Mtume Yohane
Yohane mwana wa Zebedayo alikuwa mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu, ambaye alipendwa na mwalimu wao kuliko wenzake wote.
Mitume wa Yesu |
---|
|
Mapokeo ya Kikristo yanamuona kuwa mwandishi wa Injili ya Yohane, wa barua tatu (Waraka wa kwanza wa Yohane, Waraka wa pili wa Yohane, Waraka wa tatu wa Yohane) na wa Kitabu cha Ufunuo.
Maisha
haririAlizaliwa na Salome baada ya Yakobo Mkubwa mwanzoni mwa karne ya 1 B.K. akafa mkongwe mwishoni mwa karne hiyo huko Efeso (katika Uturuki wa leo).
Kabla ya kumfuata Yesu Kristo alikuwa mvuvi na mfuasi wa Yohane Mbatizaji.
Ndiye shahidi mkuu wa miaka mitatu hivi ya utume wa Yesu, akiwa wa kwanza kumfuata (pamoja na Mtume Andrea), mshiriki wa matukio ya pekee ya mwalimu wake (kama alipogeuka sura mlimani), mtume pekee aliyesimama chini ya msalaba, wa kwanza kusadiki ufufuko wa Yesu hata kabla hajamuona.
Kutokana na udhati wa teolojia yake alifananishwa na tai.
Tangu kale anaheshimiwa na madhehebu karibu yote ya Ukristo kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 27 Desemba[1].
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo
hariri- Thenashara, Mitume Kumi na Wawili – tafsiri ya P. A. Bunju – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Ndanda 1984 – ISBN 9976-63-030-1
Viungo vya nje
hariri- The Life and Miracles of St. John the Evangelist and Apostle Archived 2 Juni 2015 at the Wayback Machine.
- "Saint John the Apostle." Encyclopædia Britannica Online.
- Answers.com
- Catholic Encyclopedia: St. John the Evangelist
- Eastern Orthodox icon and Synaxarion of Saint John the Apostle and Evangelist (May 8)
- John the Apostle on Find-A-Grave
- John the Apostle in Art Archived 22 Aprili 2006 at the Wayback Machine.
- John in Art
- Repose of the Holy Apostle and Evangelist John the Theologian Orthodox icon and synaxarion for September 26
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mtume Yohane kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |