Vita ya Miaka Saba

Vita ya Miaka Saba ilitokea kati ya 1756 hadi 1763. Ilianza kutokana na mashindano ya nchi za Ulaya ikasambaa pande nyingi za dunia. Hivyo imeitwa "Vita Kuu ya Dunia" ya kwanza hata kama jina hili kwa kawaida latumiwa kwa ajili ya vita kati ya 1914 na 1918.

Ushirikiano kati ya nchi za Ulaya mwanzoni wa vita ya miaka 7

WashirikiEdit

Washiriki katika vita hii walikuwa nchi za Ulaya na koloni zao pia watu wa sehemu mablimbali za dunia walioshikamana nao.

Walipopigana walikuwa:

Sababu za vitaEdit

Vita ilianza kwa sababu mbili hasa:

 • ndani ya Amerika ya Kaskazini Ufaransa na Uingereza zilishindana kuhusu upanuzi wa maeneo yao.
 • katika Ulaya Prussia iliwahi kutwaa jimbo la Silesia kutoka Austria na Austria ilitaka kuchukua jimbo hili tena.
 • nchi nyingi za Ulaya ziliogopa uwezo mkubwa mno wa nchi nyingine ikiruhusiwa kushinda vitani hivyo ziliamua kuingilia kati

Mashindano na hofu hizi zilisababisha kutokea kwa makambi haya mawili makubwa.

 
Vituo vikuu vya Waingereza (nyekundu) na Wafaransa (buluu) katika Uhindi kabla ya vita

MapiganoEdit

Mapigano yalitokea katika Ulaya hasa Ujerumani, halafu katika Uhindi, Amerika ya Kaskazini, kwenye visiwa vya Karibi, pwani za Afrika na Ufilipino.

 • Uingereza ilitwaa "Ufaransa mpya" au sehemu ya Kifaransa ya Kanada ya leo na kuwafukuwa Wafaransa katika maeneo magharibi ya koloni zao.
 • Katika Karibi Waingereza walitwaa visiwa vingi vya Wafaransa isipokuwa Martinique na Guadeloupe.
 • Katika Uhindi vituo vya Ufaransa vingi vilitwaliwa isipokuwa Pondicherry iliyobaki kama koloni ndogo ya Ufaransa (hadi 1960). Waingereza kwa kutwaa kipaumbele katika Ubengali waliweka msingi wa utawala wao wa baadaye juu ya Uhindi wote.
 • Katika Afrika Waingereza walitwaa kituo cha St. Louis katika Senegal kutoka Ufaransa (ilirudishwa baada ya vita)
 • Prussia iliweza kutetea jimbo la Silesia dhidi ya Austria ikapata sifa nyingi kwa sababu jeshi lake lilishindana na Waaustria, Warusi na Wafaransa wakati moja. Lakini mmnamo mwaka 1762 nguvu za Prussia zilikwisha ikaelekea kushindwa. Iliokolewa kwa sababu malkia Elizabeth wa Urusi alikufa na mfalme mpya Peter III alimpenda sana mfalme wa Prussia akaamua kupatana amani naye badala ya kumshambulia tena. Hivyo Austria ilibaki kama mpinzani wa pekee ikashindwa.
 
Vita ya miaka 7 katika Amerika ya Kaskazini
buluu: eneo la kifaransa; nyekundu: eneo la Kiingereza kabla ya vita; Ufaransa ilipotea yote

MatokeoEdit

Matokeo makuu ya vita yalikuwaEdit

 • Uingereza ilikuwa nchi yenye koloni nyingi duniani baada ya Hispania ikaelekea kuipita. Pia ilitawala bahari za dunia kwa ilikuwa taifa lenye manowari mengi na vituo pamoja na mabandari kwenye mabara yote.
 • uwezo wa Ufaransa ulipunguzwa ikipotea koloni zake katika Amerika ya Kaskazini na kubaki na maeneo madogo tu katika Karibi na Uhindi.
 • Prussia ilitoka vitani kama nchi muhimu ya tano ya Ulaya pamoja na Ufaransa, Austria, Uingereza, na Urusi.

Matokeo ya baadaye yalikuwa:Edit

 • Msingi wa Kiingereza kuwa lugha ya kwanza duniani uliwekwa kwa sababu kilitumiwa kote katika koloni za Uingereza
 • Ushindi wa Uingereza ulikuwa msingi kwa ajili ya mapinduzi na uhuru wa Marekani miaka 13 baadaye. Walowezi walijifunza mitindo ya vita waliposhiriki katika vita upande wa Uingereza na walitumia ujuzi huu baadaye dhidi ya Uingereza. Kuondolewa kwa Ufaransa kulipungua vizuizi dhidi ya upanuzi wa Marekani katika Amerika ya kaskazini.
 • Uadui wa Ufaransa dhidi ya Uingereza ulibaki ukaimarishwa na kusababisha usaidizi wa Ufaransa kwa waasi wa Amerika ya Kaskazini mwaka 1776 hivyo kuzaliwa kwa taifa jipya la Marekani.
 • Kudhoofishwa kwa Ufaransa kwa sababu ya gharama kubwa ya vita na gharama ya kusaidia Wamarekani baadaye uliathiri uchumi na sifa za utawala wa kifalme na kuwa sababu muhimu ya mapinduzi ya kifaransa
 • Ushindi wa Prussia ulisababisha mashindano ya mfululizo kati Prussia na Austria juu ya kipaumbele katika Ujerumani yaliyoonekana baadaye hadi vita ya 1866.

Picha za watawala wa nchi shiriki za Vita ya miaka sabaEdit