Helena, Montana
Helena ni mji mkuu wa jimbo la Montana nchini Marekani.
Helena | |
Nchi | Marekani |
---|---|
Jimbo | Montana |
Wilaya | Lewis and Clark |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 25,780 |
Tovuti: www.ci.helena.mt.us |
Idadi ya wakazi ni mnamo 25,780 (sensa 2000) na pamoja na maeneo jirani ni watu 67,636.
Historia
haririHelena ilikuwa na majina mbalimbali katika historia yake. Mji uliundwa mwaka 1864 baada ya kugunduliwa kwa dhahabu mtoni. Jina la kwanza la mji ulikuwa "Crabtown" kufuatana na John Crab aliyekuwa kati ya waanzilishaji wake. Baadaye jina likabadilishwa kuwa Pumpkinville halafu Squashtown.
Mwishowe jina jipya likatafutwa wakafuata pendekezo la "Saint Helena" wakaifupisha kuwa Helena.
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Helena, Montana kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |