Uislamu nchini Guinea
Uislamu kwa nchi |
Uislamu nchini Guinea ni dini yenye wafuasi wengi nchini humo, kukiwa na makadirio ya asilimia 85 ya wakazi wote wa Guinea kuwa ni Waislamu, hasa kwa mujibu wa takwimu yao ya mwaka wa 2005.
Wengi wao ni wafuasi wa dhehebu la Sunni wanaofuata mafunzo ya Maliki na mila zake pamoja na Qadiria na Tijani katika miongozo ya Sufi. Vilevile kuna nyendo za Ahmadiyya nchini humo.[1]
Ijapokuwa Wafaransa walianzisha koloni lao mnamo mwaka wa 1891, udhibiti wao dhidi ya kanda ulikuwa dhaifu mno.
Baada ya uhuru mnamo mwaka 1958, kiongozi Muislamu mwenye kufuata sera za Umarksi, Rais Sékou Touré hakupenda suala la kuendeleza Uislamu; hadi hapo uongozi na sifa ilivyoanza kwenda kombo kwenye miaka ya 1970 Touré ndipo akaomba taasisi za Kiislamu zirudishe uhusiano wake na serikali ili kuhalalisha utawala wake.
Tangu kifo cha Touré mnamo 1984, ushirikiano baina ya jumuia za Kiislamu na serikali uliendelea.[2]
Marejeo
hariri- ↑ J. Gordon Melton, Martin Baumann. Religions of the World: A Comprehensive Encyclopedia of Beliefs. uk. 1280. ISBN 978-1-59884-203-6. Iliwekwa mnamo Juni 4, 2014.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ John Esposito, The Oxford Dictionary of Islam, Oxford University Press 2003
Makala kuhusu Uislamu kwa nchi bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |