Eneo bunge la Kasarani


Eneo bunge la Kasarani ni eneo bunge la uchaguzi nchini Kenya. Ni mojawapo wa maeneo bunge kumi na saba katika Kaunti ya Nairobi. Eneo lote la bunge hili liko katika eneo la Baraza la Mji wa Nairibi. Lilikuwa linajulikana kama Eneo Bunge la Nairobi Northeast katika uchaguzi wa miaka 1963 na 1969, na kama Eneo Bunge la Mathare katika uchaguzi wa kuanzia mwaka wa 1974 hadi uchaguzi mdogo wa mwaka wa 1994. Tangu uchaguzi wa 1997, limekuwa likijulikana kama Eneo Bunge la Kasarani.

Jamhuri ya Kenya

Makala hii imepangwa kwa mfululizo:
Siasa na serikali ya
Kenya



Nchi zingine · Atlasi

Wabunge hariri

Mwaka wa Uchaguzi Mbunge [1] Chama Vidokezo
1963 Munyua Waiyaki KANU
1969 Munyua Waiyaki KANU Mfumo wa Chama kimoja.
1974 Munyua Waiyaki KANU Mfumo wa Chama kimoja.
1979 Munyua Waiyaki KANU Mfumo wa Chama kimoja.
1983 Andrew Ngumba KANU Mfumo wa Chama kimoja. Ngumba alitoroka nchini mwaka wa 1986[2].
1986 Josephat Karanja KANU Uchaguzi mdogo, Mfumo wa Chama kimoja.
1988 Josephat Karanja KANU Mfumo wa Chama kimoja.
1992 Muraya Macharia FORD-Asili
1994 Fredrick Masinde Democratic Party (DP) Uchaguzi mdogo Masinde alifariki, na kusababisha uchaguzi mwingine mdogo [3].
1994 Ochieng Mbeo Ford-Kenya Uchaguzi mdogo (wapili katika mwaka wa 1994)
1997 Adolf Muchiri NDP
2002 William Omondi NARC
2007 Elizabeth Ongoro ODM

Kata na Wadi hariri

Kata
Kata Idadi ya Watu*
Githurai 66,979
Kahawa 44,660
Kariobangi 99,825
Kasarani 52,386
Korogocho 61,294
Roysambu 38,441
Ruaraka 110,686
Jumla 338,202
sensa ya 1999.
Wadi
Wadi Wapiga kura waliosajiliwa
Githurai 18,976
Kahawa 12,940
Kariobangi North 15,543
Kasarani 13,034
Korogocho 17,842
Mathare 4 A 16,930
Roysambu 10,464
Ruaraka 110,686
Utalii/Babadogo 22,495
Jumla 128,224
*Septemba 2005 |[4].

Marejeo hariri

  1. Center for Multiparty Democracy: Politics and Paliamenterians in Kenya 1944-2007 Archived 28 Februari 2008 at the Wayback Machine.
  2. Daily Nation, 18 Februari 2002: A position dogged by controversy
  3. Daily Nation, 2002: Is re-election likely for MP?
  4. Electoral Commission of Kenya: Registered voters per polling station by electoral area/ward and constituency

Viungo vya nje hariri