Amerika ya Kaskazini
Amerika ya Kaskazini ni bara upande wa Kaskazini mwa Ikweta. Inapakana na Bahari ya Pasifiki upande wa Magharibi, na Bahari ya Atlantiki upande wa Mashariki.
Ina nchi mbili hadi tatu kutegemeana na hesabu:
- Kanada
- Marekani
- Meksiko (kijiolojia ni sehemu ya Amerika Kaskazini ingawa kiutamaduni ni sehemu ya "Amerika ya Kilatini" na kuhesabiwa pia katika Amerika ya Kati).
Kisiwa cha Greenland ni sehemu ya Amerika Kaskazini kijiografia maana kipo juu ya bamba la gandunia lileile, lakini si nchi huru, bali kipo chini ya Denmark.
Nchi za Amerika ya Kati zinahesabiwa kuwa sehemu za bara hilo katika hesabu ya kawaida ya mabara saba. Kijiolojia ziko juu ya bamba la gandunia tofauti na Amerika Kaskazini: ni bamba la Karibi pia kihistoria na kiutamaduni ziko tofauti na nchi mbili kubwa katika kaskazini.
Jina "Amerika"
haririNeno "Amerika" limetokana na jina la kwanza la Mwitalia Amerigo Vespucci (1451-1512). Vespucci alikuwa baharia na mfanyabiashara katika utumishi wa familia ya Medici kutoka Firenze (Italia). Tangu mwaka 1499 alisafiri kwenye pwani za Amerika ya Kusini na Amerika ya Kati akaandika kitabu juu ya safari zake. Humo aliandika ya kwamba hakukubaliana na Kristoforo Kolumbus ya kwamba visiwa na nchi zilizofikiwa na Kolumbus zilikuwa sehemu ya Uhindi. Amerigo alipendekeza ya kwamba zilikuwa sehemu za "dunia mpya" au bara jipya akiwa mtu wa kwanza kuandika hivyo.
Mwanajiografia Mjerumani Martin Waldseemüller alitumia jina la "Amerika" kwa heshima ya Amerigo alipochora ramani yake ya dunia ya mwaka 1507.
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|