Visasili vya Kigiriki

(Elekezwa kutoka Mitholojia ya Wagiriki)

Viasili vya Kigiriki ni jumla ya visasili vya Ugiriki ya Kale, yaani ukusanyaji wa masimulizi na hadithi kuhusu vyanzo, miungu na mashujaa wao. Ilikuwa moja ya sehemu za dini ya Ugiriki ya Kale.

Utatu wa Kigiriki na mgawanyo wa falme tatu za dunia: Zeus (mbingu), Poseidon (bahari) na Hade (kuzimu). Miungu midogo ni watoto wa watatu hao.
Kichwa cha Sanamu ya Zeu.

Chanzo kikuu kuhusu imani ya Wagiriki wa kale kabisa ni shairi la Theogonia lililotungwa na Hesiodo mnamo mwaka 700 KK.

Nasaba ya miungu ya Titani

hariri
 
Titani aliyepinduliwa.

Watitani ni nasaba ya kwanza ya miungu katika visasili vya Kigiriki. Kiasili ni Watitani 12, wakiwemo 6 wa kiume na 6 wa kike wanaofunga ndoa kati yao na kuzaa Watitani wengine. Mkuu wao alikuwa Kronos hadi alipopinduliwa na mwanawe Zeus aliyeanzisha nasaba ya pili ya miungu ya Olimpos. Sehemu ya Watitani walijaribu kumpinga Zeus wakafukuzwa mbinguni.

  1. Hyperion – mungu wa nuru na jua, aliyemzaa mungu wa jua Helios, mungu wa kike wa mwezi Selene na mungu wa kike wa mapambazuko Eos
  2. Iapetosmume wa Klymene (binti wa Okeanos), aliyefukuzwa baadaye mbinguni
  3. Koios, aliyefukuzwa baadaye mbinguni
  4. Kreios – mume wa Eurybia
  5. Kronos – mkuu wa Watitani, baba wa Zeus, mume wa Rhea; alipinduliwa na Zeus akafukuzwa mbinguni akitawala kisiwa cha heri
  6. Mnemosyne – mama wa Muzi tisa
  7. Okeanos – mkuu wa bahari na himaya ya maji, baba wa miungu yote ya mito na pepo wa bahari na visima
  8. Phoibe – mke wa Koios, mungu wa mwezi
  9. Rheamama wa Hestia, Demeter, Hera, Hades, Poseidon na Zeus; alimfuata mumewe Kronos alipoondoka mbinguni
  10. Themis – mungu wa kike wa haki na mke wa pili wa Zeus; anajua wakati ujao
  11. Tethys – mke wa Okeanos
  12. Theia – mke wa Hyperion

Miungu Kumi na Miwili ya Olimpos

hariri
Jina la Kigiriki Jina la Kiswahili Maelezo
Aφροδίτη (Afrodítē) Afrodita Mungu wa kike wa upendo na uzuri.
Aπόλλων (Apóllōn) Apolo Mungu wa nuru na ushairi.
Άρης (Árēs) Ares Mungu wa vita.
Άρτεμις (Ártemis) Artemi Mungu wa kike wa uwindo.
Αθηνά (Athēná) Athena Mungu wa kike wa elimu na hekima.
Δημήτηρ (Dēmḗtēr)

Δήμητρα (Dḗmētra)

Demetra Mungu wa kike wa mimea na kilimo.
Διόνυσος (Diónysos) Dioniso Mungu wa divai.
Έρως (Érōs) Ero Mungu wa mapenzi.
ᾍδης (Ádēs) Hade Mungu wa kuzimu na bwana wa waliokufa.
Ήφαιστος (Ḗfaistos) Hefaisto Mungu wa uhunzi.
Ήρα (Ḗra) Hera Mungu wa kike wa ndoa na malkia ya miungu.
Ερμής (Ermḗs) Herme Mjumbe wa miungu.
Ἑστία (Estía) Hestia Mungu wa kike wa moto.
Ποσειδῶν (Poseidṓn)

Ποσειδώνας (Poseidṓnas)

Poseidoni Mungu wa bahari.
Ζεύς (Zeús)

Δίας (Días)

Zeu Mungu wa radi na mfalme wa miungu.

Protogenoi

hariri
Jina la Kigiriki Jina la Kiswahili Maelezo
Αιθήρ (Aithḗr) Aitheri Mungu wa anga.
Ἀνάγκη (Anágkē) Ananka Mungu wa kike wa kudra.
Έρεβος (Érevos) Erebo Mungu wa giza.
Γαία (Gaía) Gaya Mungu wa kike wa ardhi.
Ημέρα (Ēméra) Hemera Mungu wa kike wa mchana.
Χάος (Kháos) Khaos
Χρόνος (Khrónos) Khrono Mungu wa muda.
αἱ Nῆσοι (ai Nḗsoi) Visiwa Miungu ya kike wa visiwa.
Νύξ (Nýx) Niksi Mungu wa kike wa usiku.
Ουρανός (Ouranós) Urano Mungu wa mbingu.
Ούρος (Oúros) Milima Miungu ya milima.
Πόντος (Póntos) Ponto Mungu wa bahari ya dunia nzima.
Τάρταρος (Tártaros) Tartaro Mungu wa tartaro.
Θάλασσα (Thálassa) Thalasa Malkia wa bahari na mke wa Ponto.

Titani Kumi na Wawili

hariri
Jina la Kigiriki Jina la Kiswahili Maelezo
Ὑπερίων (Yperíōn) Hiperioni Mungu wa nuru ya jua.
Ἰαπετός (Iapetós) Yapeto
Κοῖος (Koïos) Koyo Mungu wa fahamu.
Κρεῖος (Kreïos) Kreyo
Κρόνος (Krónos) Krono Mfalme wa Titani.
Mνημοσύνη (Mnēmosýnē) Mnemosina Mungu wa kike wa kumbukumbu.
Ὠκεανός (Ōkeanós) Okeano Mungu wa bahari kuu.
Φοίβη (Foívē) Foiba
Ῥέα (Réa) Rea Malkia wa Titani na mke wa Krono.
Τηθύς (Tēthýs) Tethi Mungu wa kike wa mito.
Θεία (Theía) Theya Mungu wa kike wa uonaji.
Θέμις (Thémis) Themi
  • Siklopsi (Κύκλωψ) - majitu-chongo watatu.
    • Arge (Ἄργης)
    • Bronte (Βρόντης)
    • Sterope (Στερόπης)
  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.