Istanbul

(Elekezwa kutoka İstanbul)

Istanbul (kwa Kituruki unatajwa İstanbul) ni mji mkubwa zaidi katika nchi ya Uturuki, ukiwa na wakazi wanaokadiriwa kuwa kati ya milioni 11 na 15, ambao wanaufanya kuwa miongoni mwa miji mikubwa ya dunia. Huu ndio mji mkuu wa Mkoa wa İstanbul.

Mji wa Insatbul, Uturuki
Istanbul kutoka angani; juu iko Bahari Nyeusi, chini Bahari ya Marmara; sehemu ya Asia upande wa kulia, Ulaya upande wa kushoto wa Bosporus; "Pembe ya dhahabu" ni mkono wa bahari unaoonekana chini upande wa Ulaya.
Bandari ya Istanbul ilivyowahi kuchorwa.

Eneo la Istanbul linaelekea pande zote mbili za mlangobahari wa Bosporus unaotenganisha Ulaya na Asia. Hivyo ni mji pekee duniani uliopo katika mabara mawili.

Kiini cha kihistoria kipo upande wa Ulaya kwenye sehemu yenye umbo la rasi baina ya Bahari ya Marmara na Pembe ya Dhahabu ambayo ni mkono wa bahari unaoingia ndani ya nchi na hivyo mahali pa mji ulikingwa na bahari pande tatu.

Historia

hariri

Mji huu umebadilishiwa jina mara kadhaa katika historia yake ya zaidi ya miaka 2,600. Awali jiji hilo liliundwa na Wagiriki mnamo mwaka 660 KK kwa jina la Bizanti. Mnamo mwaka 330 BK Kaisari Konstantino Mkuu aliufanya kuwa mji mkuu wa Dola la Roma akaupanua ukajulikana kama Konstantinopoli (yaani mji wa Konstantino).

Konstantinopoli uliendelea kama mji mkuu wa Dola la Roma na baadaye Roma ya Mashariki uliojulikana pia kama Milki ya Bizanti hadi mwaka 1453 ambapo mji ulitwaliwa na Waturuki. Tangu mwaka ule uliendelea kama mji mkuu wa Milki ya Osmani hadi mwaka 1923. Baadaye serikali ya Uturuki ilihamia Ankara.

Wakati wa Waosmani majina mbalimbali yalitumiwa: Konstantinopoli au kwa kifupi "Konstantiniye", halafu tangu karne ya 18 pia "Istanbul". Tangu mwaka 1873 jina rasmi kwa Kituruki limekuwa "Istanbul".

Kuwepo kwa bandari kumepelekea mji huo kuwa kitovu cha biashara katika Uturuki.

Katika Ukristo ni muhimu kama makao ya Askofu wa pili kwa heshima kati ya Maaskofu wote duniani, kadiri ya orodha iliyotolewa na mitaguso mikuu ya karne ya 4.

Hadi vita vya kwanza vya dunia Istanbul ilikuwa na wakazi wengi Wakristo, hasa Wagiriki na Waarmenia, lakini wakati ule Waarmenia waliteswa wakapungua na baada ya vita Wakristo walibaguliwa kwa jumla, hivyo wengi walihamia Ugiriki. Leo hii Wagiriki waliobaki ni 2000 - 3000 pekee na Waarmenia ni takriban 50,000.

Majengo

hariri

Istanbul huwa na majengo mengi ya kihistoria kama vile

Mjini Istanbul kuna vyuo vikuu mbalimbali, kati yake:

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Uturuki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Istanbul kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.