Kitabu cha Wamakabayo I
Kitabu cha kwanza cha Wamakabayo ni kimojawapo kati ya vitabu vya deuterokanoni vya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.
Kinasimulia jinsi Wayahudi, wakiongozwa na familia ya Wamakabayo, walivyopambana kwanza na mfalme Antioko IV (aliyejiita Antioko Epifane) halafu na Wayunani wengine katika karne ya 2 KK (175-135 KK).
Kitabu hiki si mbali na matukio kinayoyasimulia, kwa kuwa kiliandikwa kati ya mwaka 140 KK na 130 KK kwa lugha ya Kiebrania, ingawa katika lugha hiyo asili hatuna nakala yoyote, bali tuna tafsiri ya Kigiriki tu katika Septuaginta.
Mwandishi wake hajulikani, lakini kitabu hiki kinaonyesha alikuwa Myahudi wa Palestina, alipenda taifa na dini yake ya Uyahudi, na alijua kwa dhati masuala ya teolojia.
Mfalme huyo alijaribu kulazimisha Wayahudi kufuata utamaduni na dini ya Kiyunani, jambo ambalo lilipingwa na waamini waadilifu wakiongozwa na Matathia na wanae Yuda Mmakabayo, Yonathani Mmakabayo na Simoni Mmakabayo.
Tofauti na kitabu cha Tobiti, kitabu cha Yudith na Kitabu cha Esta, kitabu hiki kinajitahidi kusimulia taratibu za habari za historia, ingawa kinasifu ushujaa wa Wayahudi.
Mwandishi hamtaji Mungu, isipokuwa kwa kusema "mbingu"; lakini wapigania uhuru wanategemea sala. Hivyo hatimaye ushindi uliopatikana unahesabiwa ni tunda la msaada wa Mungu.
Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Marejeo
hariri- Bartlett, John R. 1998. 1 Maccabees. Sheffield, UK: Sheffield Academic Press.
- Borchardt, Francis. 2014. The Torah in 1 Maccabees: A Literary Critical Approach to the Text. Boston: Walter de Gruyter.
- Goldstein, Jonathan A. 1976. I Maccabees: A New Translation, with Introduction and Commentary. Anchor Bible 41. Garden City, NY: Doubleday.
- Lanzinger, Daniel. 2015. "Alcimus’ Last Command: History and Propaganda in 1 Maccabees 9:54." Journal for the Study of Judaism 46, no. 1: 86–102.
- Williams, David S. 1999. The Structure of 1 Maccabees. Washington, DC: Catholic Biblical Association.
Viungo vya nje
haririWikisource has original text related to this article: |
- The Book of First Maccabees Full text
- 1 Maccabees: 2015 Critical Translation with Audio Drama at biblicalaudio
- Knox Bible 1 Maccabees 1 Ilihifadhiwa 18 Agosti 2010 kwenye Wayback Machine.
- Links & Information on 1 Maccabees
- 1 Maccabees, article in historical sourcebook by Mahlon H. Smith
Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki
Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kitabu cha Wamakabayo I kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |