Uislamu barani Amerika

Uislamu kwa nchi

Uislamu ni dini ndogo katika nchi na maeneo yote ya Bara la Amerika.

Suriname ina asilimia kubwa ya Waislamu katika ukanda huu, ikiwa na asilimia 13 au watu 66,307, kwa mujibu wa sensa yake ya mwaka wa 2004. Hata hivyo, Marekani, inakadiriwa kuwa na idadi kubwa licha ya kukosa sensa ya dini kwa Uislamu, ina aminika kuwa ina idadi kubwa ya Waislamu, kati ya milioni 1.3 na 2.7.

Baadhi ya Waafrika Magharibi walichukuliwa na Wamarekani enzi za koloni na inaonekana walio wengi walikuwa Waislamu, ingawa walilazimishwa kubadili dini kinguvu na kuwa Wakristo. Waislamu wengi wa Karibi ya Kiingereza ya zamani walitokea Bara Hindi wakiwa kama wafanyakazi hasa kwa kufuatia kupigwa marufuku kwa utumwa. Kundi hili pia lilifika huko Suriname, ingawa Waislamu wengine walihami huko katika koloni la Kiholanzi, ambalo leo hii ni Indonesia.

Kigezo:Islam in the Americas