Jimbo Kuu la Kigali
Jimbo Kuu la Kigali (kwa Kilatini Archidioecesis Kigaliensis) ni jimbo kuu la kanda ya Kanisa Katoliki ya Kigali nchini Rwanda.
Chini yake kuna majimbo mengine yote 8 ya Rwanda: Butare, Byumba, Cyangugu, Gikongoro, Kabgayi, Kibungo, Nyundo na Ruhengeri.
Askofu mkuu ni Thaddée Ntihinyurwa (tangu mwaka 1996).
Uongozi
hariri- Maaskofu wakuu
- Vincent Nsengiyumva, 1976–1994
- Thaddée Ntihinyurwa, 1996–
Takwimu
haririEneo la jimbo lina kilometa mraba 3,116, ambapo kati ya wakazi 1,528,000 Wakatoliki ni 833,000 (54.5%) katika parokia 27.