Luxemburg
Luxemburg (pia: Lasembagi) ni nchi ndogo katika Ulaya. Imepakana na Ubelgiji, Ufaransa na Ujerumani.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Kiluxemburg: Mir wëlle bleiwe wat mir sinn (Kiingereza: "Tunataka kukaa jinsi tulivyo") | |||||
Wimbo wa taifa: Ons Hémécht ("Nchi yetu") WImbo wa kifalme: De Wilhelmus 1 | |||||
Mji mkuu | Luxemburg | ||||
Mji mkubwa nchini | Luxemburg | ||||
Lugha rasmi | Kifaransa, Kijerumani, Kiluxemburg | ||||
Serikali Mtemi mkubwa
Waziri Mkuu |
Utemi Mkubwa Mtemi Mkubwa Henri Luc Frieden | ||||
Uhuru Ilitangazwa Ilithebitishwa |
1815 1839 1867 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
2,586 km² (ya 167) -- | ||||
Idadi ya watu - 2019 kadirio - 2001 sensa - Msongamano wa watu |
613 894 (ya 164) 439,539 233.7/km² (ya 58) | ||||
Fedha | Euro (€)2 (EUR )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) | ||||
Intaneti TLD | .lu3 | ||||
Kodi ya simu | +352
- |
Ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya, tena ilikuwa kati ya nchi sita zilizoanzisha Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya mwaka 1957.
Historia
haririLuxemburg kama nchi ndogo ilikuwa mara nyingi chini ya athira ya majirani wakubwa waliotawala juu yake kwa vipindi mbalimbali.
Kwa vipindi vingi vya historia yake Luxemburg ilikuwa sehemu ya Ujerumani.
Katika karne ya 14 watemi wa Luxemburg walichaguliwa kuwa wafalme wa Ujerumani.
Baada ya vita za Napoleoni, Ufaransa na Prussia zilivutana juu ya Luxemburg. Walipatana kwenye Mkutano wa Vienna (1815) ya kurudisha Luxemburg kama nchi ya pekee itakayotawaliwa na Mtemi Mkubwa. Mfalme wa Uholanzi alikuwa mtemi wa Luxemburg na nchi yenyewe iliungwa katika Shirikisho la Ujerumani.
Baada ya mwisho wa Shirikisho la Ujerumani (1866) Luxemburg haikujiunga (1870) na Dola jipya la Ujerumani.
Badiliko la familia ya kifalme katika Uholanzi lilisababisha uchaguzi wa mtemi wa pekee (1890).
Watu
haririIna wakazi 613,894 (Januari 2019) katika eneo la km² 2,586 pekee. Kati yao 49.1% ni wahamiaji kutoka Ureno (18.2% za wakazi wote), Ufaransa (13.5%), Ujerumani (10.3%), Italia (3.4%), Ubelgiji (3.3%), na nchi nyingine.
Lugha ya taifa ni Kiluxemburg ambayo ni lahaja ya Kijerumani yenye athira nyingi za Kifaransa. Karibu wakazi wote huweza kuongea lugha hizo zote tatu na Kiingereza, lakini zaidi Kifaransa.
Upande wa dini, 68.7% wanajitambulisha kama Wakatoliki na 3.7% wanajitambulisha kama Wakristo wa madhehebu mengine. Waislamu ni 2.3%. Wasio na dini ni 26.8%.
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- Kreins, Jean-Marie (2003). Histoire du Luxembourg (kwa French) (tol. la 3rd). Paris: Presses Universitaires de France. ISBN 978-2-13-053852-3.
{{cite book}}
: CS1 maint: unrecognized language (link) - Thewes, Guy (Julai 2003). Les gouvernements du Grand-Duché de Luxembourg depuis 1848 (PDF) (kwa French) (tol. la Édition limitée). Luxembourg City: Service Information et Presse. ISBN 2-87999-118-8. Iliwekwa mnamo 10 Julai 2007.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link)
Viungo vya nje
hariri- Official website (Kifaransa)
- Luxembourg Archived 29 Agosti 2012 at the Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- Luxembourg entry at The World Factbook
- Luxemburg katika Open Directory Project
- Luxembourg profile from the BBC News
- Luxembourg's Constitution of 1868 with Amendments through 2009, English Translation 2012
- Plan d'action national luxembourgeois en matière de TIC et de haut-débit Archived 25 Septemba 2013 at the Wayback Machine.
- CEE- Europe’s Digital Competitiveness Report –Volume 2: i2010 –ICT Country Profiles- page 40-41 Archived 25 Septemba 2013 at the Wayback Machine.
- Inauguration of LU-CIX Archived 21 Februari 2011 at the Wayback Machine.
- Art and Culture in Luxembourg
- Wikimedia Atlas of Luxembourg
Nchi za Umoja wa Ulaya | |
---|---|
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Luxemburg kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |