Myanmar

(Elekezwa kutoka Burma)


Myanmar (pia: Myama; Myamari) ni nchi ya Asia ya Kusini-Mashariki inayojulikana pia kwa jina la Burma au Bama.


Pyidaunzu Thanmăda Myăma Nainngandaw

Jamhuri ya Muungano wa Myanmar
Bendera ya Myanmar Nembo ya Myanmar
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa:
Wimbo wa taifa: Kaba Ma Kyei
Lokeshen ya Myanmar
Mji mkuu Naypyidaw1
19°45′ N 96°12′ E
Mji mkubwa nchini Yangon
Lugha rasmi Kiburma
Serikali
Win Myint
Aung San Suu Kyi
Uhuru
Tarehe
4 Januari 1948
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
676,578 km² (ya 40)
3.06%
Idadi ya watu
 - [[]] kadirio
 - 2014 sensa
 - Msongamano wa watu
 
(ya 25)
51,486,253
76/km² (ya 125)
Fedha Kyat ya Myanmar (K) (mmK)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
MMT (UTC+6:30)
{{{time_zone_DST}}} (UTC{{{utc_offset_DST}}})
Intaneti TLD .mm
Kodi ya simu +95

-

1Serikali kadhaa hutambua Yangon kama mji mkuu.


Imepakana na China upande wa kaskazini, Laos upande wa mashariki, Uthai kusini-mashariki, Bangladesh na Uhindi magharibi.

Kuna pwani kwenye Bahari Hindi yenye urefu wa km 2,000.

Jiografia

hariri

Kaskazini mwa nchi kuna milima mingi. Safu tatu za Rakhine Yoma, Bago Yoma na Nyanda za Juu za Shan zimeanza katika Himalaya na kuelekea kusini. Milima ya Hengduan Shan iko mpakani kwa China. Mlima mkubwa ni Hkakabo Razi kwenye jimbo la Kachin wenye kimo cha mita 5,881.

Mito mitatu mikubwa ya Myanmar inavuka kati ya safu za milima; niː

Mto Ayeyarwady ni mto mkubwa wa Myanmar wenye urefu wa km 2,170. Bonde lake ni la rutuba na lina wakazi wengi.

Karibu nusu ya nchi imefunikwa na misitu.

Miji mikubkwa

hariri
Nafasi mwaka 2006 Mji Sensa ya 1983 Kadirio kwa 2006 Dola / Mkoa
1. Yangon (Rangoon) 2,513,023 4,572,948 Mkoa wa Yangon
2. Mandalay 532,949 1,237,028 Mkoa wa Mandalay
3. Naypyidaw (Nay Pyi Taw) * 0 924,608 Eneo la Kitaifa Naypyidaw
4. Mawlamyaing 219,961 451,011 Dola la Mon
5. Bago 150,528 248,899 Mkoa wa Bago
6. Pathein 144,096 241,624 Mkoa wa Ayeyarwady
7. Monywa 106,843 185,783 Mkoa wa Sagaing
8. Meiktila 96,492 181,744 Mkoa wa Mandalay
9. Sittwe 107,621 181,172 Dola la Rakhine
10. Mergui 88,600 177,961 Mkoa wa Tanintharyi
11. Taunggyi 108,231 162,396 Dola la Shan

Historia

hariri

Tangu karne ya 9 BK nchi iliona falme mbalimbali zilizotawala kutoka mji mkuu wa Pagan.

Katika karne ya 19 Uingereza ulianza kujishughulisha na habari za Burma (Myanmar) baada ya kutawala maeneo jirani ya Uhindi. Kwa vita tatu kati ya miaka 1826 na 1885 Uingereza ulieneza utawala wake.

Burma ilikuwa sehemu ya Uhindi wa Kiingereza tangu 1885.

Mwaka 1937 Waingereza walianza kutawala Burma kama koloni la pekee.

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia Japan ilitwaa karibu nchi yote.

Baada ya vita Burma ikapata uhuru wake tarehe 4 Januari 1948.

Serikali iliyochaguliwa kidemokrasia ilipinduliwa na jeshi mwaka 1962.

Mtawala mpya hadi mwaka 1988 alikuwa jenerali Ne Win aliyetangaza siasa ya "Ujamaa wa Kiburma". Upinzani ulikandamizwa vikali mara kadhaa.

Nchi iliona harakati kwa ajili ya demokrasia na dhidi ya udikteta mwaka 1988; hapo Ne Win alijiuzulu.

Baada ya maandamano yaliyokandamizwa mara kadhaa, Jenerali Saw Maung alichukua utawala kwa nguvu ya kijeshi.

Uchaguzi huru wa mwaka 1989 ulileta ushindi wa chama cha NLD, chini ya Aung San Suu Kyi, lakini kamati ya kijeshi ilikataa kukabidhi madaraka.

Burma ilibadilishiwa jina kuitwa "Myanmar" ikaendelea kutawaliwa na serikali ya kijeshi hadi mwaka 2011. Upinzani haukuruhusiwa.

Utawala

hariri

Myanmar imegawiwa kwa kusudi la utawala katika madola 7 na mikoa 7. "Madola" ni maeneo yanayokaliwa na jumuiya na makabila ambayo ni tofauti na kundi kubwa la taifa linaloitwa Bamar. Maeneo ya Bamar huitwa mikoa.

 
Majimbo ya Myanmar

Madola ya jumuiya ndogo yapo zaidi karibu na mipaka ya nchi. Kuanzia kusini-magharibi ni haya yafuatayo:

Halafu kuna mikoa 7:

Mazingira ya mji mkuu Naypyidaw ni eneo la kitaifa la Naypyidaw.

Madola na mikoa imegawiwa katika wilaya, tarafa, kata na vijiji.

Myanmar ni nchi ya makabila mengi (135 yametambulika rasmi) na lugha nyingi (angalia orodha ya lugha za Myanmar). Kundi kubwa (68%) ni Waburma wenye asili katika milima ya Tibet walikotokea mababu wao miaka 1000 hivi iliyopita.

Lugha kubwa ni Kiburma, ambacho ndicho lugha rasmi.

Wakazi walio wengi (80%) hufuata dini ya Ubuddha, hasa ya madhehebu ya Theravada. Wakristo ni 7%, wafuasi wa dini za jadi ni 6%, Waislamu ni 4%, Wahindu ni 2%.

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Taarifa za jumla
Uchumi
Kilimo
Biashara

22°N 96°E / 22°N 96°E / 22; 96


Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Myanmar kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.