Kanisa kama jengo


Kanisa kama jengo ni maabadi maalumu ya Wakristo.

Wakristo walipoanza kujenga mahali pa ibada, pakaja kuitwa vilevile kanisa kwa sababu ndani yake lilikusanyika Kanisa hai.

Hivyo mara nyingi neno hilo linatumika kwa maana ya jengo, ambalo ni mfano mwingine uliotumiwa na Mtume Paulo kuhusu umoja wa Wakristo, ukiwa na Yesu kama jiwe kuu la msingi.

Majengo hayo ya ibada yanaweza kuwa na ubora tofauti hata upande wa sanaa; baadhi yake yanatembelewa na watalii na kuhifadhiwa kwa bidii kwa sababu hiyo.

Kwa namna ya pekee ni muhimu Kanisa kuu la kila jimbo, halafu Basilika na Patakatifu, lakini pia kanisa la parokia, kanisa la kigango (hilo pengine linaitwa sunagogi, ambalo kwa kweli ni jina la majengo ya Wayahudi).

Christianity Symbol.png Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kanisa kama jengo kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.