Barabara nchini Tanzania

Barabara nchini Tanzania ni mtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita 91,532, ambazo kati yake kilomita 12,197 zimeainishwa kama barabara kuu (trunk roads) na kilomita 21,298 kama barabara za kimkoa (regional roads) na aina hizo za barabara husimamiwa na mamlaka ya TANROADS iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. [1]

Barabara za kiwilaya (district roads), za vijiini (feeder roads) na za mjini (urban roads) hutunzwa na halmashauri za kila eneo[2], urefu wa barabara hizo ni jumla ya km 58,037.

Barabara kuu za kitaifa zilikuwa na namba inayotanguliwa na herufi "A", barabara za kimkoa huwa na herufi "B". Barabara za hadhi za chini zingekuwa na herufi "C" lakini hizi hazionekani.

Kwa barabara kuu mfumo mpya umeanzishwa unaotumia namba za "T" lakini hauonekani kwenye ramani na hata alama za barabarani zenyewe bado huonyesha namba za "A".


Ishara iliyotolewa na wakala wa barabara za Tanzania Tanroads, kando ya barabara kuu kutoka Mwanza kwenda Shinyanga.
Barabara Na. (zamani) Urefu Kutoka-hadi kupitia Hali Maelezo
A7 km 492 Dar es Salaam - Iringa Chalinze - Morogoro - Mikumi Lami
A14 km 315 Chalinze - Horohoro Segera - Tanga Lami Inaendelea katika Kenya hadi Mombasa
A19 km 620 Mtwara - Mbamba Bay Masasi - Tunduru - Songea - Mbinga Lami/ udongo Lami: Masasi - Ngomano (km 56) na Namtumbo - Mbinga (km 168)
A23 km 117 Arusha - Holili Moshi Lami Inaendelea katika Kenya hadi Voi
A104 km 1,218 Tunduma- Namanga Mbeya - Iringa - Dodoma - Kondoa - Arusha Lami huhesabiwa kama sehemu ya njia Kairo-Cape Town, lami: Dodoma - Babati (km 257)
B1 km 263 Segera - Himo Lami Inaunganisha A14 na A23
B2 km 561 Dar es Salaam - Mtwara Kilwa - Lindi Lami Lami km 30 hadi Kilwa Masoko kutoka Nangurukuru
B3 km 625 Singida - Rusumo Falls Nzega - Isaka - Kahama Lami pamoja na B6 Nzega - Tinde (km 42), inaendelea kama RN3 katika Rwanda hadi Kigali
B4 km 293 Makambako - Songea Njombe Lami
B5 km 120 Mingoyo - Masasi Lami Inaunganisha B2 na A19
B6 km 1,071 Makongolosi - Sirari Rungwa - Tabora - Shinyanga - Mwanza Lami/Udongo Lami: Nzega - Sirari (km 524), pamoja na B3 Nzega - Tinde (km 42)
B8 km 1,128 Kasesha - Mutukula Sumbawanga - Mpnaa - Kasulu - Biharamulo - Bukoba Lami/Udongo Lami: Lusahunga (B3) - Mutukula (km 287)
B129 km 388 Morogoro - Manyoni Dodoma Lami
B141 km 308 Rungwa - SIngida Itigi - Manyoni Lami/Udongo Lami: Itigi - Singida (km 160)
B143 km 151 Singida - Babati Lami
B144 km 390 Makuyuni - Kukirango Karatu - Ngorongoro – Hifadhi ya Taifa Serengeti Lami/Udongo Lami: Makuyuni - Ngorongoro (km 79), ndani ya hifadhi hakuna lami
B163 km 230 Usagara - Biharamulo Sengerema - Geita Lami/Udongo Udongo: Bwanga - Biharamulo (km 68), njia ya lami iko kupitia Chato kwenda Bukoba
B182 km 171 Nyakasanza - Kyaka Kimisi – Hifadhi ya Burigi - Omurushaka Lami/Udongo Lami: Omurushaka - Kyaka (km 57), inaunganisha B3 na B8
B182 W km 111 Omurushaka - Murongo Udongo Inatoka B182 ikiendelea hadi mpaka wa Murongo na Ugnaa
km 173 Bulahu - Lamadi Bariadi Lami/Udongo Lami: Bariadi - Lamadai (km 72), imeainishwa na TANROADS kama barabara kuu lakini haijapewa namba bado
km 59 Nyakasanza - Kobero Ngara - Kabanga Lami Inatoka B3 hadi paka wa Kobero na Burundi, ikiendelea pale kama RN6

Mpangilio mpya wa Barabara Kuu za Tanzania hariri

Katika mpangilio mpya usionekana bado mahali pengi barabara kuu zilipewa namba zinazoanza kwa herufi "T". Zimepangwa kwa kusudi la kuunganisha miji muhimu kati yao au na mipaka, mabandari na barabara kuu nyingine. Hivyo sehemu za barabara halisi inaweza kupangwa kwa barabara kuu mbili tofauti.

Jina fupi Kutoka - hadi Urefu Ramani
(bofya ili kuona sehemu yake)
Picha
T1 Dar es SalaamMorogoroMbeyaTunduma – Mpaka wa Zambia inapoendelea kama T2 (Zambia) km 930    
T2 ChalinzeSegeraArushaNamanga – Mpaka wa Kenya km 650    
T3 MorogoroDodomaSingidaLusahungaRusumo – Mpaka wa Ruanda km 1100  
T4 Mpaka wa UgandaMutukulaBiharamuloMwanzaSirari – Mpaka wa Kenya km 820  
T5 ArushaDodomaIringa km 690  
T6 MakambakoSongeaMingoyoMtwara km 930  
T7 Dar es SalaamLindi – Mingoyo km 480  
T8 MwanzaNzegaTaboraRungwaMbeya km 900  
T9 BiharamuloLusahungaKanyaniSumbawangaTunduma – Mpaka wa Zambia inapoendelea kama T2 (Zambia) km 1000  
T10 MbeyaKasumulu – Mpaka wa Malawi km 100  
T11 NyakasanzaKabanga – Mpaka wa Burundi km 60  
T12 SongeaMbamba Bay km 165  
T13 SegeraTangaChuyuni – Mpaka wa Kenya km 135  
T14 SingidaBabati (section is currently unpaved km 145  
T15 HimoTaveta – Mpaka wa Kenya km 20  
T16 MikumiMahenge km 260  
T17 MakuyuniMusoma km 440    
T18 ManyoniTaboraKanyani km 520  
T19 Kanyani – Kigoma – Manyovu – Mpaka wa Burundi km 70  
T20 Sumbawanga – Kasesya – Mpaka wa Zambia inapoendelea kama M1 (Zambia) km 100
T21 HimoTarakea – Mpaka wa Kenia km 50  
T22 Rungwa – Itigi – Mkiwa km 200
T23 Mpanda – Ipole km 280  

Marejeo hariri

  1. "TANROADS Official Website :: Home". Tanroads. Iliwekwa mnamo 27 February 2016.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. Transport Master Plan 2011, uk 4-3

Viungo vya Nje hariri