Jamhuri ya Kituruki ya Kupro ya Kaskazini
Jamhuri ya Kituruki ya Kupro ya Kaskazini (Kituruki: Kuzey Kıbrıs Türk Cumhuriyeti) ni nchi isiyotambuliwa na jumuiya ya kimataifa iliyoko sehemu ya kaskazini ya kisiwa cha Kupro. Eneo lake ni 3,335 km² kuna wakazi lakhi mbili karibu wote ni Waturuki pamoja na Wagiriki 3,000 waliobaki kwenye rasi ya Rizokarpaso. Mji mkuu ni sehemu ya kituruki ya Nikosia.
Ni eneo lililojitenga na Jamhuri ya Kupro baada ya vita ya 1974. Hadi wakati ule Wakupro Wagiriki (waliokuwa wengi) na Wakupro Waturuki (waliokuwa takriban robo ya wakazi) waliishi pamoja pande zote za kisiwa. 1974 maafisa Wagiriki wa jeshi la Kupro walipindua serikali ya Askofu Makarios kwa shabaha ya kuunganisha kisiwa na Ugiriki. Uturuki uliingia kati ukavamia kisiwa kwa kusudi ya kukinga wakazi wenyeji Waturuki.
Jeshi la Kituruki lilitwaa theluthi ya kaskazini ya kisiwa. Wakupro Wagiriki 160,000 kutoka kaskazini walikimbia kwenda kusini na Wakupro Waturuki 50,000 kutoka kusini wakakimbia kaskazini.
Hata baada ya mwisho wa uasi na kurudi kwa rais Askofu Makarios jeshi la Uturuki likakataa kundoka tena. 1973 Dola la Kujitawala la Kituruki la Kupro likatangazwa. 1983 Jamhuri ya Kituruki ya Kupro ya Kaskazini ikatangaza uhuru wake lakini haikutambuliwa na UM wala na nchi yoyote isipokuwa Uturuki.
Wakupro Waturuki walio wengi wameondoka kisiwani wakihamia Uingereza na nchi nyingine. Idadi kubwa ya watu wenye utamaduni wa Kituruki kisiwani wamehamia kutoka Uturuki bara baada ya uvamizi wa jeshi la Uturuki.
Viungo vya Nje
hariri- Zypern Times
- North Cyprus Information Map Ilihifadhiwa 17 Juni 2007 kwenye Wayback Machine. - A Directory and Information Source for Northern Cyprus. Company Information including location maps. General and Specific Questions for Residences and Tourists
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Jamhuri ya Kituruki ya Kupro ya Kaskazini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Jamhuri ya Kituruki ya Kupro ya Kaskazini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |