Umoja wa Kilatini (kwa Kilatini: Unio Latina; kwa Kiingereza: Latin Union) ni shirika la kimataifa linalounganisha nchi mbalimbali zinazotumia rasmi lugha za Kirumi. Umoja huo ulianzishwa mnamo mwaka 1954 kama mkataba wa kimataifa na tangu mwaka 1983 ulikuwa taasisi halisi yenye ofisi mjini Paris. Ofisi kuu ilifungwa tena mnamo mwaka 2012 kwa sababu wanachama wengi hawakulipa ada zao.

Makao yake makuu yalikuwa Paris, Ufaransa, lengo lake lilikuwa kulinda na kukuza urithi wa kitamaduni wa mataifa yenye lugha za Kirumi. Idadi ya wanachamama ilifikia nchi 36 za Amerika Kaskazini, Amerika Kusini, Ulaya, Afrika, na kanda la Asia na Pasifiki. [1]

Majina rasmi ya Umoja wa Kilatini yalikuwa: Union Latine kwa Kifaransa, Unione Latina kwa Kiitalia, Uniao Latina kwa Kireno, Uniunea Latina kwa Kiromania, Union Latina kwa Kihispania na Unio Llatina kwa Kikatalunya.

Lugha rasmi hariri

Lugha rasmi za Umoja wa Kilatini zilikuwa Kihispania, Kifaransa, Kiitalia, Kireno, Kiromania, na Kikatalani. Kihispania, Kifaransa, Kiitalia na Kireno zilitumika kama lugha za kufanya kazi. Maandishi yote ya kuenezwa kwa jumla yalitafsiriwa katika lugha hizo nne, na nyingine pia zikienda kwa Kiromania na Kikatalani.

Nchi wanachama hariri

Nchi zinazotumia Kihispania hariri

Nchi zinazotumia Kifaransa hariri

Nchi zinazotumia Kireno hariri

Nchi zinazotumia Kiitalia hariri

Nchi zinazotumia Kiromania hariri

Nchi zinazotumia Kikatalani hariri

Nchi watazamaji hariri

Marejeo hariri

  1. Unión Latina; Estados miembros. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-12-28. Iliwekwa mnamo 2009-01-05.

Viungo vya nje hariri

  • (in Spanish, French, Italian, Portuguese, Romanian, and Catalan) Official site