Uislamu nchini Angola

Uislamu kwa nchi

Uislamu nchini Angola ni dini yenye waumini wachache sana. Vyanzo vingi vinakadiria kuna idadi ya watu 90,000, ingawaje wengine wanatoa kiwango kikubwa zaidi ya hapo.

Waislamu walio wengi nchini humo ni wahamiaji kutoka nchi za Afrika ya Magharibi na Mashariki ya Kati, ingawa baadhi ya wenyeji wamebadili dini na kuwa Waislamu.

Kuna taasisi kadhaa ambazo zinaendesha misikiti, mashule na vituo vinavyohusisha jumuia za Kiislamu. Waislamu wa Angola wanawakilishwa na Baraza Kuu la Waislamu Angola la mjini Luanda.[1]

Hadi mwishoni mwa mwaka 2013, serikali ya Angola haitambui uwepo halali wa jumuia na taasisi za Kiislamu nchini humo, na hivyo kupelekea misikiti kukabiliana na vikwazo mbalimbali, tena mingi ilifungwa na serikali hiyo. [2]

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. Oyebade, Adebayo O. Culture And Customs of Angola, 2006. Pages 45–46.
  2. http://www.theguardian.com/world/2013/nov/28/angola-accused-banning-islam-mosques