Jiji la New York
Jiji la New York (Kiing.: "New York City") ni jiji kubwa kabisa Marekani na kati ya miji mikubwa duniani. Iko kwenye pwani la kaskazini-mashariki ya Marekani katika jimbo la New York.
Jiji la New York | |
Majengo mengi marefu ya Jiji la New York | |
Mahali pa Jiji la New York katika Marekani |
|
Majiranukta: 40°42′15″N 73°55′5″W / 40.70417°N 73.91806°W | |
Nchi | Marekani |
---|---|
Jimbo | New York |
Wilaya | New York Kings Queens Bronx Richmond |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 8,336,697 |
Tovuti: www.nyc.gov |
Jiografia
haririMji uko kwenye mdomo wa pamoja ya mito Hudson na East River inapoishia katika Atlantiki kwa 40°42N 74°00W.
Kitovu cha mji kipo kwenye kisiwa cha Manhattan kilichopo kati ya Hudson na East River. Eneo la jiji ni funguvisiwa kwenye mdomo huo na visiwa vyake pamoja na Manhattan ni Staten Island, Long Island na visiwa vingine vidogo kwa mfano kisiwa cha Ellis na kisiwa cha Sanamu ya Uhuru (Kiingereza: "Statue of Liberty").
Jiji limepanuka kutoka kando za mito hadi barani. Eneo lote la jii ni kilomita za mraba 831.4.
Ndani ya jiji kuna mitaa au wilaya tano zinazoitwa boroughs ambazo ni:
- Manhattan (New York County)
- Brooklyn (Kings County)
- The Bronx (Bronx County)
- Queens (Queens County)
- Staten Island (Richmond County)
Historia
haririJina la Manhattan lakumbuka wakazi asilia waliokuwa Maindio wa Lenape na "manhattan" ni neno la lugha yao "Manna-hata" lililomaaanish a "kisiwa cha milima mingi". Mzugu wa kwanza aliyefika alikuwa nahodha Mwitalia Giovanni da Verrazano mwaka 1524 halafu Mwingereza Henry Hudson mwaka 1609.
Mji mwenyewe ulianzishwa na Waholanzi kwa jina la "Nieuw Amsterdam" (Amsterdam Mpya). Mwaka 1626 kisiwa cha Manhattan kilinunuliwa kwa 60 gulder kutoka wenyeji kikawa mji mkuu wa koloni ya Nieuw Nederland (Uholanzi Mpya).
Mwaka 1664 baada ya vita kati ya Uholanzi na Uingereza koloni yote ilihamishwa upande wa Uingereza pamoja na mji mwenyewe ikapewa jina jipya la "New York".
Katika karne ya 18 New York ilikuwa sehemu ya uasi dhidi ya Uingereza
Kipindi kikubwa cha mji kulitokea katika karne ya 19 wakati wahamiaji wengi sana walipofika MArekani. Idadi kubwa walifika kwenye bandari la New York.
Baada ya fitina kati ya watu wa kusini na wenyeji wa kaskazini serikali ya Kiingereza ilifunga kambi hilo.
Hali ya hewa
hariri
Viwango vya juu na chini vya joto katika miji ya New York[1] (Fahrenheit) Jiji Jan Feb Mar Apr Mei Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec Albany juu
chini31
1334
1644
2557
3670
4678
5582
6080
5871
5060
3948
3136
20Binghamton juu
chini28
1531
1741
2553
3566
4673
5478
5976
5768
5057
4044
3133
21Buffalo juu
chini31
1833
1942
2654
3666
4875
5780
6278
6070
5359
4347
3436
24Long Island juu
chini39
2340
2448
3158
4069
4977
6083
6682
6475
5764
4554
3644
28New York City juu
chini38
2641
2850
3561
4471
5479
6384
6982
6875
6064
5053
4143
32Rochester juu
chini31
1733
1743
2555
3568
4677
5581
6079
5971
5160
4147
3336
23Syracuse juu
chini31
1434
1643
2456
3568
4677
5582
6080
5971
5160
4047
3236
21Marejeo
hariri
- ↑ "Typical High and Low Temperatures For Various New York Cities". US Travel Weather. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-03-13. Iliwekwa mnamo 24 Machi 2010.