Open main menu
Mlima wa Ambohimanga

Ambohimanga ni jina la mlima karibu na Antananarivo katika Madagaska. Katika karne ya 18 ilikuwa makao makuu ya sehemu ya wafalme wa Wamerina walioteka kutoka hapa sehemu nyingine za Imerina ikaendelea kuwa mahali pa makaburi ya wafalme wa Madagaska hadi 1897. Tangu mwaka 2001 imeandikishwa katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO.

Geti kuu ya Ambohimanga

JinaEdit

Etimolojia ya jina Ambohimanga inatokana maneno mawili ya Kimalagasi: ambohi inayomaanisha "kilima" na manga inayomaanisha "takatifu" [1]. Kina lilitolewa na mfalme Andriamasinavalona wakati wa karne ya 18[2]

Maana ya kihistoria na kiroho katika MadagaskaEdit

Mlima huu pamoja na "rova" (boma la wafalme) juu yake hutazamiwa kama ishara muhimu zaidi wa utamaduni wa Wamerina. Pia ni kumbukumbu bora iliyohifadhiwa ya Ufalme wa Madagaska ya enzi kabla ya ukoloni na ufalme wa Imerina. Kuna ikulu na makaburi za wafalme mbalimbali yenye maana ya kiroho kwa Wamadagaska wengi.

Hadi leo miiko mbalimbali huheshimiwa kwa wakazi wa vijiji walio karibu ny mlima kama vile kuepukana na mahindi, mboga, nguruwe, vitunguu, matumizi ya manyasi katika upishi na kukata kuni kwenye msitu takatifu mguuni pa mlima [3].

Ambohimanga ilikuwa mahali muhimu tangu mwanzo wa karne ya 18 wakati mfalme Andriamasinavalona (1675–1710) aligawa Imerina kwa robo nne na kumpa mwanawe Andriantsimitoviaminiandriana robo ya kaskazini magharibi. Ugawaji huu ulisababisha vita ya wenyewe kwa wenyewe ya miaka 77. Watawala wa Ambohimanga walioboresha kuta za mji wao na kuenea. Mfalme Andrianampoinimerina aliweza kuunganisha Imerina chini ya utawala wake ahdi mwaka 1793. Baadaye alirudisha ikulu yake katika mji mkuu wa kihistoria Antananarivo akitangaza mii yote miwili kuwa mji mkuu na Ambohimanga kuwa mji mkuu wa kiroho. Yeye mwenyewe na wafalme waliomfuata walikuja hapa kwa ibada za kifalme na kupata makaburi yao hapa hadi Ufaransa ilivamia Madagaska na kuhamisha familia ya kifalme nje ya kisiwa.

 
Mfumo wa kuta, mifereji ya kinga na geti za Ambohimanga

Msitu mtakatifuEdit

Sehemu ya chini ya mlima inafunikwa kwa msitu ambayo ni mabaki ya misitu asilia iliyojaa nyanda za juu za Madagaska. Miti mbalimbali huwa na maana ya kiroho ikitumiwa kwa ibada ya wazimu.

Majengo ya ngomeEdit

Sehemu ya juu ya mlima penye ikulu na makazi zimezungukwa kwa mifereji ya ulinzi zenye urefu hadi mita 30 na kuta imara. Kuna geti imara 14 zilizofungwa kwa duara ya jiwe [4]. Kila geti ina jina la pekee na geti moja ilikuwa haki ya mfalme pekee aliyeweza kupita hapa. Katika karne ya 19 wageni wa nje walikataliwa kuingia geti yoyote.

Ikulu za kifalmeEdit

 
Ikulu ya Mahandrihono

Kuna majengo ya ikulu 3 zilizohifadhiwa mlimani.

Kufuatana na mapokeo ya Wamerina majengo wa watu hai walijengwa kwa ubao na zana kutokana na mimea (zana hai), lakini majengo kwa wfu kama makaburi yelitengenezwa kwa kutumia mawe. Mwishoni mwa karne ya 19 baada ya kutokea kwa moto matumizi ya jiwe iliruhusiwa pia kwa majengo ya makazi. Tangu 1966 majengo mengi yaliona matengenezo kulingana na desturi za kale.

Kuna sehemu 3 za ikulu zenye majengo na makazi ya wafalme mbalimbali ambayo ni ikulu za Bevato, Mahandrihono na Nanjakana.

Sehemu ya majengo hasa ya Bevato yalibomolewa na wakoloni Wafaransa waliotaka kuondoa maana ya kiroho katika mahali wakilenga kudhoofisha kumbukumbu ya utamaduni wa kale. Waliteneneza majengo mengine na mengine kati ya haya majengo ya kikoloni yalibomolewa tena baada ya uhuru.

Makaburi ya KifalmeEdit

 
Makaburi ya kifalme yaliotengenezwa upya

Kiasili kulikuwa na makaburi 12 ya kifalme [5]. Wafaransa walihamisha makaburi ya wafalme kwenda Atananarivo mwaka 1897 na zawadi za mazishi kuonyeshwa kwenye makumbusho ya ethnolojia ya Antananarivo. Walikuwa na shabaha ya kuvunja roho ya upinzani kati ya wazalendo.

Serikali ya Madagaska iliamua mwaka 2008 kutengeneza makaburi upya na kurudisha mifupa ya wengine hapo.

MarejeoEdit

Viungo vya NjeEdit