Open main menu
Moshi mweusi kutoka Kikanisa cha Sisto IV ni ishara ya kwamba Papa mpya hajachaguliwa.[1]
Moshi mweupe ni ishara ya kwamba Papa mpya amechaguliwa.[1]

Konklevu (kutoka Kilatini "cum clave", yaani "kwa ufunguo", kupitia Kiingereza "conclave") ni mkutano maalumu ya makardinali wote wenye umri chini ya miaka 80 unaofanyika ili kumchagua askofu wa Roma, maarufu kama Papa wa Kanisa Katoliki.

Lengo la kujifungia ndani tangu karne za kati ni kuzuia makardinali wasiingiliwe na watu wa nje, hasa watawala, ambao wanaweza kuwa na malengo tofauti na yale ya kiroho.

Kwa sasa kuna taratibu nyingi zilizopangwa kinaganaga, ambazo mojawapo ni kwamba wapigakura wasizidi 120.

TanbihiEdit

  1. 1.0 1.1 Chumley, Cheryl K.. "What Do American Catholics Want in the Next Pope?", 12 March 2013. Retrieved on 15 March 2013. 

MarejeoEdit

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Konklevu kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.