Wikipedia:2021 Told Cities Tanzania
Told Cities Tanzania 2021 ni mradi unaolenga kuandika, kuhariri, kuboresha na kuongeza maudhui kuhusu miji mikongwe nchini Tanzania ambayo kiujumla inatambulika na shirika la UNESCO kuwa ni urithi wa Dunia ikiwa ni pamoja na majengo yake. Mradi huu pia unahusisha kuhariri na kuongeza maelezo kwa Kiswahili katika mradi wa Wikidata kuhusu mada hiyohiyo ya miji, majengo ya zamani nchini Tanzania pamoja na majumba ya makumbusho.
Mradi huu unafanyika Tanzania kwa kushirikiana na Kundi la wahariri wa Wikipedia hapa Tanzania na lile la Wiki World Heritage User Group ambao ni kundi la watumiaji wanaojikita katika kuingiza habari za Orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO katika miradi ya Wikimedia.
Nchini Tanzania majengo ya kale yanayotambulika na UNESCO yanapatikana katika mji mkongwe wa Zanzibar (Zanzibar Stone Town) na pia Kilwa Kisiwani.
Shughuli za mradi huu
haririWashiriki wa mradi huu wanatakiwa kufanya kazi kuu za aina mbili:
- Moja ni kuhariri/kutafsiri makala kutoka Kiingereza kuja Kiswahili, kuboresha makala zilizopo kwa kuongeza picha, na kuhariri maelezo katika Wikidata.
- Pili ni wapiga picha kupakia picha mbalimbali za maeneo yoyote nchini Tanzania; picha hizo zinatakiwa kulenga majengo au majumba ya sanaa ya kihistoria ambayo kwa namna fulani huchukuliwa kama ni urithi wa nchi au Dunia kwa ujumla.
Orodha ya makala za kuzifanyia kazi
haririMradi huu unalenga kuongeza makala katika Wikipedia hii ya Kiswahili kuhusu maeneo/majengo mbalimbali ya kihistoria yanayotambuliwa katika orodha ya UNESCO. Tovuti ya UNESCO (angalia hapa) inataja majengo 10 za Mji Mkonge lakini inatambua Mji Mkongwe kwa jumla ukiwa pamoja na majengo mengine ya kihistoria.
Sheria ya Zanzibar imeorodhesha majengo 26 kama majengo ya kihistoria ya daraja la kwanza (Town and Country Planning Decree ya 1994; orodha iko uk. 10, Table 4: Grade I listed buildings in the Stone Town), nayo yanaorodheshwa hapo chini. Ramani ya Mji Mkonge inayoonyesha majengo hayo iko hapa.
Katika hatua ya kwanza inawezekana kutafsiri makala kutoka orodha ya Wikipedia ya Kiingereza en:List_of_landmarks_in_Stone_Town, ukiangalia makala zinazohusu majengo yanayotajwa na UNESCO au Sheria ya Zanzibar.
Jina la Kiingereza | Jina la Kiswahili | Namba (Msimbo) ya Wikidata |
---|---|---|
en:Forodhani Gardens | Bustani za Forodhani, Zanzibar | |
NN | SS |
Kwa Zanzibar tutumie jamii (categories) hizi: [[Jamii:Urithi wa Dunia katika Zanzibar]] [[Jamii:Wilaya ya Mjini Unguja]]; kama ni jumba la makumbusho, tutumie pia: [[Jamii:Makumbusho ya Tanzania]]
Sehemu nyingine ni maghofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara (Ruins of Kilwa Kisiwani and Ruins of Songo Mnara); (ukurasa wa UNESCO hapa). Makala ya enwiki en:Kilwa_Kisiwani ina maelezo mafupi kuhusu majengo kadhaa pamoja na kuonyesha vyanzo vinavyoweza kusaidia kutunga makala, lakini wachangiaji watahitaji kufanya utafiti wa undani zaidi.
Tuzo kwa Washiriki
haririMradi huu utatoa tuzo kwa washiriki hai kama ifuatavyo:
- 150USD, 100USD, na 50USD kwa wahariri bora watatu wa kwanza na
- 150USD, 100USD, na 50USD kwa wapigapicha bora watatu wa kwanza.