Liturujia ya Canterbury

Liturujia ya Canterbury ni madhehebu yanayoendeleza mambo bora ya Anglikana ndani ya Kanisa la Kilatini.

Msalaba wa Canterbury.
Hii ni sehemu ya mfululizo kuhusu
Kanisa Katoliki
Imani

Umoja wa Mungu
Utatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu)
Umwilisho Maisha ya Yesu
Msalaba Ufufuko Kupaa
Historia ya Wokovu Ufunuo
Biblia Mapokeo Ualimu Dogma
Neema Dhambi Wokovu Sakramenti
Watakatifu Bikira Maria

Muundo

Papa: Fransisko
Urika wa maaskofu Mitaguso mikuu
Kundi la Makardinali
Kanisa la Kilatini
Makanisa Katoliki ya Mashariki

Historia

Historia Ukristo
Ukatoliki Mlolongo wa Kitume
Sifa nne za Kanisa Utetezi Ekumeni
Maisha ya kiroho Amri Kumi Utawa
Sala Falsafa Teolojia
Muziki Sanaa Sayansi

Ibada

Liturujia Mwaka wa Kanisa
Ekaristi Liturujia ya Vipindi

Mapokeo ya liturujia

Liturujia ya Kilatini (Roma Liturujia ya Trento Milano Toledo Braga Lyon Canterbury)
Liturujia ya Armenia Liturujia ya Misri
Liturujia ya Ugiriki Liturujia ya Antiokia
Liturujia ya Mesopotamia

Mwaka 2011 na 2012 Papa Benedikto XVI alianzisha majimbo matatu kwa Waanglikana walioamua kujiunga na Kanisa Katoliki kama makundi.

La kwanza lilianzishwa kwa wale wa Uingereza na Wales (lakini pia Uskoti), la pili kwa wale wa Marekani (baadaye liliongezewa wale wa Kanada)[1][2], la tatu kwa wale wa Australia (halafu pia Japani). Jumla ya waamini ni 10,000 hivi, chini ya mapadri 190, wengi wao wakiwa na ndoa.

Kila mojawapo linaongozwa na padri mwenye ndoa aliyewahi kuwa askofu wa Kianglikana, isipokuwa lile la Marekani ambalo limepewa askofu wa kwanza ambaye ni mseja.

Kabla ya hapo kulikuwa na parokia tu za namna hiyo huko Marekani na Kanada, zikifuata hati maalumu ya Papa Yohane Paulo II ya tarehe 20 Juni 1980,[3][4][5]

Tarehe 9 Desemba 2009, Benedikto XVI alitoa hati Anglicanorum Coetibus, iliyoweka taratibu za uanzishaji wa majimbo yasiyopakana na majimbo ya kawaida ya Kilatini kwa Wakristo wa namna hiyo[6], na kufikia mwisho wa mwaka 2015 parokia zote zilizoanzishwa kabla ya hapo isipokuwa 2 zimejiunga na jimbo la Kimarekani. Mkutano maalumu kwa ajili hiyo ulifanyika tarehe 8-10 Novemba 2012[7].

Kwa niaba ya Papa, Idara ya Ibada ya Kimungu ilipitisha the Book of Divine Worship kwanza kwa muda mwaka 1984, halafu moja kwa moja mwaka 1987.[4] Kuanzia tarehe 29 Novemba 2015 nafasi yake imeshikwa na "Divine Worship: The Missal".

Ibada nyingine kwa ajili ya ndoa na mazishi zilipitishwa na idara hiyo tarehe 22 Juni 2012[8].

Tanbihi

hariri
  1. Cardinal Levada, William (1 Januari 2012). "Decree of Erection of the Personal Ordinariate of the Chair of Saint Peter" (PDF). Holy See. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2013-09-05. Iliwekwa mnamo 2012-10-21. {{cite journal}}: Cite journal requires |journal= (help); Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  2. Bauman, Michelle (3 Januari 2012 (1 Januari 2012 print edition)). "New U.S. Anglican Ordinariate Has an Ordinary". National Catholic Register. EWTN News, Inc. Iliwekwa mnamo 2012-01-06. {{cite web}}: Check date values in: |date= (help)
  3. William H. Stetson, "History of the Pastoral Provision"
  4. 4.0 4.1 Jack D. Barker, "A History of the Pastoral Provision for Roman Catholics in the USA", chapter 1 of Stephen E. Cavanaugh, Anglicans and the Roman Catholic Church (Ignatius Press 2011 ISBN 9781586174996)
  5. Office of the Ecclesiastical Delegate for the Pastoral Provision
  6. "Jerry Fiteau, "New ordinariate and 1980 pastoral provision: An analysis"". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-02-10. Iliwekwa mnamo 2012-10-21.
  7. "2012 Anglican Use Conference". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2012-10-21.
  8. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2005-07-09. Iliwekwa mnamo 2012-10-21.

Viungo vya nje

hariri
 
Kanisa kuu la Our Lady of Walsingham huko Houston, Texas, kwa Wakatoliki wa Marekani na Kanada wanaotumia liturujia hii.

Liturujia

hariri
  Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Liturujia ya Canterbury kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.