Open main menu

Delaware ni jimbo la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Iko kwenye pwani la Atlantiki upande wa mashariki ya Marekani bara. Imepakana na majimbo ya Pennsylvania, Maryland na kwa kilomita chache pia na New Jersey. Mji mkuu ni Dover lakini mji mkubwa ni Wilmington.

Delaware
Mahali pa Delaware katika Marekani
Mahali pa Delaware katika Marekani

Bendera

Nembo
Nchi Bendera ya Marekani Marekani
Mji mkuu Dover
Eneo
 - Jimbo 6,447 km²
 - Bara 5,060 km² 
 - Maji 1,387 km² 
Tovuti: http://delaware.gov/
Ramani ya Delaware

Jina la jimbo latokana na mto Delaware na hori la Delaware ambazo zote ziliitwa kwa heshima ya mkabaila Mwingereza De La Warr katika mnamo mwaka 1600.

Delaware ni jimbo dogo lenye eneo la 6,452 km² na wakazi 783,600 pekee. Kati ya majimbo ya Marekani ni jimbo lenye mapato ya juu kwa kila raia. Sheria zake za kodi ya mapato ni nafuu hivyo makampuni mengi yamepeleka ofisi zao hapa. Menginyevyo uzalishaji hi hasa mazao ya kilimo pamoja na ufugaji kuku.

HistoriaEdit

Ilianzishwa kama kituo cha biashara ya Uswidi mwaka 1638 iliyovamiwa na Uholanzi na kuwa baadaye koloni ya Uingereza tangu 1664. Delaware ilikuwa koloni ya kwanza ya kukubali katiba mpya ya Maungano ya Madola ya Amerika baada ya uasi wa koloni 13 za Uingereza katika Amerika ya Kaskazini.

Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Majimbo ya Marekani

AlabamaAlaskaArizonaArkansasCaliforniaColoradoConnecticutDelawareFloridaGeorgiaHawaiiIdahoIllinoisIndianaIowaKansasKentuckyLouisianaMaineMarylandMassachusettsMichiganMinnesotaMississippiMissouriMontanaNebraskaNevadaNew HampshireNew JerseyNew MexicoNew YorkNorth CarolinaNorth DakotaOhioOklahomaOregonPennsylvaniaRhode IslandSouth CarolinaSouth DakotaTennesseeTexasUtahVermontVirginiaWashingtonWest VirginiaWisconsinWyoming

  Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Delaware kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.