Zahanati ya Ithnashiri

Zahanati ya Ithnashiri (pia inajulikana kama Old Dispensary[1]) ni jengo la kihistoria katika Mji Mkongwe, Zanzibar. Liko mbele ya bahari, katika barabara ya Mizingani, katikati ya Jumba la Makumbusho la Ikulu na bandari.

Zahanati ya Ithnashiri kwa mbele, 2020.
Zahanati ya Ithnashiri kwa ndani, 2021.
Zahanati ya Ithnashiri upande wa ndani

Jina lake linatokana na ukweli kwamba ilitumika kama zahanati katika nusu ya kwanza ya karne ya 20.

Zahanati hiyo ni mojawapo kati ya majengo yaliyopambwa vizuri zaidi ya Mji Mkongwe na alama ya usanifu wa kitamaduni na urithi wa jiji.[1][2] Balkoni zake za mbao zilizochongwa, na mapambo ya vioo, ni ya ushawishi wa India; muundo mkuu umejengwa na kitambara cha jadi cha matumbawe ya Kizanzibari na chokaa, lakini imefunikwa na mapambo ya mpako ya ladha ya Ulaya mamboleo.[2] Ndani ya jengo ni sawa tu, na ua uliofunikwa na madaraja ya kuchonga yanayounganisha sakafu. Zahanati hiyo ni kimojawapo katika vivutio vikuu vya Mji Mkongwe. Ina jumba la makumbusho dogo kuhusu historia ya Zanzibar.[1]

Historia

hariri

Ujenzi wa Zahanati ya Kale uliamriwa mnamo 1887 na Tharia Topan, mfanyabiashara tajiri wa Ismaili, kusherehekea jubilii ya Dhahabu ya malkia Viktoria wa Uingereza. Kusudi la Topan lilikuwa kwamba jengo hilo litumiwe kama hospitali ya hisani kwa maskini. Alipofariki mnamo 1891, jengo lilikuwa halijamalizika. Mjane wake alianza tena kazi hiyo lakini ilibidi aisimamishe mnamo 1893 kwa kuwa bajeti yake haikutosha. Hatimaye nyumba ilimalizika kwenye mwaka 1894, lakini pesa haikutosha tena kufungua hospitali yenyewe.[3]

Mnamo mwaka wa 1900 jengo hilo liliuzwa kwa warithi wa mfanyabiashara mwingine mashuhuri wa Kihindi aliyeishi Zanzibar, Haji Nasser Nurmohamed,[4] aliyewahi kutenga sehemu ya mali yake kwa taasisi ya hisani. Warithi waliamua kwamba ghorofa la chini litatumika kama zahanati, wakati ghorofa za juu ziligawanywa kuwa vyumba vya kuishi. Ilhali Haji Nasser alikuwa mfuasi wa Shia Ithnashiri na taasisi iliyoundwa kutokana na urithi wake ilimilikiwa kufuatana na kanuni ya dhehebu hilo, ikaitwa sasa Zahanati ya Ithnashiri.

Mnamo mwaka wa 1964, kufuatia Mapinduzi ya Zanzibar (ambapo Wahindi wengi wa Kizanzibari, pamoja na wale walioishi katika zahanati hiyo, waliuawa au walikimbilia nje ya nchi), jengo hilo lilitwaliwa na serikali, na baadaye likaanza kutotumika na kuoza.

Mnamo 1990, kama sehemu ya mpango wa jumla wa ukarabati wa majengo ya kihistoria ya Mji Mkongwe, Taasisi ya Aga Khan ya Utamaduni ilipokea idhini kutoka kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kurejesha Zahanati hiyo.Hii ilikamilishwa Aprili 1994.[5]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 "Stone Town". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Agosti 2010. Iliwekwa mnamo 29 Oktoba 2010. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 Zanzibar Stone Town Projects: Conservation Works in the Former Old Dispensary Ilihifadhiwa 3 Machi 2016 kwenye Wayback Machine., Aga Khan Trust for Culture
  3. Aga Khan Historic Cities Programme - Zanzibar Stone Town Projects name, kijitabu cha 1997 kwenye tovuti ya Taasisi ya Aga Khan, iliangaliwa Machi 2021
  4. Tharia Topan
  5. "The Palace Museum". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-21. Iliwekwa mnamo 2021-03-14.