Biashara ya utumwa kupitia Bahari ya Hindi
Biashara ya utumwa kupitia Bahari ya Hindi ni sehemu ya biashara hiyo haramu iliyoendeshwa hasa na Waarabu tangu zamani za uenezi wa Uislamu hadi karne ya 20 kwa kutumia watu kutoka sehemu za ndani za Afrika.
Wanahistoria wa Ulaya na Amerika wamekadiria kwamba kati ya mwaka 650 na miaka ya 1960, milioni 10 hadi 18 walifanywa watumwa na Waarabu huko Ulaya, Asia na hasa Afrika kupitia Bahari ya Shamu, Bahari ya Hindi na jangwa la Sahara.[1][2]
Historia ya biashara hiyo
haririBiashara ya kupitia bahari ya Hindi ina historia ndefu, kuanzia Waarabu na Waswahili kuteka njia za baharini na pwani ya Afrika Mashariki katika karne ya 9 (tazama Usultani wa Zanzibar). Wafanyabiashara hao waliteka Wabantu (Zanj) kutoka maeneo ya ndani ya Kenya, Msumbiji na Tanzania ya leo na kuwaswaga hadi pwani,[3] Unguja na Pemba.[4]
Watumwa waliuzwa kotekote katika Mashariki ya Kati. Biashara hiyo ilistawi kadiri meli zilivyozidi kuboreshwa na hitahi la watu mashambani lilivyoongezeka. Hatimaye, kila mwaka walitekwa na kuuzwa watu makumi elfu.[4][5][6]
Biashara ya utumwa kupitia Bahari ya Hindi ilibadilikabadilika na kuelekea maeneo mapya: Misri, Rasi ya Arabia, Ghuba ya Uajemi, India, Asia Mashariki, visiwa vya Bahari ya Hindi, Ethiopia na Somalia.[7][8]
Afrika Mashariki watumwa walitokana na Wabantu walioitwa Zanj. Kwa karne kadhaa hao walisafirishwa na Waarabu hadi nchi zote kando ya Bahari ya Hindi.
Mahalifa wa Umayyad na Abbasid walitumia watumwa wengi kama askari, na kuanzia mwaka 696, watumwa wa Kizanj walijaribu kuasi mabwana wao Warabu huko Iraq (tazama Uasi wa Zanj).
Maandishi ya kale ya Kichina yanataja mabalozi kutoka Java (leo nchini Indonesia) wakimtolea Kaisari wa China watumwa wawili Seng Chi (Zanj) kama zawadi, na Seng Chi wengine wakisafirishwa hadi China kutoka ufalme wa Kihindu wa Srivijaya huko Java.
Uasi wa Zanj, uliofuatwa na mfululizo wa matukio ya namna hiyo series kati ya miaka 869 na 883 karibu na Basra (Iraq), unasadikiwa kuhusisha watumwa kutoka [[Maziwa makuu ya Afrika na hata kusini zaidi.[9] Uasi ulifikia kuhusisha watu zaidi ya 500,000 na kusababisha vifo makumi elfu kusini mwa Iraq.[10]
Waafrika hao walisafirishwa hadi Mashariki ya Kati na kulazimishwa kufanya kazi ngumu sana mashambani[11] kadiri uchumi wa kilimo (hasa wa miwa) ulivyostawi na kutajirisha Waarabu, kwa kuwa hao waliona mkulima ni mtu duni, lakini walihitaji watu wa kufanya kazi hiyo.
Ni hakika kwamba idadi kubwa ya watumwa ilihamishwa kutoka Afrika Mashariki; uthibitisho wa wazi zaidi ni ukubwa wa uasi wa Zanj huko Iraq katika karne ya 9, ingawa si watumwa wote waliohusika walikuwa Zanj. Hakuna hakika sana kutoka sehemu gani ya Afrika mashariki hao Zanj walitokea, kwa sababu ni wazi kuwa hapa jina hilo limetumika kwa maana pana, si kwa kutaja pwani maalumu kati ya 3°N. to 5°S., ambayo kwa kawaida inatajwa kuhusu watu hao.[12]
Zanj walihitajika pia katika maeneo yaliyopatwa na mafuriko kwenye delta ya Tigri-Eufrate, na katika migodi ya chumvi ya Mesopotamia, hasa karibu na Basra.[13][14]
Tanbihi
hariri- ↑ "Focus on the slave trade", BBC
- ↑ "The Unknown Slavery: In the Muslim world, that is — and it's not over" Archived 26 Novemba 2009 at the Wayback Machine., National Review
- ↑ Ochiengʼ, William Robert (1975). Eastern Kenya and Its Invaders. East African Literature Bureau. uk. 76. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2015.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 4.0 4.1 Lodhi, Abdulaziz (2000). Oriental influences in Swahili: a study in language and culture contacts. Acta Universitatis Gothoburgensis. uk. 17. ISBN 9173463779.
- ↑ A History of Africa (tol. la 4). Budapest: Routledge. Desemba 2001. uk. 258. ISBN 978-0415252485.
{{cite book}}
:|access-date=
requires|url=
(help); Cite uses deprecated parameter|authors=
(help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Edward R. Tannenbaum, Guilford Dudley (1973). A History of World Civilizations. Wiley. uk. 615. ISBN 0471844802.
- ↑ Refugee Reports, November 2002, Volume 23, Number 8
- ↑ Gwyn Campbell, The Structure of Slavery in Indian Ocean Africa and Asia, 1 edition, (Routledge: 2003), p.ix
- ↑ Rodriguez, Junius P. (2007). Encyclopedia of Slave Resistance and Rebellion, Volume 2. Greenwood Publishing Group. uk. 585. ISBN 0313332738.
- ↑ ""Revisiting the Zanj and Re-Visioning Revolt: Complexities of the Zanj Conflict - 868-883 Ad - slave revolt in Iraq"". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-06. Iliwekwa mnamo 2016-02-07.
- ↑ "Islam, From Arab To Islamic Empire: The Early Abbasid Era". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-09-24. Iliwekwa mnamo 2016-02-07.
- ↑ "The Zanj Rebellion Reconsidered".
- ↑ ""the Zanj: Towards a History of the Zanj Slaves' Rebellion"". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-10-27. Iliwekwa mnamo 2009-10-27.
- ↑ "Hidden Iraq". "William Cobb". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-02-17. Iliwekwa mnamo 2016-02-07.
Marejeo
hariri- Edward A. Alpers, The East African Slave Trade (Berkeley 1967)
- Ibn Khaldun, The Muqaddimah, trans. F. Rosenthal, ed. N. J. Dawood (Princeton 1967)
- Murray Gordon, Slavery in the Arab World (New York 1989)
- Habeeb Akande, Illuminating the Darkness: Blacks and North Africans in Islam (Ta Ha 2012)
- Bernard Lewis, Race and Slavery in the Middle East (OUP 1990)
- Patrick Manning, Slavery and African Life: Occidental, Oriental, and African Slave Trades (Cambridge 1990)
- Paul E. Lovejoy, Transformations in Slavery: A History of Slavery in Africa (Cambridge 2000)
- Allan G. B. Fisher, Slavery and Muslim Society in Africa, ed. C. Hurst (London 1970, 2nd edition 2001)
- The African Diaspora in the Mediterranean Lands of Islam (Princeton Series on the Middle East) Eve Troutt Powell (Editor), John O. Hunwick (Editor) (Princeton 2001)
- Ronald Segal, Islam's Black Slaves (Atlantic Books, London 2002)
- Robert C. Davis, Christian Slaves, Muslim Masters: White Slavery in the Mediterranean, the Barbary Coast, and Italy, 1500-1800 (Palgrave Macmillan, London 2003) ISBN 978-1-4039-4551-8
- Doudou Diène (2001). From Chains to Bonds: The Slave Trade Revisited. Berghahn Books. ISBN 1571812652. Iliwekwa mnamo 26 Mei 2015.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
hariri- Robert Davis. "British Slaves on the Barbary Coast". BBC. Iliwekwa mnamo 29 Aprili 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - "Slavery in Islam". BBC. Iliwekwa mnamo 29 Aprili 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - "Encyclopædia Britannica's Guide to Black History". www.britannica.com. Encyclopædia Britannica. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-10-06. Iliwekwa mnamo 29 Aprili 2015.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - iAbolish.ORG! American Anti-Slavery Group (AASG) - particular focus on North African slaves
Tazama pia
hariri- Wahindi Weusi
- Biashara ya ng'ambo ya Sahara
- Biashara ya utumwa kupitia Atlantiki
- Biashara ya masafa marefu ya Afrika Mashariki
- Biashara ya utumwa
- Ukomeshaji wa Biashara ya Watumwa
- Yosefina Bakhita
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Biashara ya utumwa kupitia Bahari ya Hindi kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |