Mkoa wa Bonde la Ufa
| ||
Makao Makuu | Nakuru | |
’‘‘Mji Mkubwa’’’ | Nakuru | |
Eneo - Jumla |
Nafasi ya 1 kati ya mikoa ya Kenya 182,413 km² | |
Wakazi - Jumla (2007) - Msongamano wa watu / km² |
Nafasi ya 1 kati ya mikoa ya Kenya 7,630,300 42/km² | |
Lugha mkoani | Kikalenjin Kimaa Kikuyu | |
Mkoa wa Bonde la Ufa ni mkubwa kati ya mikoa minane ya Kenya. Umepakana na Sudani, Ethiopia, Uganda na Tanzania, halafu na mikoa ya Magharibi, Nyanza, Mashariki, Kati na Pwani. Jina latokana na Bonde la Ufa linalopita katika mkoa.
Eneo la mkoa ni 173,854 km² kuna wakazi karibu milioni saba (6,987,036 mwaka 2000). Umbo lake ni kanda ndefu linalounganisha watu wwenye maisha na utamaduni tofauti sana. Makao makuu ya mkoa yapo Nakuru.
Ndani ya mkoa kuna maeneo yenye rutba sana lakini pia nchi yabisi hata jangwa. Maziwa makubwa ya magadi ni tabia mojawapo wa mkoa huu kama vile Ziwa Turkana, Ziwa Nakuru au Ziwa Naivasha.
Watu wa mkoa wa Bonde la Ufa ni wa makabila mengi. Wenyeji ni wafugaji kama Wamassai au Samburu au wakulima kama sehemu kubwa ya Wakalenjin ambao ni kundi la makabila yaliyo karibu kiutamaduni. Kundi kubwa ni Wakalenjin.
Idadi ya wakazi huongezeka haraka. 1989 palikuwa na wakazi milioni 4.9, 1999 tayari na wakazi milioni 6.9 na kadirio la 2007 ni milioni 8.8.
Mwenye kaskazini ya mkoa kunwa wakimbizi wengi kutoka Sudan katika kambi kubwa la Kakuma.
Wilaya za Mkoa wa Bonde la Ufa
haririWilaya (Makao Makuu):
- Baringo (Kabarnet)
- Bomet (Bomet)
- Buret (Litein)
- Kajiado (Kajiado)
- Keiyo (Iten / Tambach)
- Kericho (Kericho)
- Koibatek (Eldama Ravine)
- Laikipia (Nanyuki)
- Marakwet (Kapsowar)
- Nakuru (Nakuru)
- Nandi (Kapsabet)
- Narok (Narok)
- Samburu (Maralal)
- Trans Mara (Kilgoris)
- Trans-Nzoia (Kitale)
- Turkana (Lodwar)
- Uasin Gishu (Eldoret)
- Pokot Magharibi (Kapenguria)
Bonde la Ufa | Kaskazini-Mashariki | Kati | Magharibi | Mashariki | Nairobi | Nyanza | Pwani |