Warangi
Warangi ni mojawapo kati ya makabila yanayopatikana katika wilaya ya Kondoa, mkoa wa Dodoma, mji ambao ndiyo makao makuu ya nchi ya Tanzania.
Kirangi ndiyo hasa lugha ya Warangi, ambayo wao huiita Kilaangi.
Warangi wamegawanyika katika dini ya Uislamu na Ukristo, hasa wa Kanisa Katoliki.
Asili na uenezi
haririNi kati ya makabila yaliyotokea Mijikenda (leo nchini Kenya). Inasemekana Warangi ni kabila lenye asili ya Ethiopia yaani Wakushi wa Kusini. Waliweza kuhamia Tanzania kutoka Ethiopia mnamo miaka ya 1700[1].
Hadi leo, kwa muonekano Warangi wanafanana na Wahabeshi kuwa wana sura nyembamba, pua ndefu na nywele za kuchanganya asili ya Asia na Afrika.
Utamaduni
haririKuhusu utamaduni wa Warangi, kijitabu kimetolewa juu ya vifaa vya zamani, kama kirindo, kyome kipekecho na vinginevyo.
Chakula kikuuu cha Warangi ni ugali wa mahindi au uwele, na mboga zinazotumika ni kama vile maziwa(masusu), kirumbu (mlenda) na nyama.
Pia Warangi hujishughulisha na kilimo cha mazao ya chakula na biashara; mazao ya chakula ni kama uwele, mtama, mahindi n.k. na mazao ya biashara ni kama vile karanga, alizeti, njugu mawe na kunde.
Vazi rasmi la kabila hili ni kaniki, lakini wengi wanavaa mavazi ya Kiarabu yakiwemo hijjab, kanzu na n.k.
Kuhusu ngoma, kuna ngoma kama mdundiko wa Kirangi ambao huchezwa na watu wa kabila hilo, mara nyingi ukiwa mchana.
Majina mara nyingi huendana na wakati uliopo, kwa mfano: Mwasu (jua), Mbula (mvua), Nchira (ngozi), Nyange, Ndudya, Kichiko (masika), Salala (kimvua kidogo), Mnjira, Kifuta, Mwapwani, Ichuka, Luji, Kidunda n.k.
Tanbihi
hariri- ↑ "Ijue historia na asili ya kabila la Warangi wa Kondoa". JamiiForums (kwa American English). 2018-02-16. Iliwekwa mnamo 2024-01-13.
Marejeo
hariri- Fosbrooke, H.A. 1958 “Blessing the Year: a Wasi/Rangi Ceremony”, Tanganyika Notes and Records 50, 21-2
- Fosbrooke, H.A. 1958 “A Rangi Circumcision Ceremony: Blessing a New Grove”, Tanganyika Notes and Records 50, 30-36
- Gray, R.F. 1953 “Notes on Irangi Houses”, Tanganyika Notes and Records 35, 45-52
- Kesby, J. 1981 “The Rangi of Tanzania: An introduction to their culture”, HRAF: Yale
- Kesby, J. 1982 “Progress and the past among the Rangi of Tanzania”, HRAF: Yale
- Kesby, J. 1986 “Rangi natural history: The taxonomic procedures of an African people”, HRAF: Yale
- Maingu, Yovin na Brunhilde Bossow, 2006 "Mazingira ya Warangi na Wajerumani wa Kale", Kutolewa na Heimat- und Kulturverein Gellersen (Shirika la Historia na Utamaduni za Vijiji vya Gellersen, Ujerumani)
- Masare, A.J. 1970 “Utani Relationships: The Rangi”, muswada usiotolewa rasmi, Dar es Salaam
- Mung’ong’o, Claude G. 1995 “Social Processes and Ecology in the Kondoa Irangi Hills, Central Tanzania”, Chuo Kikuu cha Stockholm, Idara ya Human Geography, Meddlanden Series B 93
- Östberg, W. 1979 “The Kondoa Transformation”, research report no. 76, SIAS: Uppsala
Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Warangi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |