01, 5 Januari 2008 (UTC)
Hi there :)
re: Inactive sysops and bureaucrats
Hi Patho, saw you popping up at our place. Maybe you have an advice for us: we are a wiki with very few regular contributors. At the moment more or less 4 who are at it regularly and a few poppping up once in a while. We have a whole bunch of people who once strted the project and have since left - either because they lost interest or because they cannot cope any more with the language (I think a number of these smaller wikis was started by non-speakers who just felt there should be something in African languages..). Now, we have a list of people on our sysop list who just don`t show up any more. Better leave them or any way to clean up?
And a bit pressing: our only bureaucrat does not function any more. Thats why we have all those bots without flag. What to do about a inactive bureaucrat? sw:user:Kipala --78.49.52.138 07:38, 11 January 2008 (UTC)
- Hello Kipala. Sysop and bureaucrat access are a matter of local consensus, so you can remove access from inactive users if there is a general agreement to do so. One large wiki with this kind of policy is the English Wikisource (see en:s:Wikisource:Administrators#Confirmation discussions).
- Generally, having no active bureaucrat is not a problem until the wiki is much larger. You can hold votes or discussions for access on the wiki, then post a request on m:Requests for permissions or m:Requests for bot status. A steward (like myself) who has bureaucrat access on all wikis will do it for you, usually within 24 hours.
- If you'd like to respond, please do so at m:user talk:Pathoschild. I will notify you of any responses here. —Pathoschild 07:59:27, 11 Januari 2008 (UTC)
Asante
Thanks a million Kipala! If you need any help with anything related to Spanish, please let me know. Is there any other language you could help with? Asante, Blianca Chica 19:55, 12 Januari 2008 (UTC)
Kipala, shikamoo. Naomba unisaidie maarifa namna ya kuelezea televisheni na matangazo yake. Mfano hii ya TVT, binafsi nimeeleza lakini naona kama sio mazuri zaidi. Je unaweza kutia neno lolote lile lenye kufanya makala ile kuwa bora zaidi?--Mwanaharakati 07:42, 16 Januari 2008 (UTC)
Angalia na hii: Televisheni. Nimejaribu kufuata kidoogo taratibu za uandikaji wako (yaani nimeiba namna unavyo andika). Makala hii ninawasiwasi nayo pale katika vipimo vya cm na inches, je unaweza kuitazama na hii kisha ukarekebisha mawili matatu? Japo kwa muda mchache...--Mwanaharakati 12:01, 16 Januari 2008 (UTC)
Kipala, salam. Naam, nimeoona mabadilisho yako kadhaa katika makala ya TV. Lakini kuna swali nataka nikuulize kidoogo.. Ile picha ulitengeneza vipi? Maana nilibaki nang'aa sharubu (kung'aa sharubu ni kushangaa) tu kwa kuiangilia ile picha. Ningependa kufahamu ulifanza vipi!!!!!--Mwanaharakati 05:12, 23 Januari 2008 (UTC)
Yote kwa ujumla. Maana ile si ni picha moja ulioiunganisha mpaka ikawa inasoma vile!! Basi nielezee yote kwa ujumla!!--Mwanaharakati 14:50, 23 Januari 2008 (UTC)
Salam. Nimeona. Lakini bado naona maluweluwe tu katika mfumo ulionitajia. Pale umetoa maelezo yaliyojitolsheleza pasipo zana za kufanyia kazi ama sivyo? Labda ningeuliza zaidi nini kilifanyika kabla ya ile picha ya jicho na nyenzake iliyofuta ulitumia nini? a) kamera b) Kompyuta? c) Ama kifaa kingine tofauti na hivyo viwili!!!--Mwanaharakati 05:43, 24 Januari 2008 (UTC)
Kingine: naomba ile makala inayohusu mimi ifutwe. Sijapenda kuitaja miaka yangu dhahiri katika wiki hii. Vilevile mimi sasa hivi sifanyi tena kazi ya uproducer, limebaki jina tu. Pia mimi sasa hivi ni mchangiaji haitoleta maana mchangiaji akawa na makala. Tafadhali naomba uifute nd. Kipala.. Makala inaitwa: Muddyb Blast Producer. Niko radhi. Kwasababu nilitaka kuandika miaka ya ungo katika ukurasa wangu wa mtumiaji, lakini ile makala ya Muddyb Blast Producer inanifunga. Naomba iondoshe mkubwa kazi..--Mwanaharakati 06:44, 24 Januari 2008 (UTC)
Kipala umeelewa vibaya. Ya kufuta ni makala (Muddyb Blast Producer) na sio user page.--Mwanaharakati 07:14, 24 Januari 2008 (UTC)
Tobaa, ndio hairudi tena!!!--Mwanaharakati 07:17, 24 Januari 2008 (UTC)
Re:Kufutwa kwa user:Muddy
Salam. Hicho ndicho ninachotaka haswaaa. Kama inawezekana kuirudisha ile user-page yangu ya awali itakuwa bora zaidi, kwani nilitumia mda mwingi sana kuihariri. Ile makala ya http://sw.wikipedia.org/wiki/Muddyb_Blast_Producer ndio ya kufutwa, kwasababu mie sasa hivi si matayrishaji tena, hivyo nisingependa niwe na makala katika mtandao huu. Futa tu ile. Halafu ile kurasa yangu ya awali ilete upya kama inawezekana!! Kingine usidhani nimekasirika na hili la. Muda ulionitumia ujumbe nilikuwa tayari nimekwisha hondoka shule, hivyo sikuwa tena online kitu ambacho kilipelekea kutojibiwa kwa ujumbe wako. Naomba tuswameheane kwa yote, amina...--Mwanaharakati 04:43, 25 Januari 2008 (UTC)
Naisubiri kwa hamu.--Mwanaharakati 07:37, 25 Januari 2008 (UTC)
Bado haijaja hadi sasa..--Mwanaharakati 09:17, 25 Januari 2008 (UTC)
Kipala, Idee lako halikuwa Straße, maana toka Uhr za asubuhi nakuomba unirudihie Antwort langu bado kimya vipi? Itarudi ama? (leo nimeamua kukupa na Kijerumani kidogo labda utanisoma vizuri: siko nyuma kwa lugha).--Mwanaharakati 15:23, 25 Januari 2008 (UTC)
Uchaguzi
Salam. Ahsante kwa kula yako..--Mwanaharakati (niambie) 15:56, 1 Februari 2008 (UTC)
Vipi umefaulu?--Mwanaharakati (talk) 05:00, 2 Februari 2008 (UTC)
Tafadhalia, naomba angalia Sanduku la mchanga kwa jaribio la kutaka kuhariri ukurasa wa mwanzo..--Mwanaharakati (talk) 16:14, 2 Februari 2008 (UTC)
Kutia sahihi
Salam. Nilimaanisha kwamba umefaulu kuweka zile kodi katika nick name yako ili iweze kufanya kazi? Basi kama hujaelewa labda nitoe tena mfano!!
1. Nakili hizi kodi kisha paste katika sehemu ya nick name yako, automatic zitaweka user page yako na user talk page yako:[[User:Kipala|Kipala]] ([[User talk:Kipala|talk]]),
2. Weka off hii: Raw signatures (without automatic link) ili zile kodi ziweze kufanya kazi. Vinginevyo hazito fanya kazi.
Kila lakheri na nakutakia afya njema...--Mwanaharakati (talk) 04:20, 4 Februari 2008 (UTC)
Ukurasa wa Mwanzo
Salam. Nimebadilisha ukurasa wa Mwanzo na nimimweka: Dwight D. Eisenhower. Unaweza kuangalia kama ni sawa.. Nitakuwa nabadilisha kila baada ya wiki, unaonaje?--Mwanaharakati (talk) 16:05, 5 Februari 2008 (UTC)
Sawa tu. Nitasubiria. Endapo utakuwa hauja badilisha kurasa, basi nitaibadili!! Na vipi kuhusu lile swala la kutia sahihi?--Mwanaharakati (talk) 04:23, 6 Februari 2008 (UTC)
All system message
Salam. Ukiona una muda wa kuweza kubadili baadhi ya viungo vilivyopo katika wiki hii (yaani, kama vile neno viungo viungacho nk.) Ipo sehemu nimeona ya kubadilisha system nzima iliyoandikwa Kiingereza au Kiswahili kilicho kosewa!! Basi unaweza kubadilisha kwa kutumia HAPA. Mie nilijaribu ikakataa, inataka mtu aliyemkabdhi ndiyo afanye hivyo!! Natumai utaweza kuifanya hiyo kazi (ama sivyo?) Jaribu tuone... Kisha naomba unijulishe kama iko sawa!!--Mwanaharakati (talk) 11:50, 7 Februari 2008 (UTC)
Dear Kipala; please look at the links at commons:user:i18n#useful links. Thanks in advance! Best regards Gangleri
·לערי ריינהארט·T·m:Th·T·email me· 13:08, 7 Februari 2008 (UTC)
- I looked - and saw nothing! What is it about? I have no clue. --User_talk:Kipala 21:10, 7 Februari 2008 (UTC)
Re:Picha za Dar
Kipala, salam. Kazi hiyo ni rashisi kufanya. Lakini mimi sina kamera, je nitafanyaje? Labda nijaribu kutafuta kama kuna moja kati ya marafiki zangu watakuwa nayo!! Nikiipata basi mara moja nitafanya hivyo!! Wasalaam.--Mwanaharakati (talk) 06:53, 11 Februari 2008 (UTC)