Historia ya Urusi inahusu historia ya eneo ambalo leo linaunda nchi inayoitwa Shirikisho la Urusi.

Ramani ya aina za utamaduni za Urusi magharibi wakati wa ujio wa Wavarangi na kabla ya uenezi wa Waslavi.
Dola la Kiev, chanzo cha Urusi

Historia ya kale

hariri

Urusi kama nchi ya pekee ilianza polepole pale ambako makabila ya wasemaji wa Kislavoni cha Mashariki walipoanza kujenga maeneo yao kuanzia karne ya 8 BK.

Waviking waliunda dola la kwanza katika eneo la Kiev, wakalitawala kama dola la Kislavoni. Wenyewe waliingia haraka katika lugha na utamaduni wa wenyeji, lakini waliacha jina lao kwa sababu "Rus" kiasili ilikuwa jina la Waskandinavia wale kutoka Uswidi ya leo.

Mwaka 988 Kiev ilipokea Ukristo wa Kiorthodoksi kutoka Bizanti. Tukio hilo liliathiri moja kwa moja utamaduni na historia yote iliyofuata.

Dola la Kiev liliporomoka kutokana na mashambulio ya Wamongolia baada ya Jingis Khan, na maeneo madogo zaidi yalijitokeza yaliyopaswa kukubali ubwana wa Wamongolia.

Upanuzi wa utemi wa Moscow

hariri
 
Utemi wa Moscow 1390 - 1525

Kubwa kati ya maeneo yale madogo ulikuwa utemi wa Moscow. Watemi wa Moscow walichukua nafasi ya kwanza kuunganisha Waslavoni wa Mashariki dhidi ya Wamongolia na kupanua utawala wao.

Baada ya anguko la Konstantinopoli mwaka 1453 watawala wa Moscow walipokea cheo cha Kaisari wa Roma kilichoitwa "tsar" na kuwa cheo cha watawala wa Urusi hadi mwaka 1917.

Mpaka karne ya 18 eneo la Moscow lilikuwa tayari kubwa likabadilika kuwa Milki ya Kirusi iliyoendelea kupanuka katika Siberia na Asia ya Kati, ikawa kati ya milki kubwa kabisa za historia ikienea kutoka Poland upande wa magharibi hadi bahari ya Pasifiki upande wa mashariki.

Matengenezo ya kisiasa chini ya Petro I

hariri

Tsar Petro I (1689-1725) alitambua ya kwamba nchi yake ilikuwa nyuma upande wa teknolojia na elimu kulingana na mataifa ya Ulaya. Alianzisha mabadiliko mengi ya kuiga mfano wa Ulaya ya Magharibi akahamisha mji mkuu kutoka Moscow kwenda mji mpya aliounda sehemu ya magharibi ya milki yake akauita Sankt Peterburg.

Tangu wakati wa Petro I nchi ilishiriki katika siasa ya Ulaya pamoja na vita vingi vya huko.

Mwanzo wa karne ya 19 milki ikashambuliwa na Napoleon Bonaparte aliyeteka Moscow lakini Warusi walifaulu kuwafukuza maadui kwa msaada wa baridi iliyoua askari wengi wa Ufaransa.

Upanuzi barani Asia

hariri
 
Upanuzi wa Urusi 1533 - 1896

Matsar wa Urusi waliendelea kutawala kwa kuwa na mamlaka zote bila kushirikisha wananchi jinsi ilivyokuwa kawaida katika sehemu nyingine za Ulaya. Miji iliona maendeleo ya viwanda na jamii ya kisasa, lakini sehemu kubwa ya wakulima waliendelea kukaa chini ya utawala wa makabaila.

Katika sehemu ya pili ya karne ya 19 Urusi ulipanua utawala wake juu ya maneo makubwa ya Asia ya Kati na milima Kaukasus ukashindana na Milki ya Osmani, Uajemi na athira ya Uingereza katika Asia.

Mapinduzi za 1905 na 1917

hariri
 
Picha za Vita kati ya Japani na Urusi
Juu: Manowari; Picha kwa mwendo wa saa: Wanajeshi Wajapani, Wanafarasi Wajapani, Manowari 2 za Urusi, Wanajeshi Warusi wakitazama maiti za Wajapani mbele ya Port Arthur
 
Eneo la vita: Nyekundu ni Manchuria; rasi ya Liaodong inaitwa "Daijan" (katikati ya ramani katika Manchuria kusini upande wa bahari)

Mwanzoni mwa karne ya 20 Urusi ukaonekana tena kuwa nyuma ya nchi za magharibi na sababu kuu ilikuwa nafasi kubwa ya serikali iliyojitahidi kusimamia mabadiliko yote katika jamii na kuzuia mabadiliko yaliyoonekana magumu machoni pa Tsar, pa makabaila na pa maaskofu wa Kanisa la Kiorthodoksi.

Mwaka 1903 upanuzi wa Urusi katika Asia uligongana na upanuzi wa Japan na kusababisha vita ya Japani na Urusi ya 1905. Sababu kuu ya vita ilikuwa mashindano ya nchi zote mbili juu ya athira na kipaumbele katika Korea na Manchuria. Urusi ulishindwa, hivyo ililazimika kujiondoa katika Manchuria na Korea na kukubali maeneo haya mawili kuwa chini ya athira ya Japani. Ilikuwa mara ya kwanza kwa taifa la Asia kushinda nchi ya "watu weupe" wa Ulaya tangu zama za kati.

Tukio hili lilisababisha mapinduzi ya Urusi ya 1905. Tsar Nikolas alipaswa kukubali uchaguzi wa bunge la duma kwa mara ya kwanza. Hata hivyo haki za duma zilikuwa chache na mabadiliko yalitokea polepole mno.

Urusi ulijiunga mwaka 1914 na vita kuu ya kwanza ya dunia ukisimama upande wa Uingereza na Ufaransa dhidi ya Ujerumani na Austria-Hungaria. Vita havikuenda vizuri, wananchi wakaona njaa na mapinduzi ya Februari 1917 yakamfukuza Tsar aliyejiuzulu.

Vita vikaendelea na Wajerumani walizidi kusogea mbele. Serikali mpya ya bunge ikapinduliwa katika mwezi wa Oktoba 1917 na mapinduzi ya Bolsheviki chini ya kiongozi wao Vladimir Ilyich Lenin.

Utawala wa kikomunisti na Umoja wa Kisovyeti

hariri
 
Lenin na Stalin, viongozi na watawala wa Urusi wa kikomunisti

Huo ulikuwa mwanzo wa vita ya wenyewe kwa wenyewe. Wakomunisti chini ya Lenin walishinda na kugeuza Urusi kuwa Umoja wa Kisoveti tangu mwaka 1922, wakitawala kwa mfumo wa kiimla wa chama chao. Ili kurahisisha utawala wao Wakomunisti waliamua kutawala Urusi wa awali kwa muundo wa shirikisho, wakaunda jamhuri mbalimbali kufuatana na mataifa ndani ya eneo hilo kubwa.

Urusi lilikuwa sasa jina la jamhuri kubwa katika umoja huu nao ukaitwa Shirikisho la Jamhuri ya Kisovyiet ya Kijamii ya Kirusi.

Kikatiba jamhuri hizo zote zilikuwa nchi huru lakini hali halisi zilitawaliwa zote kutoka makao makuu ya chama cha kikomunisti huko Moscow. Katiba hiyo ilipata umuhimu tangu 1989, wakati wa mwisho wa utawala wa Wakomunisti ambako jamhuri zote zilitafuta uhuru wao zikaachana na Umoja.

Mji mkuu Sant Peterburg ulibadilishwa jina kuwa Leningrad na baadaye makao makuu ya nchi yakahamishwa tena kwenda Moscow.

Kiongozi aliyemfuata Lenin mwaka 1924 alikuwa Josef Stalin aliyeweza kugeuza utawala wa chama kuwa utawala wake mwenyewe akiongoza kwa jina la Katibu Mkuu wa chama cha kikomunisti.

Mwaka 1939, mwanzoni mwa vita kuu ya pili ya dunia Stalin alipatana na Ujerumani wa Adolf Hitler kugawa maeneo ya Poland na nchi za Baltiki kati yao lakini mwaka 1941 Hitler alishambulia pia Umoja wa Kisovyeti.

Warusi walipoteza askari milioni kadhaa, lakini waliweza kuwazuia Wajerumani wasiteke Moscow na Leningrad. Kwa msaada wa Marekani Warusi waliweza kurudisha jeshi la Ujerumani na kusogea magharibi. Umoja wa Kisovyeti ukawa kati ya nchi washindi wa vita kuu ya pili ya dunia.

Mashindano ya vita baridi dhidi ya Marekani

hariri
 
Ndege za kivita za Kisovyeti na Kimarekani zikitazamiana angani

Tangu mwaka 1945 jeshi la Urusi lilikaa katika nchi zote za Ulaya ya Mashariki hadi katikati ya Ulaya. Katika nchi hizo zote serikali za kikomunisti zilianzishwa na kusimamiwa na ofisi kuu ya chama cha kikomunisti huko Moscow.

Urusi ulikuwa kiongozi wa nchi za kijamaa, ukishindana katika vita baridi dhidi ya nchi za magharibi zilizoongozwa na Marekani. Athira ya Umoja wa Kisovyeti ilipanuka hadi Afrika, Asia na Amerika ya Kati ambako nchi mbalimbali zilianza kuiga mtindo wa kikomunisti.

Kusambaratika kwa Umoja kwa Kisovyeti

hariri
 
Mikhail Gorbachev, kiongozi wa Kisovyeti aliyesimamia kusambaratika ya Umoja wa Kisovyeti

Utawala wa kikomunisti uliendelea hadi mwaka 1990. Mwishoni matatizo ya uchumi yalizidi kwa sababu mfumo wa uchumi ulioongozwa moja kwa moja na serikali kuu, pamoja na utaratibu wa kiimla uliozuia wananchi kupinga siasa ya viongozi na kuleta hoja tofauti, ulisababisha tena nchi kubaki nyuma.

Tangu mwaka 1990 jamhuri kadhaa za Umoja wa Kisovyeti ziliondoka katika umoja na kutangaza uhuru wao ilhali serikali ilishindwa nguvu ya kuwazuia. Mwaka 1991 jamhuri wanachama za mwisho Urusi, Belarus na Ukraine ziliamua kumaliza Umoja wa Kisovyeti.

Urusi mpya

hariri

Tangu mwaka 1991 Urusi ulipungukiwa na maeneo mengi yaliyotwaliwa katika karne ya 19 na ya 18, ukabaki peke yake ingawa bado ni dola kubwa kuliko yote duniani.

Marais wa Urusi baada ya 1991 walikuwa Boris Yeltsin na Vladimir Putin.

Dmitry Medvedev alichaguliwa kuwa rais wa Urusi mwaka 2008 na mtangulizi wake Vladimir Putin akawa waziri mkuu, akifuatwa tena na raisi Putin.

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri

Kwa jumla

hariri
  • Bushkovitch, Paul. A Concise History of Russia (2011) excerpt and text search
  • Freeze, Gregory L. (ed.). Russia: A History. 2nd ed. New York: Oxford University Press, 2002. ISBN 0-19-860511-0.
  • Jelavich, Barbara. St. Petersburg and Moscow: tsarist and Soviet foreign policy, 1814-1974 (1974)
  • McKenzie, David & Michael W. Curran. A History of Russia, the Soviet Union, and Beyond. 6th ed. Belmont, CA: Wadsworth Publishing, 2001. ISBN 0-534-58698-8.
  • Perrie, Maureen, et al. The Cambridge History of Russia. (3 vol. Cambridge University Press, 2006). excerpt and text search
  • Riasanovsky, Nicholas V. and Mark D. Steinberg. A History of Russia. 7th ed. New York: Oxford University Press, 2004, 800 pages. ISBN 0-19-515394-4
  • Stone, David. A Military History of Russia: From Ivan the Terrible to the War in Chechnya excerpts
  • Ziegler; Charles E. The History of Russia (Greenwood Press, 1999) online edition Archived 30 Machi 2009 at the Wayback Machine.

Dola la Urusi

hariri
  • Christian, David. A History of Russia, Central Asia and Mongolia. Vol. 1: Inner Eurasia from Prehistory to the Mongol Empire. Malden, MA: Blackwell Publishers, 1998. ISBN 0-631-20814-3.
  • De Madariaga, Isabel. Russia in the Age of Catherine the Great (2002), comprehensive topical survey
  • Fuller, William C. Strategy and Power in Russia 1600-1914 (1998) excerpts
  • Hughes, Lindsey. Russia in the Age of Peter the Great (Yale University Press, 1998), Comprehensive topical survey.
  • Lincoln, W. Bruce. The Romanovs: Autocrats of All the Russias (1983) excerpt and text search, sweeping narrative history
  • Manning, Roberta. The Crisis of the Old Order in Russia: Gentry and Government. Princeton University Press, 1982.
  • Mironov, Boris N., and Ben Eklof. The Social History of Imperial Russia, 1700-1917 (2 vol Westview Press, 2000) vol 1 online Archived 29 Septemba 2008 at the Wayback Machine.; vol 2 online Archived 29 Septemba 2008 at the Wayback Machine.
  • Moss, Walter G. A History of Russia. Vol. 1: To 1917. 2d ed. Anthem Press, 2002.
  • Pipes, Richard. Russia under the Old Regime (2nd ed. 1997)
  • Seton-Watson, Hugh. The Russian Empire 1801-1917 (Oxford History of Modern Europe) (1988) excerpt and text search

Chini ya Ukomunisti

hariri
  • Chamberlin, William Henry. The Russian Revolution 1917-1921 (2 vol 1935)
  • Cohen, Stephen F. Rethinking the Soviet Experience: Politics and History since 1917. (Oxford University Press, 1985)
  • Fitzpatrick, Sheila. The Russian Revolution. (Oxford University Press, 1982), 208 pages. ISBN 0-19-280204-6
  • Gregory, Paul R. and Robert C. Stuart, Russian and Soviet Economic Performance and Structure (7th ed. 2001)
  • Hosking, Geoffrey. The First Socialist Society: A History of the Soviet Union from Within (2nd ed. Harvard UP 1992) 570pp
  • Kort, Michael. The Soviet Colossus: History and Aftermath (7th ed. 2010) 502pp
  • Kotkin, Stephen. Stalin: Paradoxes of Power, 1878–1928 (2014)
  • Library of Congress. Russia: a country study edited by Glenn E. Curtis. (Federal Research Division, Library of Congress, 1996). online
  • Lincoln, W. Bruce. Passage Through Armageddon: The Russians in War and Revolution, 1914-1918 (1986)
  • Lewin, Moshe. Russian Peasants and Soviet Power. (Northwestern University Press, 1968)
  • McCauley, Martin. The Rise and Fall of the Soviet Union (2007), 522 pages.
  • Moss, Walter G. A History of Russia. Vol. 2: Since 1855. 2d ed. Anthem Press, 2005.
  • Nove, Alec. An Economic History of the USSR, 1917–1991. 3rd ed. London: Penguin Books, 1993. ISBN 0-14-015774-3.
  • Regelson, Lev. Tragedy of Russian Church. 1917–1953. http://www.regels.org/Russian-Church.htm
  • Remington, Thomas. Building Socialism in Bolshevik Russia. Pittsburgh: University of Pittsburgh Press, 1984.
  • Service, Robert. A History of Twentieth-Century Russia. 2nd ed. Cambridge, MA: Harvard University Press, 1999. ISBN 0-674-40348-7.
  • Service, Robert. Stalin: A Biography (2004), along with Tucker the standard biography
  • Tucker, Robert C. Stalin as Revolutionary, 1879-1929 (1973); Stalin in Power: The Revolution from Above, 1929-1941. (1990) online edition with Service, a standard biography; online at ACLS e-books Archived 7 Julai 2000 at the Wayback Machine.

Baada ya Ukomunisti

hariri
  • Asmus, Ronald. A Little War that Shook the World : Georgia, Russia, and the Future of the West. NYU (2010). ISBN 978-0-230-61773-5
  • Cohen, Stephen. Failed Crusade: America and the Tragedy of Post-Communist Russia. New York: W.W. Norton, 2000, 320 pages. ISBN 0-393-32226-2
  • Gregory, Paul R. and Robert C. Stuart, Russian and Soviet Economic Performance and Structure, Addison-Wesley, Seventh Edition, 2001.
  • Medvedev, Roy. Post-Soviet Russia A Journey Through the Yeltsin Era, Columbia University Press, 2002, 394 pages. ISBN 0-231-10607-6
  • Moss, Walter G. A History of Russia. Vol. 2: Since 1855. 2d ed. Anthem Press, 2005. Chapter 22.
  • Stent, Angela. The Limits of Partnership: U.S.-Russian Relations in the Twenty-First Century (2014)

Ramani, jiografia

hariri
  • Blinnikov, Mikhail S. A geography of Russia and its neighbors (Guilford Press, 2011)
  • Catchpole, Brian. A map history of Russia (1983)
  • Chew, Allen F. An Atlas of Russian History: Eleven Centuries of Changing Borders (2nd ed. 1967)
  • Gilbert, Martin. Routledge Atlas of Russian History (4th ed. 2007) excerpt and text search
  • Henry, Laura A. Red to green: environmental activism in post-Soviet Russia (2010)
  • Kaiser, Robert J. The Geography of Nationalism in Russia and the USSR (1994).
  • Medvedev, Andrei. Economic Geography of the Russian Federation by (2000)
  • Parker, William Henry. An historical geography of Russia (University of London Press, 1968)
  • Shaw, Denis J.B. Russia in the modern world: A new geography (Blackwell, 1998)

Historiografia

hariri
  • Confino, Michael. "The New Russian Historiography and the Old—Some Considerations," History & Memory Vol. 21#2 Fall/Winter 2009 doi:10.1353/ham.0.0027 in Project MUSE
  • Cox, Terry. "The New History of the Russian Peasantry," Journal of Agrarian Change 2, no. 4 (October 2002): 570–86.
  • David-Fox, Michael et al. eds. After the Fall: Essays in Russian and Soviet Historiography (Bloomington: Slavica Publishers, 2004)
  • Martin, Russell E (2010). "The Petrine Divide and the Periodization of Early Modern Russian History". Slavic Review. 69 (2): 410–425. JSTOR 25677105.
  • Orlovsky, Daniel (1990). "The New Soviet History". Journal of Modern History. 62 (4): 831–50. doi:10.1086/600602. JSTOR 1881065.
  • Sanders, Thomas, ed. Historiography of Imperial Russia: The Profession and Writing of History in a Multinational State (1999).
  • Winkler, Martina (2011). "Rulers and Ruled, 1700-1917". Kritika: Explorations in Russian and Eurasian History. 13 (4): 789–806.

Vyanzo

hariri
  • Kaiser, Daniel H. and Gary Marker, eds. Reinterpreting Russian History: Readings 860-1860s (1994) 464pp excerpt and text search; primary documents and excerpts from historians
  • Vernadsky, George, et al. eds. Source Book for Russian History from Early Times to 1917 (3 vol 1972)
  • Seventeen Moments in Soviet History (An on-line archive of primary source materials on Soviet history.)

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: