Martha wa Bethania
Martha wa Bethania (jina lake kwa Kiebrania na Kiaramu ni מַרְתָּא, Martâ, kwa Kigiriki Μαρθα, Martha) alikuwa mwanamke wa Bethania, kitongoji cha Yerusalemu, katika karne ya 1[1].
Ndugu zake walikuwa Maria na Lazaro wa Bethania, ambao wote Yesu alifurahia urafiki wao alipokuwa akihiji kwenda Yerusalemu.
Wanaheshimiwa na Wakristo wengi kama watakatifu[2].
Sikukuu yao inaadhimishwa pamoja tarehe 29 Julai[3] au 4 Juni, kadiri ya madhehebu.
Maisha
haririAnajulikana hasa kutokana na Injili, kwa namna ya pekee Injili ya Luka (10:38-42) na Injili ya Yohane (11), katika Agano Jipya ndani ya Biblia ya Kikristo.
Humo anaonekana mwenye silika ya utendaji na imani kwa Yesu Kristo, ambaye alipendezwa na ukarimu wake, pamoja na kumuonya azingatie kwanza kilicho muhimu pekee, yaani kusikiliza Neno la Mungu.
Kisha kumkiri Yesu kuwa Kristo, Mwana wa Mungu aliyekuja ulimwenguni, alishuhudia alivyomfufua kaka yake Lazaro siku nne baada ya kifo chake.
Maneno yake kwa Yesu yalikuwa haya: "Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. Lakini hata sasa najua ya kuwa yoyote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa... Naam, Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni". (Yoh. 11:21-22, 27)
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
hariri- "St. Martha, Virgin", Butler's Lives of the Saints
- St. Martha on catholic.org
- Mary & Martha, the sisters of Lazarus Ilihifadhiwa 26 Oktoba 2009 kwenye Wayback Machine., Greek Orthodox Archdiocese of America
- Patron Saints: Martha Ilihifadhiwa 29 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.
- "St. Martha". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
- "The Life of Saint Martha" Ilihifadhiwa 30 Machi 2010 kwenye Wayback Machine., text from the Golden Legend
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Martha wa Bethania kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |