Biashara ya masafa marefu ya Afrika Mashariki
Biashara ya masafa marefu ya Afrika Mashariki ni jina la kutaja aina ya biashara iliyokuwa ikifanyika kutoka katika pwani hadi ndanindani ya Afrika Mashariki. Awali ilianza katika maeneo ya pwani ya Afrika Mashariki na kisha kuenea katika vijieneo vya ndani kabisa vya Afrika Mashariki.
Historia
haririKipindi
haririBiashara hii inasemekana ilianzia karne ya 18 na 19, ikachukua zaidi ya miaka 30-50 hadi ilipokuja kuingiliwa na wakoloni mwishoni kabisa mwa karne ya 19.
Washiriki
haririWafanyabiashara wakuu waliohusishwa na biashara hiyo walikuwa Waarabu na Waswahili kutoka Pwani na Wayao kutoka kusini mwa Tanganyika, Wakamba kutoka kusini mwa Kenya na vilevile Wanyamwezi kutoka Tabora. Makabila mengi yalishiriki katika biashara hiyo, lakini vingunge wenyewe ni Wayao, Wakamba na Wanyamwezi.
Muundo wa biashara
haririBiashara ilikuwa katika muundo wa misafara mitatu ambayo ilianzia pwani ikaenda hadi ndanindani kabisa mwa ukanda wa Afrika Mashariki. Misafara hiyo ilikuwa kama ifuatavyo:
Msafara wa Kaskazini
haririSafari ilianzia Mombasa na baadhi ya maeneo ya Pangani hadi maeneo ya Kilimanjaro kuelekea pembezoni mwa ziwa Victoria, kupitia Wakikuyu, Wataita, Wamaasai, na Wanyika. Msafara huo ulikuwa unaongozwa na Wakamba kutoka Kenya.
Msafara wa Kati
haririMsafara huu ulianzia Bagamoyo kupitia maeneo ya kati ya Tanganyika - Tabora (Unyanyembe). Kuanzia huko msafara ulienda hadi Ujiji, halafu Buganda kupitia Buhaya, magharibi mwa fukwe ya Ziwa Victoria. Msafara ulikuwa chini ya Wanyamwezi ambao katika karne ya 19 walikuwa chini ya Mtemi Mirambo na Mtemi Nyungu ya Mawe na Mtemi Fundikira mnamo 1839. Msafara huu ulikuwa una shughuli nyingi na muhimu sana kupita misafara yote mitatu.
Msafara kusini
haririMsafara huu ulianzia katika bandari ya Mikindani na Kilwa kuelekea kanda ya Ziwa Tanganyika kupitia kusini mwa Ziwa Nyasa. Msafara ulifika Monomutapa kwa ajili ya dhahabu. Ulikuwa chini ya Wayao ambao walikuwa chini ya Mataka I kwenye karne ya 19. Wayao walifanya biashara kaskazini mwa Kilwa na Zambezi ya chini kuelekea Kusini. Baadaye walipata silaha wakawa viongozi mara moja katika maeneo ya Ziwa Nyasa na pwani. Wayao walishikiri msafara wa Kusini ambao uliishia Afrika ya Kati wakati Wakamba walikuwa Kaskazini na Wanyamwezi walishikiria msafara wa Kati ulioanzia Bagamoyo hadi Ujiji.
Bidhaa zilizokuwa zinapatikana katika biashara
haririWafanyabiashara wa Waswahili na Waarabu kutoka pwani waliuza bunduki, shanga, unga wa bunduki, nguo na bidhaa nyingine za kiwandani. Watu kutoka ndanindani kabisa mwa Afrika Mashariki walitoa bidhaa kama vile pembe za ndovu, nta ya nyuki, dhahabu, ngozi za wanyama na vitu vingine vya thamani.
Sababu za kuibuka kwa Biashara ya Masafa Marefu ya Afrika Mashariki
haririKuibuka na kuendelea kwa biashara ya masafa marefu ya Afrika Mashariki kulichangiwa na mambo kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na:
(A) Upatikanaji wa bidhaa za kutosha katika Afrika Mashariki
haririHili lilitokana na kuongezeka kwa uzalishaji hasa katika sekta ya kilimo.
(B) Kuibuka kwa wafanyabiashara wakubwa
haririKuibuka kwa jamii kubwa ya wafanyabiashara katika Afrika Mashariki kama vile Wanyamwezi, Wayao na Wakamba nako kulichangia kukua kwa biashara.
(C) Uwepo wa miji mikubwa ya pwani
haririUwepo wa miji mikubwa ya pwani kama vile Bagamoyo, Mikindani na Pangani kuliongezea ukuaji wa biashara kwa kufuatia wa kwamba miji hiyo ilikuwa kianzio cha safari za masafa marefu wakati wa uendeshaji wa biashara.
Matokeo/madhara ya biashara ya masafa marefu ya Afrika Mashariki
haririBiashara ya masafa marefu ilikuwa na matokeo kadha wa kadha katika maeneo ya pwani hadi ndanindani kabisa mwa Afrika Mashariki. Matokeo hayo ni pamoja na:
(A) Ukuaji wa miji
haririBiashara ilipelekea kukua kwa miji na vijiji hasa ndanindani huko mwa Afrika Mashariki kwa mfano Ujiji, Mpwapwa, Tabora na kwingineko.
(B) Ukuaji wa dola za kitemi
haririBiashara hii ilichangia kiasi kikubwa kukua kwa dola mbalimbali za kitemi kama vile Wanyamwezi, Ukimbu, na Wahehe katika maeneo ya Tanganyika. Vilevile dola la Buganda lilikuja kukua mno katika karne ya 19 kwa kufuatia biashara hii.
(C) Utambulisho wa tamaduni mpya
haririTamaduni mpya, kwa mfano dini ya Kiislamu na mtindo wa uvaaji wa kanzu na baraghashia ulienea ndani kabisa ya Afrika Mashariki.
(D) Maendeleo/ukuaji wa lugha ya Kiswahili
haririLugha ya Kiswahili ilienea kwa kiasi kikubwa sana kutoka katika pwani ya Afrika Mashariki hadi maeneo ya ndani kwa sababu wafanyabiashara walikuwa wanatumia Kiswahili kama chombo cha mawasiliano wakati wa kubadilishana bidhaa.
(E) Ukuaji wa biashara ya utumwa
haririBiashara ya masafa marefu ilienda sambamba na ukuaji wa biashara ya utumwa - hasa katika maeneo ya ndani ya Afrika Mashariki.
(F) Kuibuka kwa wafanyabiashara na viongozi wakubwa
haririKuna baadhi ya watu walioibuka kama wafanyabiashara na viongozi wakubwa nje ya biashara kwa kufuatia utajiri uliokithiri kutoka katika biashara. Hili lilijumlisha Mirambo, Machemba, [Nyungu ya Mawe]] na Mkwawa.
(G) Ndoa za mseto
haririWatu kutoka maeneo ya pwani walioana au kuzaliana na watu kutoka ndani kabisa mwa Afrika Mashariki.