Uislamu nchini Gabon

Uislamu kwa nchi

Uislamu nchini Gabon unategemea hasa wahamiaji kutoka nchi nyingineː unakadiriwa kuwa asilimia 12 ya idadi ya wakazi wote wa Gabon ni waumini wa Kiislamu, ambao kati yao asilimia 80 hadi 90 ni wageni.

Uislamu, Kanisa Katoliki, na madhehebu ya Uprotestanti yanaendesha shule za msingi na sekondari nchini Gabon. Shule hizi zinahitaji kujisajili kwa Wizara ya Elimu, ambapo hutozwa ili zifikie viwango vinavyohitajika kutoa huduma kama shule za umma. Serikali haichangii wala kutoa ruzuku kwa shule za binafsi, haijalishi ni ya kilimwengu au ya kidini.

Msikiti mjini Port-Gentil, Gabon

Tanbihi

hariri