Papa Yohane XXIII

Mkuu wa Kanisa Katoliki kutoka 1958 hadi 1963
(Elekezwa kutoka Yohane XXIII)

Papa Yohane XXIII (25 Novemba 18813 Juni 1963) alikuwa Papa kuanzia tarehe 28 Oktoba/4 Novemba 1958 hadi kifo chake[1]. Alitokea Sotto il Monte, Bergamo, Italia[2].

Mtakatifu Yohane XXIII.

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Angelo Giuseppe Roncalli. Watu walipenda kumuita "Papa mwema" kutokana na tabia yake ya kuvutia.

Alimfuata Papa Pius XII akafuatwa na Papa Paulo VI.

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 3 Septemba 2000, halafu Papa Fransisko alimtangaza mtakatifu tarehe 27 Aprili 2014.

Mtu mwenye utu usio wa kawaida, kwa maisha, kazi na ari yake kubwa ya kichungaji alijitahidi kueneza kwa watu wote wingi wa upendo wake wa Kikristo na kuhamasisha umoja wa kidugu kati ya mataifa[3].

Umuhimu wa Papa huyu ni hasa kwamba aliitisha Mtaguso wa pili wa Vatikano (1962-1965) ambao ulikutanisha karibu maaskofu wote wa Kanisa Katoliki (wakati huo 3,000 hivi) na kuleta matengenezo mbalimbali ndani ya Kanisa hilo ili utume wake duniani kote ufanikiwe kama alivyotamani.

Ndiyo sababu sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 11 Oktoba[4], siku aliyofungua mtaguso mkuu huo.

Maisha

hariri

Angelo Giuseppe Roncalli alikuwa mtoto wa nne kati ya 14 wa familia ya mkoa wa Lombardia.[5] Alipata upadrisho tarehe 10 Agosti 1904 akapangwa sehemu mbalimbali, hata kama balozi wa Papa nchini Ufaransa, Bulgaria, Ugiriki na Uturuki.

Tarehe 12 Januari 1953 Papa Pius XII alimfanya Roncalli kuwa kardinali pamoja na kuwa Patriarki wa Venice.

Roncalli alichaguliwa kuwa Papa tarehe 28 Oktoba 1958 akiwa na umri wa miaka 76 baada ya kura kupigwa mara 11 na tofauti na matarajio.

Papa Yohane XXIII alizidi kushangaza wote alipoitisha mtaguso mkuu pamoja na Sinodi ya Roma na urekebisho wa Mkusanyo wa Sheria za Kanisa tarehe 25 Januari 1959.

Yohane alifariki kwa kansa ya tumbo, miezi miwili baada ya kutoa barua yake maarufu Pacem in Terris kuhusu amani duniani.

Heshima baada ya kifo

hariri

Alizikwa katika mahandaki ya Basilika la Mt. Petro tarehe 6 Juni 1963 na kesi ya kumtangaza mtakatifu ilifunguliwa tarehe 18 Novemba 1965 na mwandamizi wake Papa Paulo VI. Baada ya kukubaliwa heshima kama Venerable tarehe 20 Desemba 1999, alitangazwa mwenye heri tarehe 3 Septemba 2000 pamoja na Papa Pius IX na watatu wengine.

Baada ya hatua hiyo, masalia yalisogezwa kwenye altare ya Mt. Jeromu yaweze kuonekana na waamini kwa urahisi.

Tarehe 5 Julai 2013, Papa Fransisko alisamehe uthibitisho wa muujiza wa pili aweze kutangazwa mtakatifu pamoja na Papa Yohane Paulo II tarehe 27 April 2014.[6][7]

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  2. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  3. https://www.santiebeati.it/dettaglio/55725
  4. Martyrologium Romanum
  5. "Pope John XXIII". IT: Vatican. Iliwekwa mnamo 2013-06-23.
  6. "Popes John Paul II, John XXIII to be declared saints in April", World News, Fox, Sep 30, 2013{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Antonimuthu, Rajamanickam (27 Aprili 2014). "Pope Francis declares Popes John Paul II and John XXIII Saints" (YouTube). Iliwekwa mnamo 27 Aprili 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Maandishi yake

hariri

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Yohane XXIII kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.