Vatikani

(Elekezwa kutoka Vatican)

Mji wa Vatikani ni dola-mji lenye eneo la kilomita za mraba 0,44 tu. Hivyo ni nchi ndogo kuliko zote duniani. Pande zote inazungukwa na Italia.

Uwanja wa Mt. Petro ni sehemu ya Mji wa Vatikani; majengo mengine karibu yote yanayoonekana pichani ni sehemu ya Italia tayari.
Status Civitatis Vaticanae
Stato della Città del Vaticano

Dola la Mji wa Vatikani
Bendera ya Vatikani Nembo ya Vatikani
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa:
Wimbo wa taifa: Inno e Marcia Pontificale (Kiitalia)
Wimbo la Papa
Lokeshen ya Vatikani
Mji mkuu Mji wa Vatikani1
41°54′ N 12°27′ E
Mji mkubwa nchini Mji wa Vatikani
Lugha rasmi Kilatini2, Kiitalia
Serikali Ufalme
Papa Fransisko
Pietro Parolin
Uhuru
Mkataba wa Laterani

11 Februari 1929
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
0.44 km² (ya 232)
Idadi ya watu
 - 2008 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
791 (ya 229)
1,780/km² (ya 6)
Fedha Euro (€)4 (EUR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD .va
Kodi ya simu +395

-


Ramani ya Mji wa Vatikani

Idadi ya wakazi ni 791; raia ni 565 tu (mnamo Oktoba 2008).

Ni nchi ya Papa ambaye ni askofu wa Roma na mkuu wa Kanisa Katoliki duniani kote.

Jina limetokana na kilima cha Vatikani (kwa Kilatini: Mons Vaticanus) ndani ya jiji la Roma, upande wa magharibi wa mto Tiber.

Pamoja na Basilika la Mt. Petro, jengo la kanisa kubwa kuliko yote duniani, Vatikani ina makanisa mengine saba, jumba la Vatikani, ofisi za utawala wa Kanisa Katoliki, mabustani, stesheni ya treni, nyumba za kuishi, hosteli kwa ajili ya mafukara na makumbusho yenye hazina kubwa za sanaa kiasi kwamba nchi nzima inahesabiwa na UNESCO kuwa Urithi wa dunia (tangu mwaka 1984).

Historia

hariri

Mabaki ya Dola la Papa

hariri

Mji wa Vatikani ni mabaki ya Dola la Papa lililotawala sehemu kubwa ya Italia ya Kati kwa karne nyingi hadi 1870.

Tangu 1860 baadhi ya maeneo hayo yalitwaliwa na Ufalme mpya wa Italia uliolenga kuunganisha sehemu zote za peninsula ya Italia.

Utawala wa Papa juu ya mji na mkoa wa Roma ulilindwa na Ufaransa hadi 1870.

Vita ya 1870 kati ya Ujerumani na Ufaransa ililazimisha Ufaransa kuondoa jeshi lake Roma, ambao hivyo ulitekwa na jeshi la Italia tarehe 20 Septemba 1870.

Wakati huo serikali ya Italia ilitaka kumuachia Papa Pius IX sehemu ya mji wa Roma kama eneo lake lakini Papa alikataa akitumaini Wakatoliki wa Italia na nchi nyingine duniani watalazimisha serikali ya Italia kumrudishia mji wote.

Kwa miaka 57 Mapapa walijifungia ndani ya jumba la Vatikani.

Mkataba wa Laterani 1929

hariri

Mwaka 1929 serikali ya Benito Mussolini ilitafuta amani na Papa Pius XI aliyekuwa tayari kukubali mabadiliko.

Mkataba wa Laterani wa 11 Februari 1929 ukampa Papa mamlaka na madaraka ya nchi huru juu ya basilika la Mt. Petro pamoja na maeneo mengine.

Serikali

hariri

Mkuu wa Dola ni Papa mwenyewe, kwa sasa Papa Fransisko (Jorge Mario Bergoglio). Nafasi yake ni kama mfalme wa kuchaguliwa asiyebanwa na katiba au masharti yoyote. Mambo ya utawala yako mkononi mwa gavana anayeteuliwa na Papa pia.

Vatikani ina uhusiano wa kibalozi na nchi 180 duniani kote kupitia Ukulu mtakatifu.

Vatikani ina jeshi dogo kabisa lakini lenye historia ndefu kabisa duniani. Ni kikosi cha Walinzi Waswisi ambacho kipo tangu mwaka 1506 na chenye wanajeshi 100 hivi. Wote ni Wakatoliki raia wa Uswisi kwa kuzaliwa.

Vatikani ina Posta pia, ikitoa stempu na hata sarafu za euro.

 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Vatikani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vatikani kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.