Idi Amin
Idi Amin Dada (/ˈiːdi ɑːˈmiːn/; 1923–1928 – 16 Agosti 2003) alikuwa mwanasiasa na afisa wa jeshi ambaye alipata kuwa Rais wa Uganda kuanzia mwaka 1971 hadi 1979. Alitawala kidikteta ilhali uchumi wa nchi uliporomoka na makosa mengi ya jinai dhidi ya haki za kibinadamu yalitendwa.
Idi Amin | |
Idi Amin, 1975 | |
3 Rais wa Uganda
| |
Muda wa Utawala 25 Januari 1971 – 11 Aprili 1979 | |
Makamu wa Rais | Mustafa Adrisi |
---|---|
mtangulizi | Milton Obote |
aliyemfuata | Yusuf Lule |
tarehe ya kuzaliwa | [1] Nakasero, Kampala, Uganda | 30 Mei 1928
tarehe ya kufa | 16 Agosti 2003 (umri 75) Jeddah, Saudi Arabia |
mahali pa kuzikiwa | Ruwais Makaburi |
ndoa | 6:
|
watoto | 43 (alidai)[2] |
signature | |
Military service | |
Allegiance |
|
Service/branch |
|
Years of service | 1946–1979 |
Rank |
|
Commands | Mkuu wa Jeshi la Uganda |
Battles/wars |
Idadi ya watu waliouawa Uganda chini ya utawala wake imekadiriwa kuwa kati ya 100,000[3] na 500,000.[4]
Katika miaka yake ya kushika serikali Amin alibadilika kutoka uhusiano wa kirafiki na nchi za magharibi, na hasa Israeli, kuhamia upande wa Muammar Gaddafi wa Libya, Mobutu Sese Seko wa Zaire, Umoja wa Kisovyeti na Ujerumani ya Mashariki.[5][6][7] Hata hivyo Amin alipata usaidizi wa ofisi ya upelelezi ya Marekani CIA iliyotuma silaha na vifaa vingine kwa jeshi lake.[8]
Mwaka 1977 Amin alivunja uhusiano wa kidiplomasia na Ufalme wa Maungano (Uingereza) akajitangaza kuwa alishinda na kujiongezea sifa ya CBE ("Conqueror of the British Empire"). Kuanzia wakati ule cheo chake rasmi kilikuwa "His Excellency President for Life, Field Marshal Alhaji Dr. Idi Amin Dada, VC, DSO, MC, CBE".[4]
Jaribio la Amin la kutwaa sehemu za Mkoa wa Kagera wa Tanzania kwenye mwaka 1978 lilisababisha Vita vya Kagera baina ya Tanzania na Uganda na mwisho wa utawala wake. Amin alikimbia kukaa ugenini Libya na baadaye Saudia alipoishi hadi kifo chake mwaka 2003.
Maisha
haririAlikotoka
haririHakuna uhakika juu ya mwaka na mahali alikozaliwa. Amin mwenyewe hakuandika kumbukumbu ya maisha yake wala hakuagiza taarifa rasmi juu ya maisha yake. Vyanzo mbalimbali vinasema ya kwamba alizaliwa mnamo 1925 Koboko au Kampala. [9] Mtafiti Fred Guweddeko amedai Amin alizaliwa 17 Mei 1928,[10] lakini hii imepingwa.[11] Mwanawe Amin Hussein alisema babake alizaliwa Kampala mwaka 1928.[12]
Kufuatana na Fred Guweddeko wa Chuo Kikuu cha Makerere Idi Amin alikuwa mwana wa Andreas Nyabire (1889–1976) wa kabila la Wakakwa, ambaye alikuwa Mkatoliki aliyehamia Uislamu mnamo 1910 akibadilisha jina lake kuwa Amin Dada na kumpa mwana wa kwanza jina hilo pia.
Iddi Amin alilelewa na mama yake bila baba kijijini katika Uganda ya Kaskazini-magharibi. Kufuatana na Gudewekko mamake Amin Assa Aatte (1904–1970) alikuwa Mlugbara aliyetibu watu kwa mitishamba. Amin alisoma miaka kadhaa kwenye shule ya Kiislamu huko Bombo kuanzia mwaka 1941.
Amin mwanajeshi
haririBaada ya miaka michache ya shule na kazi ndogondogo aliajiriwa mwaka 1946 na afisa Mwingereza wa jeshi la kikoloni King's African Rifles (KAR).[10]
Aliingia jeshini huko Jinja akifanya kazi ya msaidizi jikoni akiendelea kupokea mafunzo ya kijeshi.[13] Baadaye Amin alidai ya kwamba alilazimishwa kuhudumia huko Burma katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia.[4][14][15] Mwaka 1947 alihamishiwa Gilgil, Kenya. Mwaka 1949 alitumwa kaskazini kwa kupigania waasi Wasomalia huko. Tangu mwaka 1952 kikosi chake kilihudhuria katika juhudi za kupambana na wanamgambo wa Maumau karibu na Mlima Kenya.
Aliendelea kupanda vyeo vilivyopatikana kwa Waafrika katika jeshi la KAR na muda mfupi baada ya uhuru alipewa cheo cha luteni yaani afisa kamili kama mmoja wa Wauganda wawili. Baada ya uhuru wa Uganda mwaka 1962 alikuwa kapteni halafu mwaka 1963 meja. Mwaka 1964 alikuwa makamu wa mkuu na mwaka 1965 mkuu wa jeshi, mwaka 1970 mkuu wa mikono yote ya kijeshi.[10] In 1970, he was promoted to commander of all the armed forces.[16]
King's African Rifles | |
---|---|
1946 | aliingia King's African Rifles |
1947 | Askari wa kawaida |
1952 | Koplo |
1953 | Sajenti |
1958 | Sajenti mtumishi |
1959 | Effendi (afisa mteule) |
1961 | Luteni (mmoja kati ya Wauganda wawili waliofikia cheo hiki katika KAR) |
Jeshi la Uganda | |
1962 | Kapteni |
1963 | Meja |
1964 | Makamu wa Mkuu wa Jeshi la Uganda |
1965 | Kanali, Mkuuwa Jeshi |
1968 | Meja Jenerali |
1971 | Mkuu wa dola Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi wa Dola Amiri Jeshi Mkuu wa Uganda |
1975 | Field Marshal |
Mkuu wa Jeshi na mapinduzi
haririAmin alipandishwa cheo na waziri mkuu Milton Obote baada ya uasi wa wanajeshi katika Afrika ya Mashariki wa 1964 uliokomeshwa na askari Waingereza katika Tanganyika, Kenya na Uganda akawa makamu wa mkuu wa Jeshi aliyekuwa bado Mwingereza. Kutoka hapa alishirikiana na Obote katika hatua za kuimarisha utawala wa waziri mkuu. Wakati bunge la Uganda lilitaka utafiti kuhusu mashtaka ya Obote kushiriki katika biashara ya siri ya pembe za ndovu kutoka Kongo Obote iliamua kubadilisha katiba na jeshi la Amini lilimfukuza Mkuu wa Dola Kabaka Mutesa kwa nguvu, halafu Obote alijitangaza kuwa rais. Sasa Amin alikuwa kanali na Mkuu wa Jeshi.[17][18]
Amin alianza kuajiri hasa askari kutoka kaskazini ya Uganda mpakani mwa Sudani.[19]
Mwaka 1970 Obote aliendelea kumpa Amin cheo cha mkuu wa mikono yote ya jeshi na ulinzi. Lakini Amin alisikia pia ya kwamba kulikuwa na mashtaka dhidi yake kutokana na matumizi ya makisio ya jeshi na mipango ya Obote kumfanyia utafiti. Hapo Amin alitumia nafasi ya safari ya Obote kwenda nje kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola, akatwaa mamlaka ya serikali tarehe 25 Januari 1971.[20]
Mtawala wa Uganda
haririMwaka 1971 alimpindua rais Milton Obote akajitangaza kuwa rais mpya, lakini wengine hawakumtaka.
Mara moja alianza kuwatesa wafuasi wa Obote na watu wote waliompinga. Kuna makadirio ya kwamba jumla ya watu 100,000 hadi 500,000 waliuawa katika miaka minane ya utawala wake.
Aliharibu uchumi wa Uganda kwa ufisadi na majaribio ya kuongoza biashara. Hatua kubwa ya uharibifu ilikuwa kufukuza watu wote wenye asili ya Kihindi na kugawa maduka na biashara yao kwa ndugu au wafuasi wa rais. Takriban watu 80,000 walipaswa kuondoka kwao wakihamia Uingereza, Marekani au Kanada hasa.
Mnamo Oktoba 1978 Amin alianzisha vita dhidi ya Tanzania kwa kuvamia sehemu za mkoa wa Kagera. Rais Julius Nyerere wa Tanzania aliamua kumwondoa Amin kabisa na jeshi la Tanzania likatwaa Kampala tarehe 11 Aprili 1979.
Amin alitorokea Libya, halafu Irak na mwishowe Saudia alikopewa kimbilio kwa masharti ya kutoshughulikia siasa tena.
Marejeo
hariri- ↑ Leopold, Mark (2021). Idi Amin: The Story of Africa's Icon of Evil. New Haven (Conn.): Yale University Press. ISBN 978-0-300-15439-9.
- ↑ Nakajubi, Gloria. "Ugandan dictator Idi Amin's widow Sarah Kyolaba dies in the UK aged 59", The Independent, 15 July 2015.
- ↑ Ullman, Richard H. (Aprili 1978). "Human Rights and Economic Power: The United States Versus Idi Amin". Foreign Affairs. Iliwekwa mnamo 26 Machi 2009.
The most conservative estimates by informed observers hold that President Idi Amin Dada and the terror squads operating under his loose direction have killed 100,000 Ugandans in the seven years he has held power.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 4.0 4.1 4.2 Keatley, Patrick. "Obituary: Idi Amin", The Guardian, 18 August 2003. Retrieved on 18 March 2008.
- ↑ Roland Anthony Oliver, Anthony Atmore. Africa Since 1800. uk. 272.
- ↑ Dale C. Tatum. Who influenced whom?. uk. 177.
- ↑ Gareth M. Winrow. The Foreign Policy of the GDR in Africa, p. 141.
- ↑ New York Times, Dec. 17, 1986; Paper Cites CIA Aid to Amin's Army in 70s
- ↑ Encyclopædia Britannica, Encarta na Columbia Encyclopedia vinasema alizaliwa Koboko au Kampala takriban 1925 na tarehe kamili haijulikani.
- ↑ 10.0 10.1 10.2 Guweddeko, Fred (12 Juni 2007). "Rejected then taken in by dad; a timeline". The Monitor. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Juni 2007. Iliwekwa mnamo 8 Agosti 2009.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ O'Kadameri, Billie. "Separate fact from fiction in Amin stories", Originally published in The Monitor', 1 September 2003. Retrieved on 8 May 2010.
- ↑ Elliott, Chris. "Idi Amin's son complains about the Guardian’s obituary notice", 30 November 2014. Retrieved on 1 December 2014.
- ↑ "Idi Amin". Encyclopædia Britannica. 19 Desemba 2008. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Machi 2007. Iliwekwa mnamo 8 Agosti 2009.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ General Idi Amin Dada: A Self Portrait. Le Figaro Films.
- ↑ Bay, Austin. "Why Didn't Amin Rot and Die in Jail?", Strategy Page, 20 August 2003. Retrieved on 8 August 2009.
- ↑ "General Idi Amin overthrows Ugandan government". British Council. 2 Februari 1971. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Februari 2007. Iliwekwa mnamo 8 Agosti 2009.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Country Studies: Uganda: Independence: The Early Years". Federal Research Division. United States Library of Congress. Iliwekwa mnamo 8 Agosti 2009.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Idi Amin Dada Biography". Encyclopedia of World Biography. Thomson Gale. 2005. Iliwekwa mnamo 20 Machi 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Nantulya, Paul (2001). "Exclusion, Identity and Armed Conflict: A Historical Survey of the Politics of Confrontation in Uganda with Specific Reference to the Independence Era" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 4 Oktoba 2006.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "General Idi Amin overthrows Ugandan government". British Council. 2 February 1971. Archived from the original on 25 February 2007. Retrieved 8 August 2009.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Idi Amin kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |