Alfabeti ya Kigiriki
Alfabeti ya Kigiriki ni mwandiko maalumu wa lugha ya Kigiriki. Herufi zake zilitumika pia kama tarakimu na sasa hutumiwa kimataifa kama alama za kisayansi.
Alfabeti ya Kigiriki | |||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Herufi za kawaida | |||||||
Α α Alfa | 1 | Ν ν Ni | 50 | ||||
Β β Beta | 2 | Ξ ξ Ksi | 60 | ||||
Γ γ Gamma | 3 | Ο ο Omikron | 70 | ||||
Δ δ Delta | 4 | Π π Pai | 80 | ||||
Ε ε Epsilon | 5 | Ρ ρ Rho | 100 | ||||
Ζ ζ Dzeta | 7 | Σ σ ς Sigma | 200 | ||||
Η η Eta | 8 | Τ τ Tau | 300 | ||||
Θ θ Theta | 9 | Υ υ Ipsilon | 400 | ||||
Ι ι Iota | 10 | Φ φ Phi | 500 | ||||
Κ κ Kappa | 20 | Χ χ Khi | 600 | ||||
Λλ Lambda | 30 | Ψ ψ Psi | 700 | ||||
Μ μ Mi | 40 | Ω ω Omega | 800 | ||||
Herufi za kihistoria1 | |||||||
Digamma | 6 | San | 90 | ||||
Stigma | 6 | Koppa | 90 | ||||
Heta | 8 | Sampi | 900 | ||||
Yot | 10 | Sho | 900 | ||||
1 Viungo vya Nje: Alfabeti_ya_Kigiriki#Viungo_vya_Nje |
|
|
Problems listening to this file? See media help. |
Historia
haririAlfabeti ya Kigiriki ilianzishwa wakati wa ustaarabu wa Ugiriki wa Kale na imeendelea kutumiwa hadi katika Ugiriki ya leo.
Ni alfabeti mama ya lugha za Ulaya, kwa sababu ni asili ya Alfabeti ya Kilatini ambayo ni mwandiko unaotumiwa leo duniani kushinda miandiko mingine. Ni pia asili ya alfabeti za Kikyrili na Kikopti. Kuna miandiko mingine ya kihistoria iliyotokana na Kigiriki.
Asili ya mwandiko huo ulikuwa alfabeti ya Kifinisia inayoaminiwa kuwa alfabeti ya kwanza kabisa duniani. Wagiriki waliongeza alama za vokali (kama a-e-i-o) na kubadilisha mwendo wa mwandiko kutoka kushoto kwenda kulia, tofauti na Kifinisia iliyoandikwa kutoka kulia kwenda kushoto jinsi ilivyo hadi sasa katika mwandiko wa Kiarabu na wa Kiebrania ambazo ni lugha za Kisemiti jinsi ilivyokuwa Kifinisia.
Sehemu ya herufi zilizopokewa kutoka Kifinisia ziliachwa baadaye kwa sababu lugha haikuwa na sauti za kulingana nazo. Tangu mwaka 300 KK sehemu ya juu ya alfabeti inayoonyeshwa kwenye sanduku ilikuwa herufi za kawaida na alama za chini hazikutumiwa isipokuwa kama alama za namba.
Katika historia ndefu ya alfabeti hii matamshi ya alama yamebadilika pamoja na mabadiliko ya lugha yenyewe. Mwanafunzi wa Kigiriki cha Kale anayesoma maandiko ya Plato au vitabu vya Agano Jipya katika lugha asilia ataona shida akifika Ugiriki na kuwasikia Wagiriki wa leo: hata kama anaweza kusoma maandishi yote, hataelewa mengi.
Matumizi ya herufi kama namba
haririKila herufi ilikuwa pia na matumizi kama tarakimu ya namba kwa sababu Wagiriki wa Kale hawakuwa na alama za pekee kwa namba. Herufi tatu za kihistoria ambazo hazikutumiwa tena kwa maandishi ziliendelea kama alama za namba, yaani Digamma au Stigma = 6 (alama ϝ au ς), Koppa = 90 (alama ϙ au ϟ) na Sampi = 900 (alama ͳ au ϡ au kama kwenye sanduku).
Kwa kutofautisha herufi na namba alama yake ilipewa mstari mdogo juu yake kama αʹ = 1, βʹ = 2, γʹ = 3. Kwa namba kuanzia 1,000 mstari upande wa kushoto uliongezwa, kwa mfano ͵α = 1,000, ͵β = 2000, ͵βηʹ = 2008.
Matumizi ya kisayansi
haririHerufi za Kigiriki zinatumiwa sana katika hesabu na sayansi. Mifano inayojulikana zaidi ni matumizi ya α, β na γ kama majina ya pembe za pembetatu.
Katika mahesabu ya duara namba π (pai) ni muhimu sana.
Kuna matumizi mengine mengi: karibu kila herufi ina maana fulani kisayansi.
Viungo vya Nje
hariri- Unicode ya Kigiriki (unicode.org) (Kiingereza)
- Unicode ya Kigiriki (opoudjis.net) (Kiingereza)
- Digamma Wau (Kiingereza)
- Digamma Pamphylia (Kiingereza)
- Stigma (Kiingereza)
- Heta (Kiingereza)
- Yot (Kiingereza)
- San (Kiingereza)
- Koppa herufi (Kiingereza)
- Koppa namba (Kiingereza)
- Sampi herufi (Kiingereza)
- Sampi namba (Kiingereza)
- Sho (Kiingereza)
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Alfabeti ya Kigiriki kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |