Inkadinasio
Inkadinasio (kwa Kiingereza "incardination", kutoka Kilatini incardinatio) ni msamiati wa sheria za Kanisa unaoeleza sharti la kwamba kila mkleri awe daima chini ya askofu au padri fulani, na kwa njia yake awe ndani ya jimbo au shirika fulani[1].
Kinyume chake kwa Kiingereza ni excardination, ambapo mkleri anaruhusiwa kuacha incardinasio yake ili kupata nyingine.
Maneno yote mawili yanategemea neno cardo ("bawaba"), ambalo pia ni shina la neno kardinali.
Sheria husika zinapatikana katika kanuni 265-272 za Mkusanyo wa Sheria za Kanisa (kwa Kanisa la Kilatini). Nyingine zinazofanana nazo zinapatikana katika kanuni 357-366 za Mkusanyo wa Kanuni za Makanisa ya Mashariki (kwa Makanisa Katoliki ya Mashariki).
Tanbihi
haririViungo vya nje
hariri- Code of Canon Law Canons 265-272
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Inkadinasio kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |