Bhutan
Bhutan ni nchi ndogo ya Bara Hindi katika milima ya Himalaya.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: "Nchi moja, taifa moja" | |||||
Wimbo wa taifa: Druk tsendhen | |||||
Mji mkuu | Thimphu | ||||
Mji mkubwa nchini | Thimphu | ||||
Lugha rasmi | Kidzongkha | ||||
Serikali | Ufalme Jigme Khesar Namgyal Wangchuck (འཇིགས་མེད་གེ་སར་རྣམ་རྒྱལ་དབང་ཕྱུག) Tshering Tobgay (ཚེ་རིང་སྟོབས་རྒྱས) | ||||
Ufalme wa kikatiba Wangchuk Dynasty |
17 Desemba 1907 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
38,394 km² (ya 133) 1.1 | ||||
Idadi ya watu - 2021 kadirio - 2022 sensa - Msongamano wa watu |
777,486 (ya 159) 727,145 20.3/km² (ya 210) | ||||
Fedha | Ngultrum (BTN )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
BTT (UTC+6:00) (haitumiki) (UTC+6:00) | ||||
Intaneti TLD | .bt | ||||
Kodi ya simu | +975
- |
Nchi imepakana na Uhindi na jimbo la Tibet la China.
Imetawaliwa na mfalme Jigme Khesar Namgyel Wangchuck tangu 2006.
Kuna wakazi takriban lakhi saba unusu.
Mji mkuu unaitwa Thimphu.
Jiografia
haririBhutan ni nchi ya milima, na zaidi ya 80% za eneo la Bhutan ziko juu ya kimo cha mita 2,000. Mpakani kwa China kuna milima ya juu ya Lunana. Kula Kangri ni mlima mkubwa wenye kimo cha mita 7,553. Kusini tu kuna kanda nyembamba ya tambarare ya Duar.
Watu walio wengi hukalia eneo la milimani kati ya mita 2,000 hadi 3,000 juu ya UB.
Historia
haririBhutan ilianzishwa mwaka 1644 na mmonaki Mbuddha Shabdrung Ngawang Namgyel.
Nchi iliweza kutunza uhuru wake hadi leo, lakini ililazimishwa kukubali maeneo ya kusini yatwaliwe na Waingereza na kuunganishwa na Uhindi wa Kiingereza. Uingereza ilishughulikia pia mahusiano ya nje ya Bhutan.
Uhusiano huu umeendelea na India kulingana na mkataba wa urafiki wa tarehe 8 Agosti 1949.
Tarehe 12 Februari 1971 Bhutan ikapokewa kama nchi mwanachama wa UM.
Wakazi na Utamaduni
haririWabhutan walio wengi huishio mlimani wako karibu kiutamaduni na kilugha na watu wa Tibet na Burma. Hao hufuata dini ya Ubuddha (74.7%) ambayo ndiyo dini rasmi. Lugha za jamii hiyo zinazotumika nchini humo ni 23. Mojawapo, Kidzongkha, ndiyo lugha rasmi.
Watu wa kusini wanafanana zaidi na watu wa Nepal na hutumia Kinepali, mojawapo ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Wanafuata dini ya Uhindu (22.6%).
Bhutan inajitahidi kutunza utamaduni wake. Hadi mwaka 1974 watalii hawakuruhusiwa kutembelea nchi. Baadaye imewezekana lakini si rahisi kupata kibali.
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- Karma Phuntsho (2013). The History of Bhutan. Nodia: Random House India. ISBN 9788184003116.
- Osmani, Siddiqur R.; Bajracharya, B.B.; Tenzing, S.; Wangyal, T. (2007). Macroeconomics of Poverty Reduction: The Case Study of Bhutan (PDF) (tol. la 2). Colombo: UNDP. uk. 302. ISBN 978-955-1416-00-3. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2011-07-28. Iliwekwa mnamo 2015-10-16.
- Wangchhuk, Lily (2008). Facts About Bhutan: The Land of the Thunder Dragon. Thimphu: Absolute Bhutan Books. ISBN 99936-760-0-4.
- Revkin, Andrew C.. "A New Measure of Well-Being From a Happy Little Kingdom", The New York Times, 4 October 2005. Retrieved on 4 October 2005.
- "Border tension pushes MEA allocation". The Tribune, Chandigarh. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2005-07-22. Iliwekwa mnamo 8 Septemba 2005.
{{cite web}}
: Unknown parameter|deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - "Bhutan". Bhutan. MSN Encarta. Archived from the original on 31 October 2009. http://www.webcitation.org/5kwQ2kjMZ. Retrieved 8 September 2005. Archived 28 Oktoba 2009 at the Wayback Machine.
- "BTI 2008 — Bhutan Country Report". Gütersloh: Bertelsmann Stiftung. 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-02-24. Iliwekwa mnamo 11 Desemba 2008.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - A.P. Agarwala (2003). Sikkim and Bhutan. Nest and Wings. ISBN 81-7824-008-4.
- Datta-Ray, Sunanda K. (1984). Smash and Grab: The Annexation of Sikkim. Vikas. ISBN 0-7069-2509-2.
- Foning, A.R. (1987). Lepcha, My Vanishing Tribe. Sterling Publishers. ISBN 81-207-0685-4.
- Rose, Leo. The Nepali Ethnic Community in the Northeast of the Subcontinent. University of California, Berkeley.
- Napoli, Lisa (2011). Radio Shangri-La: What I Learned in Bhutan, the Happiest Kingdom on Earth. Crown. ISBN 0-307-45302-2.
- Niestroy, Ingeborg; García Schmidt, Armando; Esche, Andreas (2013). "Bhutan: Paradigms Matter", in: Bertelsmann Stiftung (ed.): Winning Strategies for a Sustainable Future. Reinhard Mohn Prize 2013. Verlag Bertelsmann Stiftung, Gütersloh. ku. 55–80. ISBN 978-3-86793-491-6.
{{cite book}}
: External link in
(help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)|title=
Viungo vya nje
hariri- (Kiingereza) Tovuti ya serikali Archived 30 Desemba 2005 at the Wayback Machine.
- (Kiingereza) The Bhutan Times (gazeti)
- Bhutan entry at The World Factbook
- Bhutan Links Archived 10 Aprili 2009 at the Wayback Machine. at the National Library of Bhutan.
- Bhutan profile, BBC News.
- Bhutan Archived 29 Agosti 2012 at the Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs.
- Bhutan, Encyclopædia Britannica entry.
- Bhutan katika Open Directory Project
- Wikimedia Atlas of Bhutan
- Tourism Council of Bhutan
- Key Development Forecasts for Bhutan from International Futures.
Nchi na maeneo ya Asia |
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China. |
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Bhutan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |