Siti Nurhaliza
Siti Nurhaliza binti Tarudin (alizaliwa 11 Januari 1979) ni mwanamke mwimbaji, mwandishi wa nyimbo, mwigizaji na mfanyabiashara[1] kutoka Malaysia mwenye zaidi ya tuzo 300 za kitaifa na kimataifa.[2][3]
Alifanya wimbo wake wa kwanza baada ya kushinda onyesho la ndani la mashindano ya kuimba "Bintang HMI" mnamo 1995 alipokuwa na miaka 16. Wimbo wake wa kwanza Jerat Percintaan, ulishinda "11th Anugerah Juara Lagu" na tuzo nyingine mbili za Utumbuizaji Bora na “Ballad” Bora.[4] Albamu ya mwaka 2005, imeuza zaidi ya nakala 800,000 huko Malaysia.[5] Amerekodi na kuimba katika lugha mbalimbali, zikiwemo “Malaysian”, “Javanese” Kiingereza[6] na “Mandarin”.[7]
Katika kipindi cha kazi yake, Siti amepokea idadi nyingi ya tuzo za muziki ambayo haijawahi kutokea katika Malaysia na nchi jirani.[8] 42 Anugerah indusri Muzik, 25 Anugerah Bintang Popular, 27 Anugerah Planet Muzik 20 Anugerah Juara Lagu, 4 MTV Asia Awards, 3 World Music Awards, 2 Anugerah Musik Indonesia (Indonesia Music Awards), na 2 rekodi kwenye Malaysia Book Rekords. Akiwa na 17 Studio albamu ni mmoja kati ya wasanii maarufu katika mikoa ya Malay Archpelago na Nusantara - amepigiwa kura kwa Regional Most Popular Artiste (Msanii Maarufu wa Kanda) kwa mfululizo akiwapita wasanii wenzake kutoka Malaysia, Indonesia na Singapore katika Anugerah Planet Muzik tangu 2001.[9] Kwa sasa ameorodheshwa kama tajiri wa Malaysia,[10] mshawishi mkuu,[11] mshindi wa tuzo nyingi na msanii mwenye nyimbo nyingi zaidi.[12] Pia ni mmoja ya wasanii bora wanaouza Malaysia, na mauzo ya albamu yake yamechangia asilimia 10 ya jumla ya mauzo ya albamu Malaysia kwa mwaka 2001.[13] Mpaka sasa, ameuza zaidi ya milioni 6 kwenye rekodi za mauzo.
Katika majukwaa ya kimataifa, Siti alishinda Tuzo ya Dhahabu (Gold Award) kwenye Mashindano ya Mwimbaji Mpya wa Asia (Asia New Singer Competition) katika Tamasha la Muziki la Shanghai Asia (Shanghai Asia Music Festival) mnamo 1999,[11] tuzo mbili kutoka “South Pacific International Song and Singing Competition 1999 iliyofanyika huko Gold Coast, Queensland, Australia,na Grand Prix Champion taji katika Voice of Asia mnamo 2002 iliyofanyika katika Almaty, kazakhstan. Mnamo 2020, baada yakupokea kuvunja rekodi ya kura, alishinda chaguo la umma kwenye Adelaide Festival Centre’s Walk of Fame 2019.[14]
Mbali na tuzo za muziki, ana mafanikio mengineyo. Mnamo 1998, Siti alichaguliwa kutumbuiza wakati wa kufunga sherehe ya mwaka 1998 ya Commonwealth of Nations.[15] Mnamo 2005, Siti alikuwa mwimbaji wa kwanza wa Kusini mashariki mwa Asia, na mwimbaji wa tatu wa Asia kutumbuiza tamasha binafsi katika ukumbi wa Royal Albert Hall, London, wakati akisaidiwa na London Symptom Orchestra.[16] Aliorodheshwa wa pili na MTV Asia katika Msanii Bora wa Muziki (Best Musical Artiste)[17] wa Asia na Biggest Asian Artiste ya Channel V mnamo 2005.[17] Mnamo 2008 baadaye, alitajwa kama mmoja wa “Idol “ wa Asia na Asia News Network.[18] Pia ameorodheswa kama mmoja ya Waislamu 500 - Waislamu 500 wenye Ushawishi zaidi Duniani kutoka mwaka 2015 mpaka 2021.[19] Mafanikio yake katika ukanda wa Asia yamempa mataji ya heshima yakijumuisha Sauti ya Asia “Voice of Asia” [20] na Celine Dion wa Asia “Asia’s Celine Dion”.[21]
Maisha ya awaliEdit
Siti Nurhaliza alizaliwa 11 Januari 1979, huko Berek Polis (kambi za polisi) Kampung Awah huko Temerloh, Pahang ambapo alikuwa mtoto wa tano katika familia ya ndugu wanane kwa Tarudin Ismail, afisa wa polisi na Siti Salmah Bachik, mama wa nyumbani.[22][23] Anatoka kwenye familia yenye kupenda muziki, kaka yake, Saiful Bahri Tarudin, na dada zake, Siti Norsaidia na Siti Saerah pia ni waimbaji.[24] Babu yake alikuwa mpiga violini, na mama yake alikuwa mwimbaji wa kijadi.[22]
Wakati wa utoto wake, alijiusisha kwenye shughuli mbalimbali za shule, zikiwemo michezo na zile za mitaala.[25] Alisoma shule yake ya awali katika Tabika Perkep, Balai Polis Kampung Awah, Temerloh ambapo alionyesha kipaji chake cha kuimba akiwa na miaka 6 ambapo aliimba “Sinh Pinang”,[26] wimbo wa jadi wa Malay, katika tukio la chekechea la upokeaji wa vyeti.[22] Baadaye alisoma shule ya msingi katika Sekolah Menengah Kebangsaah Clifford, Kuala Lipis, Pahang.[25] Mnamo 1991, alipokuwa na umri wa miaka 12, alishinda moja ya mashindano yake ya awali ya kuimba, na wimbo “Bahtera Merdeka” katika Shindano la Kuimba Siku ya Merdeka (Merdeka Day Singing Contest), shindano la ndani la wimbo wa kizalendo.[27][28] Wakati wa miaka yake shule, alikuwa na hali katika michezo, hasa mpira wa wavu (netball)[29] na hii ilidhihirishwa alipokuwa anashiriki katika matukio mawili tofauti ya michezo - mpira wa wavu na “5x80 meter relay” wakati wa Fiesta Media Idola 2006 huko Kuantan.[30] Pia alichaguliwa kama mmoja wa washika mwenge kumulika michezo ya Fiesta, kuashiria ufunguzi wake sambamba na mwigizaji wa Malaysia, Fasha Sandha.[30]
Kutoka kwenye familia maskini,[28][31] akiwa na umri wa miaka tisa,[32] Siti ilimbidi kuamka saa kumi kamili (10:00) usiku kumsaidia mama yake kutengeneza na kuuza “kuih” mbalimbali za kutengenezea nyumbani kwenye mtaa wake, ambapo mara nyingine, alilazimka kubeba meza ya kuamishika chini ya ngazi tatu kwenda kwenye barabara kuu kuweka kiduka cha kuuzia.[33] Alitoa maoni kwamba magumu yote hayajamsaidia tu kuwa na busara wakati wa kutumia, lakini pia kujiamini wakati akiwasiliana na umma.[32] Pia alisema kwa kutania kwamba uzoefu wote umemsaidia kuboresha ujuzi wa sauti yake sababu alilazimika kupiga kelele kuwaita wateja.[34] Licha ya kushiriki kwenye mashindano ya kuimba, alikuwa pia akimfuata mjomba wake Abdul Rhim Bachik, kwa maonyesho kama sherehe za harusi na karamu za chakula cha jioni, ambazo zimemsaidia kumfanya afanye maonyesho ya moja kwa moja.
KaziEdit
Mafanikio ya awali kibiashara (1995 - 1996)Edit
Familia ya Siti Nurhaliza ilitumbuiza katika sherehe nyingi za umma ndani ya mji wao, kama vile harusi na wageni wa umma. Akiwa na miaka 2, Siti alianza kujifunza nyimbo za jadi kutoka kwa mama na aliendelea kutumbuiza aina hiyo ya muziki wakati wa hafla maalum na matukio.
Pia alikuwa mwimbaji wa “Family Group”, bendi ndogo iliyoanzishwa na mjomba wake, Abdul Rahim Bachik. Alianza kuboresha ujuzi wake wa kuimba kwa kushiriki katika mashindano mbalimbali. Alipokuwa na miaka 14, alienda kwenye usahili kwa Asia Bagus lakini alishindwa kuendelea.[35] Licha ya mfadhaiko wake, lakini hakukata tamaa. Miaka miwili baadaye, alishiriki katika mashindano ya 1995 RTM Bintang HMI akiwa na umri wa miaka 16 ambapo alifanya usahili na wimbo uliofanywa maarufu na Ruth Sahnaya, Kaulah Segalanya. Katika mashindano, alikutana na Adnan Abu Hassan, mtunzi wa muziki aliyemfundisha na kumsaidia kwa utendaji wake sauti yake, kabla ya kushinda shindano kwa wimbo wa Aishah, Camar Yang.
Maendeleo ya kazi (1997 - 1998)Edit
Mnamo 1997, Siti alianza kuwa mtu mashuhuri katika tasnia ya muziki wa Indonesia ambapo hadithi yake ilipoonekana katika moja ya majarida maarufu huko Indonesia, POS Kota, Aprili toleo la mwaka 1997.[36] Alichukuliwa kama mtu mwenye kutisha kwasababu ilikuwa ngumu kwa wasanii wa kigeni kupenya katika tasnia ya muziki Indonesia kama msanii ana ofa ndogo ukilinganisha na wa kwao.[36] Siti pia alisemekana kuwa msanii wa kwanza wa Malaysia kufanya tamasha la mubashara kwenye Indosiar, kituo cha television maarufu katika Indonesia na ilirushwa hewani nchini pote.[36] Amekuwa mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa huko Indonesia, hili lilithibitishwa na mfululizo wa matamasha makubwa aliyofanya katika Jakarta, Bandung, Yogyakarta na miji mingine mingi baada ya miaka michache.[37] Pia alishinda Msanii Bora Mpya "Best New Artist" na "Best Song" (Jerat Percintaan) kutoka Anugerah Industri Muzik 1997.[8]
Mwaka 1998, katika umri wa 19, alizindua kampuni yake mnamo 12 Januari (siku moja baada ya siku yake ya kuzaliwa ya 19), Siti Nurhaliza Productions (M) Sdn. Bhd. ambayo hufanya kama timu rasmi ya usimamizi.[38] Siti alijitokeza kwa mara ya kwanza na kubwa kwenye jukwaa la kimataifa wakati wa 1998 Commonwealth Games ambayo ilifanyikia huko Kuala Lumpur, Malaysia ambapo alitumbuiza mbele ya Queen Elizabeth II na mume wake, Prince Philip miongoni mwa waheshimiwa na viongozi na watendaji kutoka nchi 70 za Commonwealth.[15] Pia alishiriki jukwaa moja na wasanii nyota wawili Celine Dion na Rod Stewart kuuburudisha umati wakati wa kufunga.[39] Sherehe ilionyeshwa kwa njia ya telesheni katika mataifa 70 duniani kote, ilimpelekea kujulikana katika uwanja wa kimataifa kwa mara ya kwanza. Mnamo Novemba wa mwaka huo, aliarikwa kutumbuiza Japan kwa siku tano katika Pop Queen Festival, pia likijulikana kama Saga Fiesta ‘98.[40]
DiskografiaEdit
Albamu binafsiEdit
- 1996: Siti Nurhaliza I
- 1997: Siti Nurhaliza II
- 1997: Cindai
- 1998: Adiwarna
- 1999: Pancawarna
- 2000: Sahmura
- 2001: Safa
- 2002: Sanggar Mustika
- 2003: E.M.A.S
- 2003: Anugerah Aidilfitri
- 2004: Prasasti Seni
- 2006: Transkripsi
- 2007: Hadiah Daripada Hati
- 2008: Lentera Timur
- 2009: Tahajjud Cinta
- 2011: All Your Love
- 2014: Fragmen
- 2017: SimetriSiti
- 2020: ManifestaSITI2020
- 2021: Legasi
Albamu za ushirikianoEdit
- 1999: Seri Balas (pamoja na Noraniza Idris)
- 2009: CTKD (pamoja na Krisdayanti)
Matamasha na ziaraEdit
- Malaysia
- 1999: Konsert Live Siti Nurhaliza, Stadium Putra Bukit Jalil, Malaysia
- 2001: Konsert Mega Siti Nurhaliza, Bukit Jalil 2001, Malaysia
- 2002: Konsert Salam Akhir Siti Nurhaliza – Untukmu Sudir, Istana Budaya, Malaysia
- 2004: Siti Nurhaliza Live in Concert 2004, Stadium Nasional Bukit Jalil, Malaysia
- 2006: Konsert Akustik Siti Nurhaliza, Malaysia
- 2007: Konsert Istana Cinta, Istana Budaya, Malaysia
- 2009: SATU Konsert Eksklusif Dato' Siti Nurhaliza]], Istana Budaya, Malaysia
- 2009: Konsert Seribu Warna, Stadium Malawati, Shah Alam, Malaysia
- 2010: Konsert SATU Suara, Istana Budaya, Malaysia
- 2012: Dato' Siti Nurhaliza Concert Live in Kuantan 2012, Bukit Gambang Resort City, Gambang, Malaysia
- 2013: Siti Nurhaliza in Symphony Live with The Malaysian Philharmonic Orchestra, Petronas Philharmonic Hall, Malaysia
- 2013: Konsert Lentera Timur Dato' Siti Nurhaliza Esklusif Bersama Orkestra Tradisional Malaysia]], Istana Budaya, Malaysia
- 2014: Dato' Siti Nurhaliza Live in Concert – Where The Heart Is, Plenary Hall, Kuala Lumpur City Centre (KLCC), Malaysia
- 2015: Dato' Siti Nurhaliza Unplugged 2015, Istana Budaya, Malaysia
- 2015: Konsert Satu Suara, Vol. 2, Istana Budaya, Malaysia
- 2016: Dato' Siti Nurhaliza & Friends Concert, Stadium Negara, Malaysia
- 2019: Dato' Sri Siti Nurhaliza On Tour Concert, Axiata Arena, Kuala Lumpur, Malaysia
- 2019: Konsert Amal Orkestra Tradisional Malaysia bersama Siti Nurhaliza, Auditorium POWIIS, Prince of Wales Island International School, Penang, Malaysia[41]
- 2019: Shopee X SIMPLYSITI Mini Concert, KL Convention Centre, Conference Hall 1–3, Malaysia[42]
- 2019: Karya Agung Pak Ngah (Datuk Suhaimi Mohd Zain) bersama Orkestra Tradisional Malaysia dan Dato' Sri Siti Nurhaliza[43]
- Singapore
- 2000: Siti Nurhaliza Live at Harbour Front, Singapore
- 2005: Siti Nurhaliza Live 2005, Indoor Stadium, Singapore
- 2008: Konsert Diari Hati Siti Nurhaliza, Esplanade Theatre, Singapore
- 2010: Konsert Bagaikan Sakti, Esplanade Theatre, Singapore
- 2014: Dato' Siti Nurhaliza Live in Singapore, The Star Theatre, Singapore
- 2019: Dato' Sri Siti Nurhaliza on Tour Concert, Singapore Expo, Singapore
- 2020: Konsert Karya Agung Pak Ngah – Pak Ngah's Legendary Hits in Concert by Orkestra Tradisional Malaysia ft. Dato' Sri Siti Nurhaliza, Esplanade Theatre, Singapore
- Indonesia
- 2002: Konsert 1 Jam Bersama Siti Nurhaliza
- 2003: Konsert Azimat Siti Nurhaliza
- 2003: Konsert Special Siti Nurhaliza
- 2004: Konsert Exclusive Melanesia - Siti Nurhaliza
- 2004: Konsert Mutiara Negeri Jiran - Siti Nurhaliza
- 2004: Siti Nurhaliza Indonesia Tour 2004, Indonesia
- 2011: Charity Concert Banjarmasin, Indonesia
- 2017: Golden Memories International Spesial Siti Nurhaliza
- 2019: Dato' Sri Siti Nurhaliza on Tour Concert, Istora Senayan, Jakarta, Indonesia
- Nyinginezo
- 2002: Siti Nurhaliza Live in Brunei, Brunei
- 2005: Siti Nurhaliza in Concert, Royal Albert Hall London, United Kingdom
- 2010: Siti Nurhaliza Live @ Alumbra, Australia
- 2019: Siti Nurhaliza The Voice of Asia in Australia For One Night Only – OzAsia Festival, Festival Theatre, Adelaide, Australia[44]
FilmografiaEdit
FilamuEdit
Mwaka | Jina | Jukumu | Maelezo |
---|---|---|---|
2009 | Kelip-Kelip | Kunang-Kunang (voice) | Mhusika mkuu |
2018 | Konsert Hora Horey Didi & Friends[45] | Mak Iti (voice) | Mwonekano maalum |
VideografiaEdit
|
|
Maonyesho ya sanaaEdit
- 2014: SITI: An Iconic Exhibition of Dato' Siti Nurhaliza
Kazi za maandishiEdit
Licha ya kuimba na kutangaza, ameandika pia makala nyingi kwenye magazeti mengi na majarida.
Mwaka | Jina | Gazeti / Jarida |
---|---|---|
1999 | Lenggok Siti | Metro Ahad (Sunday Edition) |
2006 | Pena Siti | Kosmo! Ahad (Sunday Edition) |
2010–2012 | Catatan Siti Nurhaliza | Mangga |
2011–mpaka leo | Dari Dalam Diri Siti Nurhaliza | Berita Harian[46] |
MarejeoEdit
- ↑ Jadi pengacara, Siti bukan pengacau. Utusan Online. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-10-21. Iliwekwa mnamo 2021-04-15.
- ↑ Ulang tahun ke-40 Siti Nurhaliza hari ini. Astro AWANI Network Sdn. Bhd..
- ↑ Siti Azira Abd. Aziz (25 October 2009). Siti akui jualan album terjejas ekoran kekeruhan Malaysia-Indonesia (ms). mStar Online. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-10-17. Iliwekwa mnamo 2021-04-15.
- ↑ Siti Nurhaliza. SitiZone. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-02-28. Iliwekwa mnamo 2021-04-15.
- ↑ Malay Mail Staff (9 May 2005). Career Highlights: Adnan Abu Hassan. The Malay Mail. AccessMyLibrary.
- ↑ Whitney Houston & Dato' Siti Nurhaliza - Memories | Official Music Video (in English), retrieved 2021-03-11
- ↑ Dato' Siti Nurhaliza - Zheng Fu (Full Studio Version) (in English), retrieved 2021-03-11
- ↑ 8.0 8.1 Her Achievements. SitiZone. Jalada kutoka ya awali juu ya 2009-06-11. Iliwekwa mnamo 2021-04-15.
- ↑ Senarai Keputusan Pemenang Anugerah Planet Muzik APM 2011. Sensasi Selebriti.
- ↑ Mohd Azam Shah Yaa'cob, Hidayatul Akmal Ahmad & Raja Norain Hidayah Raja Abdul Aziz (20 June 2010). Milik harta tujuh angka (ms). myMetro.
- ↑ 11.0 11.1 Shuib Taib (7 September 2009). Top 10 influential celebrities in Malaysia: Stars with the x-factor sizzle. The New Straits Time. AsiaOne.com. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-08-29. Iliwekwa mnamo 2021-04-15.
- ↑ SACC showcase: Dato' Siti Nurhaliza and Krisdayanti. New Straits Time. Digital Collections DC5: Text Archive (14 April 2010).
- ↑ New Straits Times Staff (21 August 2000). RIM takes on pirates. New Straits Times. AccessMyLibrary.
- ↑ Stars celebrated and record breaking votes for Adelaide Festival Centre’s Walk of Fame. AussieTheatre.com.
- ↑ 15.0 15.1 Best Ever Commonwealth Games Comes to a Close. Utusan Online. Utusan Online (22 September 1998). Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-12-11. Iliwekwa mnamo 2021-04-15.
- ↑ Hafidah Samat (14 January 2005). Siti all set for London show.. New Straits Times. AccessMyLibrary.
- ↑ 17.0 17.1 Charlie Lancaster (9 May 2010). Top of the pops. Southeast Asia Globe. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-10-29. Iliwekwa mnamo 2021-04-15.
- ↑ Asia's Idols. Inquirer.net – Philippine News for Filipino (5 January 2008). Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-02-21. Iliwekwa mnamo 2021-04-15.
- ↑ Siti Nurhaliza Disenarai 500 Muslim Paling Berpengaruh Empat Tahun Berturut-Turut. Vijandren Ramadass.
- ↑ SACC showcase: Dato' Siti Nurhaliza and Krisdayanti. New Straits Times (10 April 2010). “"Dato' Siti Nurhaliza is a multiple-award winning Malaysian pop singer-songwriter who has garnered more than 100 local awards. Known as the Voice of Asia, Siti has recorded more than 30 albums including singles. She is also known to have the most number one singles than any other artist in Malaysia."”
- ↑ Siti Nurhaliza's Journey To Stardom Aired on Astro's History Channel. Bernama (12 January 2012). Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-11-10. Iliwekwa mnamo 2021-04-15. “" The diva also became the first Malaysian artiste to ever perform at the prestigious Royal Albert Hall in London, where she was dubbed "Asia's Celine Dion" by the British press."”
- ↑ 22.0 22.1 22.2 Seneviratne, Kalinga (2012). Countering Mtv Influence in Indonesia and Malaysia. ISBN 9789814345231.
- ↑ Siti Nurhaliza (id). KapanLagi.com – Kalau bukan sekarang, kapan lagi?.
- ↑ Siti Azira Abd. Aziz (22 October 2009). Siti nafi ditawar jutaan ringgit untuk 'Konsert Seribu Warna' (ms). mStar Online. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-01-29. Iliwekwa mnamo 2021-04-15.
- ↑ 25.0 25.1 Shazryn Mohd. Faizal (6 July 2010). Siti teruja 'kembali' ke sekolah (ms). Utusan Online. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-06-17. Iliwekwa mnamo 2021-04-15.
- ↑ Siti teruja 'kembali' ke sekolah. SimplySiti.com.my (2013). Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-06-19. Iliwekwa mnamo 2021-04-15.
- ↑ Saharuddin Mustafa (31 August 2003). Siti Nurhaliza terkenang Bahtera Merdeka (ms). Utusan Online. Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-02-03. Iliwekwa mnamo 2021-04-15.
- ↑ 28.0 28.1 New Straits Times Staff. "Will this be you?", New Straits Time, AccessMyLibrary, 10 January 2003.
- ↑ Nor Asikin Hassan (8 August 2010). Siti Nurhaliza merakam nostalgia Clifford (ms). Utusan Online. Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-02-03. Iliwekwa mnamo 2021-04-15.
- ↑ 30.0 30.1 Nor Fadzillah Baharuddin (4 April 2006). Fiesta Media Idola '06 tetap meriah walaupun kecoh (ms). Utusan Online. Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-02-03. Iliwekwa mnamo 2021-04-15.
- ↑ Khadijah Ibrahim (4 September 2003). Siti Nurhaliza – Melabur untuk masa depan adik (ms). Utusan Online. Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-02-03. Iliwekwa mnamo 2021-04-15.
- ↑ 32.0 32.1 Muhammad Arif Nizam Abdullah (13 November 2006). Siti Nurhaliza muncul di Jalan Masjid India (ms). Utusan Online. Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-02-03. Iliwekwa mnamo 2021-04-15.
- ↑ Amirah Amaly Syafaat (29 July 2012). Antara Permata dan Hati (ms). Utusan Online. Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-02-03. Iliwekwa mnamo 2021-04-15.
- ↑ Nizam Abdullah (17 October 2011). Siti Nurhaliza Tidak Ambil Mudah (ms). mStar Online. Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-02-01. Iliwekwa mnamo 2021-04-15.
- ↑ Hizreen Kamal (6 January 2012). Siti's inspiring journey. New Straits Time.
- ↑ 36.0 36.1 36.2 Hos Rancangan Tv Indonesia. (ms). Berita Harian. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-08-11. Iliwekwa mnamo 2021-04-15.
- ↑ Konser Tunggal Siti Nurhaliza Di Gelar di 5 Kota Indonesia (id). KapanLagi.com – Kalau bukan sekarang, kapan lagi?.
- ↑ Dato' Hajjah Siti Nurhaliza (ms). Siti Zone. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-01-26. Iliwekwa mnamo 2021-04-15.
- ↑ Siti all set for London show. New Straits Time. Digital Collections DC5: Text Archive (14 January 2005).
- ↑ Saharudin Musthafa (1 November 1998). Siti Nurhaliza dapat pengiktirafan di Jepun (ms). Utusan Online. Jalada kutoka ya awali juu ya 2011-06-17. Iliwekwa mnamo 2021-04-15.
- ↑ Konsert amal bantu penggiat seni kumpul dana RM80,000 (21 July 2019).
- ↑ "Siti kekal pendirian berehat daripada sertai AJL", Kosmo! Online, Utusan Melayu (Malaysia) Berhad, 15 September 2019. Retrieved on 2021-04-15. Archived from the original on 2019-10-02.
- ↑ "#Showbiz: Honouring a giant", New Straits Times, New Straits Times Press (M) Bhd., 8 November 2019.
- ↑ The Voice of Asia in Australia For One Night Only. Adelaide Festival Centre.
- ↑ "Siti meriahkan Konsert Hora Horey Didi & Friends", Kosmo Online, Utusan Group. Retrieved on 13 March 2018. Archived from the original on 2018-06-12.
- ↑ Siti Nurhaliza. "Iktibar dari tanah runtuh", Berita Harian, Digital Collections DC5: Text Archive, 28 May 2011. (ms)