Jimbo Kuu la Bujumbura
Jimbo Kuu la Bujumbura (kwa Kilatini Archidioecesis Buiumburaensis) ni mojawapo kati ya majimbo 8 ya Kanisa Katoliki nchini Burundi na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Kikanisa lina majimbo ya Bubanza na Bururi chini yake.
Askofu mkuu wake ni Evariste Ngoyagoye.
Historia
hariri- 11 Juni 1959: Kuanzishwa kwa Apostolic Vicariate ya Usumbura.
- 10 Novemba 1959: Kufanywa dayosisi (kwa jina la Usumbura hadi 9 Oktoba 1964)
- 25 Novemba 2006: Kupandishwa cheo na kuwa jimbo kuu.
Uongozi
hariri- Maaskofu wakuu wa Bujumbura
- Evariste Ngoyagoye (2006 - )
- Maaskofu wa Usumbura halafu Bujumbura
- Evariste Ngoyagoye (1997 – 2006)
- Simon Ntamwana (1988 – 1997)
- Michel Ntuyahaga (1959 – 1988)
- Vicar Apostolic wa Usumbura
- Michel Ntuyahaga (1959)
Takwimu
haririEneo ni la kilometa mraba 2,200, ambapo kati ya wakazi 1,968,000 (2012) Wakatoliki ni 1,542,000 (78.4%) katika parokia 29.