Orodha ya makabila ya Kenya
(Elekezwa kutoka Orodha ya Makabila nchini Kenya)
Hii orodha ya makabila ya Kenya inatokana na orodha ya lugha za Kenya iliyotolewa na Ethnologue.
Ni orodha ya makabila ya watu ambao wamekuwa wanaishi tangu zamani katika eneo ambalo sasa linaitwa Kenya, pamoja na makabila yaliyogawiwa na mipaka baina ya Kenya na nchi za jirani.
Orodha hii haizingatii makabila yanayoishi Kenya kama wakimbizi kutoka vita katika nchi za jirani, wala vikundi vya wahamiaji kutoka nchi za kigeni, kama wahamiaji au wazao wao kutoka Arabia, Uhindi au nchi nyinginezo.
Makabila makuu
haririAsilimia inaonyesha mgao wao ukifananishwa na idadi yote ya Wakenya[1]:
Makabila kwa jumla
haririKuna makabila asilia karibu arubaini nchini Kenya, yakiwemo[2]:
- Waata
- Waaweer (au Waboni)
- Wabajuni
- Waborana
- Waburji
- Wachonyi
- Wachuka
- Wadaasanach
- Wadahalo
- Wadigo
- Waduruma
- Waembu
- Waendo
- Wagikuyu
- Wagiryama
- Wagusii (au Wakisii)
- Wakalenjin (wakijumisha Wapokot, Wamarakwet, Waelgeyo, Wanandi, Wasabaot, Wakipsigis, na Watugen)
- Wakamba
- Wakore
- Wakuria
- Waluo
- Waluhya (au Waluyia, wakijumuisha Wabukusu, Wanyala, Watachoni, Wakabras, Watsotso, Waidakho, Waisukha, Wamaragoli, Wawanga, Watiriki, Wanyore, Wakhayo, Wasamia, Wakisa, Wamarama)
- Wamaasai
- Wamalakote (au Wailwana)
- Wambeere
- Wameru
- Wamijikenda
- Wamwimbi
- Waogiek (au Waokiek)
- Waorma
- Waoromo
- Wapokomo (Wapokomo wa Chini na Wapokomo wa Juu)
- Warendille
- Wasagalla
- Wasamburu
- Wasanye
- Wasengwer
- Wasomali (au Wariyaahe)
- Wasuba
- Waswahili
- Wataita
- Wataveta
- Wateso
- Watharaka
- Waturkana
- Wayaaku
Makabila mengine yasiyo ya Kenya lakini yamekaa nchini kwa miaka mingi ni:
Tanbihi
hariri- ↑ "Kenya is stuck in tribalism, and calls for national unity are all too often manipulative". D+C (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-03-27.
- ↑ Julie Kwach (2022-03-26). "Tribes in Kenya: List and details about the Kenyan tribes". Tuko.co.ke - Kenya news. (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-03-27.
Marejeo
hariri- 1989 Kenya Population Census Ilihifadhiwa 29 Novemba 2006 kwenye Wayback Machine.
- http://www.minorityrights.org/download.php?id=147 Ilihifadhiwa 14 Juni 2008 kwenye Wayback Machine.