Yohane Mbatizaji
Yohane Mbatizaji (7 K.K. - 29 B.K. hivi) alikuwa nabii wa Uyahudi aliyeishi wakati wa Yesu wa Nazareti na kumtangulia miezi tu kuzaliwa, kuanza utume na kuuawa.
Kufuatana na Injili ya Luka sura 1-2 Yohane na Yesu walikuwa ndugu na mama zao walikuwa wazito kwa wakati mmoja.
Habari zake zinapatikana katika Biblia ya Kikristo na katika vitabu vya mwanahistoria Yosefu Flavius.
Anaheshimiwa na Wakristo na Waislamu kama nabii na mtakatifu.
Pengine sikukuu yake muhimu zaidi ni ile ya kuzaliwa [1] (inayoadhimishwa na Kanisa la magharibi tarehe 24 Juni [2], miezi sita kabla ya Krismasi), lakini ipo pia sikukuu ya kifodini chake [3] tarehe 29 Agosti [4].
Utoto
haririKadiri ya Injili ya Luka, Yohane alizaliwa kimuujiza na kuhani mzee Zakaria na mke wake tasa Elizabeti[5].
Bado mtoto alikwenda kuishi jangwani, labda kutokana na kifo cha wazazi. Wataalamu mbalimbali wanadhani kwamba huko alikuwa akiishi kati ya Waeseni, wafuasi wa madhehebu ya Kiyahudi yenye msimamo mkali hata kuliko ule wa Mafarisayo.
Mhubiri katika jangwa
haririAlipofikia utu uzima alianza kuhubiri "mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio" (Luka 3,1) yaani mnamo 27/29 BK.
Yohane alikuwa mhubiri aliyewaonya kwa ukali wasikilizaji wake na kudai wajiandae kwa hukumu ya Mungu.
Akawakaribisha wapate ubatizo wa maji kama alama ya utakaso na mwanzo wa maisha mapya.
Injili ya Mathayo katika sura ya 3 inasimulia: "4 Yohane alivaa vazi lililoshonwa kwa manyoya ya ngamia, na ukanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni. 5 Basi, watu kutoka Yerusalemu, kutoka mkoa wote wa Yudea na sehemu zote za kandokando ya mto Yordani, walimwendea, 6 wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mto Yordani."
Alimbatiza pia Yesu ambaye naye baadaye akaanza kuhubiri.
Hivyo katika Injili Yohane anatazamwa kama mtangulizi wa Yesu aliyetangaza ujio wake na kumtambulisha kama "Mwanakondoo wa Mungu aondoaye dhambi ya ulimwengu" na atakayebatiza kwa Roho Mtakatifu.
Kifo cha Yohane
haririYohane katika mahubiri yake alipinga bila hofu matendo ya mfalme Herode Antipa hata akakamatwa naye na kufungwa katika ngome ya Makeronte, katika Yordani ya leo.
Kufuatana na Injili ya Marko sura ya 6 aliuawa gerezani huko alivyotaka Herodia mke wa mfalme, akakatwa kichwa kwa ombi la Salome, binti yake, nacho kilipelekwa katika sinia au bakuli mbele ya mfalme na wageni wake wakiwa wanasherehekea sikukuu yake ya kuzaliwa.
Hivyo huyo mtangulizi wa Bwana, kama taa iwakayo na kung'aa, alishuhudia ukweli kwa maisha na mauti yake vilevile.
Wafuasi wa Yohane
haririYohane alikuwa pia na kundi la wafuasi walioendelea kama ushirika baada ya kifo chake.
Dini ya Wamandayo inadai kuwa imetokana na ushirika huo: katika Kurani hao wanaitwa "sabiyuna" au wabatizaji.
Nabii Yahya katika Kurani
haririYohane anatajwa kwa heshima katika Kurani pia, kwa jina la nabii Yahya (يحيى بن زكريا, Yahya ibn Zakariya).
Fuvu la kichwa
haririKichwa cha Yohane kiliaminiwa kimeweza kutunzwa kikaheshimiwa kama salia takatifu.
Kuna vichwa mbalimbali vilivyotajwa kuwa kichwa cha Yohane.
Kaburi moja la kichwa kipo mjini Dameski kilipokuwa ndani ya kanisa kuu, na baada ya Waislamu kubomoa kanisa, kaburi lilitunzwa na liko sasa ndani ya msikiti wa Umawiya.
Kichwa kingine kinachoitwa ni cha Yohane chaonyeshwa katika kanisa la "San Silvestro in Capite" mjini Roma; kingine huko Amiens (Ufaransa).
Kuna pia mikono ya Yohane inayoonyeshwa mahali mbalimbali.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/20300
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/24300
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ 1:5 Wakati Herode alipokuwa mfalme wa Yudea, kulikuwa na kuhani mmoja jina lake Zakaria, wa kikundi cha Abia. Mke wake alikuwa anaitwa Elisabeti, naye alikuwa wa ukoo wa kuhani Aroni. 6 Wote wawili walikuwa wanyofu mbele ya Mungu, wakiishi kwa kufuata amri na maagizo yote ya Bwana bila lawama. 7 Lakini hawakuwa wamejaliwa watoto kwa vile Elisabeti alikuwa tasa, nao wote wawili walikuwa wazee sana. 8 Siku moja, ilipokuwa zamu yake ya kutoa huduma ya ukuhani mbele ya Mungu, 9 Zakariya alichaguliwa kwa kura, kama ilivyokuwa desturi, kuingia hekaluni ili afukize ubani. 10 Watu, umati mkubwa, walikuwa wamekusanyika nje wanasali wakati huo wa kufukiza ubani. 11 Malaika wa Bwana akamtokea humo ndani, akasimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia ubani. 12 Zakariya alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia. 13 Lakini malaika akamwambia, "Zakariya, usiogope, kwa maana sala yako imesikilizwa, na Elisabeti mkeo atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yohane. 14 Utakuwa na furaha kubwa na watu wengi watashangilia kwa sababu ya kuzaliwa kwake. 15 Atakuwa mkuu mbele ya Bwana. Hatakunywa divai wala kileo, atajazwa Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mama yake. 16 Atawaelekeza wengi wa watu wa Israeli kwa Bwana Mungu wao. 17 Atamtangulia Bwana akiongozwa na nguvu na roho kama Eliya. Atawapatanisha kina baba na watoto wao; atawafanya wasiotii wawe na fikira za uadilifu, na hivyo amtayarishie Bwana watu wake." 18 Zakariya akamwambia huyo malaika, "Ni kitu gani kitakachonihakikishia jambo hilo? Mimi ni mzee, hali kadhalika na mke wangu." 19 Malaika akamjibu, "Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele ya Mungu, na nimetumwa niseme nawe, nikuletee hii habari njema. 20 Sikiliza, utakuwa bubu kwa sababu huyasadiki haya maneno yatakayotimia kwa wakati wake. Hutaweza kusema mpaka hayo niliyokuambia yatakapotimia." 21 Wakati huo, wale watu walikuwa wanamngoja Zakariya huku wakishangaa juu ya kukawia kwake Hekaluni. 22 Alipotoka nje, hakuweza kusema nao. Ikawa dhahiri kwao kwamba alikuwa ameona maono Hekaluni. Lakini akawa anawapa ishara kwa mikono, akabaki bubu. 23 Zamu yake ya kuhudumu ilipokwisha, alirudi nyumbani. 24 Baadaye Elisabeti mkewe akapata mimba. Akajificha nyumbani kwa muda wa miezi mitano, akisema: 25 "Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana; ameniangalia na kuniondolea aibu niliyokuwa nayo mbele ya watu."
Marejeo
haririVitabu juu yake
hariri- Brooks Hansen (2009) John the Baptizer: A Novel. New York: W. W. Norton. ISBN 978-0-393-06947-1
- Murphy, Catherine M. (2003) John the Baptist: Prophet of Purity for a New Age. Collegeville: Liturgical Press. ISBN 0-8146-5933-0
- Taylor, Joan E. (1997) The Immerser: John the Baptist within Second Temple Judaism. Grand Rapids: Eerdmans. ISBN 0-8028-4236-4
- W. Barnes Tatum (1994) John the Baptist and Jesus: A Report of the Jesus Seminar., Sonoma, California: Polebridge Press, 1994, ISBN 0-944344-42-9
- Webb, Robert L. (1991) John the Baptizer and Prophet: a Socio-Historical Study. Wipf and Stock Publishers. ISBN 978-1-59752-986-0 (first published Sheffield: JSOT Press, 1991)
Taarifa zake katika vyanzo vya zamani
hariri- Josephus wrote that "...Herod slew him, who was a good man, and commanded the Jews to exercise virtue, both as to righteousness towards one another and piety towards God, and so to come to baptism; for that the washing would be acceptable to him, if they made use of it, not in order to the remission of some sins, but for the purification of the body; supposing still that the soul was thoroughly purified beforehand by righteousness." (Josephus, AJ, 18.5.2)
Mtazamo wa Kiislamu
hariri- Rippin, A.. "Yahya b. Zakariya". In P.J. Bearman, Th. Bianquis, C.E. Bosworth, E. van Donzel, W.P. Heinrichs. Encyclopaedia of Islam Online. Brill Academic Publishers.
.
- J.C.L Gibson, John the Baptist in Muslim writings, in MW, xlv (1955), 334-345
Madondoo kutoka Qur'an
hariri- Appraisals for Yahya: 6:85 Archived 3 Desemba 2005 at the Wayback Machine., 19:7 Archived 3 Desemba 2005 at the Wayback Machine., 19:12 Archived 4 Desemba 2005 at the Wayback Machine., 19:13 Archived 27 Machi 2007 at the Wayback Machine., 19:14 Archived 4 Desemba 2005 at the Wayback Machine., 19:15 Archived 4 Desemba 2005 at the Wayback Machine.
- Yahya's prophecy: 3:39 Archived 3 Desemba 2005 at the Wayback Machine., 6:85 Archived 3 Desemba 2005 at the Wayback Machine., 19:12 Archived 4 Desemba 2005 at the Wayback Machine.
Viungo vya nje
haririWikisource has the text of the 1911 Encyclopædia Britannica article John the Baptist. |
- Catholic Encyclopedia: St. John the Baptist
- Jewish Encyclopedia: John the Baptist
- Prophet Yahya (John) in the light of Islamic tradition.
- Prophet John (Yahya) Archived 10 Julai 2012 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yohane Mbatizaji kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |