Orodha ya Makaizari wa Bizanti
(Elekezwa kutoka Orodha ya Makaizari wa Byzantini)
Orodha hii inataja makaizari wa Bizanti kuanzia nasaba ya Theodosius hadi mwisho wa Dola la Roma Mashariki mwaka wa 1453.
Nasaba ya akina Theodosius
haririMiaka ya Utawala | Jina la Kaizari | Maelezo |
---|---|---|
28 Machi, 364 hadi 9 Agosti, 378 | Valens | Alikufa kwenye mapigano ya Adrianopoli. |
19 Januari, 379 hadi 17 Januari, 395 | Theodosius I | Alipewa mamlaka katika Mashariki kutoka kwa Flavius Gratianus aliyekuwa Kaizari wa Magharibi. |
17 Januari, 395 hadi 1 Mei, 408 | Arkadius | Mwana wa Theodosius I |
1 Mei, 408 hadi 28 Julai, 450 | Theodosius II | Mwana wa Arkadius |
450 hadi 2 Januari, 457 | Markian | Alipata kuwa Kaizari baada ya kumwoa Pulkeria, dada wa Theodosius II |
Nasaba ya Thraki
haririMiaka ya Utawala | Jina la Kaizari | Maelezo |
---|---|---|
7 Februari, 457 hadi 18 Januari, 474 | Leo I | Aliteuliwa na jenerali Aspar. |
18 Januari, 474 hadi 17 Novemba, 474 | Leo II | Mjukuu wa Leo I. |
17 Novemba, 474 hadi 9 Januari, 475 | Zeno | Baba yake Leo II. |
9 Januari, 475 hadi Agosti 476 | Basilisko | Shemeji wa Leo I. |
Agosti 476 hadi 9 Aprili, 491 | Zeno | awamu yake ya pili |
11 Aprili, 491 hadi 9 Julai, 518 | Anastasi I | Aliteuliwa na Ariadne, mjane wa Zeno, na kumwoa baadaye. |
Nasaba ya akina Justiniani
haririMiaka ya Utawala | Jina la Kaizari | Maelezo |
---|---|---|
Julai 518 hadi 1 Agosti, 527 | Justini I | |
1 Agosti, 527 hadi 14 Novemba, 565 | Justiniani I | Mpwa na mrithi wa Justini I |
14 Novemba, 565 hadi 5 Oktoba, 578 | Justini II | Mpwa na mrithi wa Justiniani I |
5 Oktoba, 578 hadi 14 Agosti, 582 | Tiberi II | Labda aliuawa kwa sumu |
14 Agosti, 582 hadi Novemba 602 | Maurikios | Alimwoa binti Tiberi II |
Bila nasaba
haririMiaka ya Utawala | Jina la Kaizari | Maelezo |
---|---|---|
Novemba 602 hadi Oktoba 610 | Fokas |
Nasaba ya akina Heraklios
haririMiaka ya Utawala | Jina la Kaizari | Maelezo |
---|---|---|
5 Oktoba, 610 hadi 11 Februari, 641 | Herakli | |
Februari 641 hadi 24 Mei, 641 | Konstantino III | Mwana wa Herakli; Kaizari-Mshiriki pamoja na Heraklonas |
Februari 641 hadi Septemba 641 | Heraklonas | Mwana wa Herakli; Kaizari-Mshiriki pamoja na Konstantino III |
641 hadi 15 Septemba, 668 | Konstas II | Mwana wa Konstantino III |
Septemba 668 hadi Septemba 685 | Konstantino IV | Mwana wa Konstas II |
Septemba 685 hadi 695 | Justiniani II | Mwana wa Konstantino IV |
695 hadi 698 | Leontios | Mnyang'anyi |
698 hadi 705 | Tiberi III | Mnyang'anyi |
705 hadi Desemba 711 | Justiniani II | awamu yake ya pili |
Bila nasaba
haririMiaka ya Utawala | Jina la Kaizari | Maelezo |
---|---|---|
Desemba 711 hadi 3 Juni, 713 | Philippikos Bardanes | |
Juni 713 hadi 715 | Anastasi II | katibu wa Philippikos |
715 hadi 717 | Theodosi III |
Nasaba ya Isauri
haririMiaka ya Utawala | Jina la Kaizari | Maelezo |
---|---|---|
717 hadi 18 Juni, 741 | Leo III | |
Juni 741 hadi 741 | Konstantino V | |
741 hadi 743 | Artabasdos | waziri chini ya Leo III |
743 hadi 14 Septemba, 775 | Konstantino V | awamu yake ya pili |
Septemba 775 hadi 8 Septemba, 780 | Leo IV | mwana wa Konstantino V |
Septemba 780 hadi 15 Agosti, 797 | Konstantino VI | mwana wa Leo IV |
15 Agosti, 797 hadi 802 | Malkia Irene | mama ya Konstantino VI |
Nasaba ya Nikephoros
haririMiaka ya Utawala | Jina la Kaizari | Maelezo |
---|---|---|
802 hadi 26 Julai, 811 | Nikeforo I | |
Julai 811 hadi Agosti 811 | Staurakios | mwana wa Nikeforo I |
811 hadi Juni 813 | Mikaeli I Rangabe | alimwoa binti Nikeforo I |
Bila nasaba
haririMiaka ya Utawala | Jina la Kaizari | Maelezo |
---|---|---|
Julai 813 hadi 25 Desemba, 820 | Leo V |
Nasaba ya Frigia
haririMiaka ya Utawala | Jina la Kaizari | Maelezo |
---|---|---|
25 Desemba, 820 hadi Oktoba 829 | Mikaeli II | mke wake alikuwa binti Konstantino VI |
Oktoba 829 hadi 20 Januari, 842 | Theofilo | mwana wa Mikaeli II, alikuwa Kaizari-Mshiriki tangu 820 |
20 Januari, 842 hadi Novemba 855 | Malkia Theodora I | mke wa Theophilos, alimtawalia mwana wake |
Novemba 855 hadi 23 Septemba, 867 | Mikaeli III | mwana wa Theophilos, alitawala kumpitia mamake tangu 842 |
Nasaba ya Makedonia
haririMiaka ya Utawala | Jina la Kaizari | Maelezo |
---|---|---|
23 Septemba, 867 hadi 29 Agosti, 886 | Basili I | alimwoa mjane wa Mikaeli III |
29 Agosti, 886 hadi 11 Mei, 912 | Leo VI | mwana wa Basili I, Kaizari-Mshiriki tangu 870 |
11 Mei, 912 hadi 6 Juni, 913 | Aleksanda III | mwana wa Basili I, Kaizari-Mshiriki tangu 879 |
6 Juni, 913 hadi 9 Novemba, 959 | Konstantino VII | mwana wa Leo VI, Kaizari-Mshiriki tangu 911 |
919 hadi 944 | Romano I | baba mkwe wa Konstantino VII aliyemtawalia |
959 hadi 15 Machi, 963 | Romano II | mwana wa Konstantino VII |
3 Julai, 963 hadi Desemba 969 | Nikeforo II | alimwoa mjane wa Romano II |
Desemba 969 hadi 10 Januari, 976 | Yohane I | alimwoa dada wa Konstantino VII |
Januari 976 hadi 15 Desemba 1025 | Basili II | mwana wa Romano II |
15 Desemba 1025 hadi 11 Novemba 1028 | Konstantino VIII | mwana wa Romano II, Kaizari-Mshiriki tangu 976 |
11 Novemba 1028 hadi 1050 | Malkia Zoe | binti Konstantino VIII |
11 Novemba 1028 hadi 11 Aprili 1034 | Romano III | mume wa kwanza wa Zoe |
Aprili 1034 hadi 10 Desemba 1041 | Mikaeli IV | mume wa pili wa Zoe |
10 Desemba 1041 hadi Aprili 1042 | Mikaeli V | Mpwa wa Mikaeli IV |
Aprili 1042 hadi Juni 1042 | Malkia Theodora II | Malkia-Mshiriki na dada yake, Zoe |
Juni 1042 hadi 11 Januari 1055 | Konstantino IX | mume wa tatu wa Zoe |
11 Januari 1055 hadi Agosti 1056 | Malkia Theodora II | awamu yake ya pili |
Bila nasaba
haririMiaka ya Utawala | Jina la Kaizari | Maelezo |
---|---|---|
21 Agosti 1056 hadi 31 Agosti 1057 | Mikaeli VI | jenerali aliyeteuliwa na Theodora II |
Nasaba ya akina Komnenos
haririMiaka ya Utawala | Jina la Kaizari | Maelezo |
---|---|---|
8 Juni 1057 hadi 25 Desemba 1059 | Isaka I | alijiuzulu kwa sababu ya ugonjwa |
Nasaba ya akina Doukas
haririMiaka ya Utawala | Jina la Kaizari | Maelezo |
---|---|---|
Desemba 1059 hadi 21 Mei 1067 | Konstantino X | aliteuliwa na Isaak I |
21 Mei 1067 hadi 31 Machi 1078 | Mikaeli VII | mwana wa Konstantino X |
Januari 1068 hadi 24 Oktoba 1071 | Romano IV | alimwoa mjane wa Konstatino X; Kaizari-Mshiriki na Michael VII |
7 Januari 1078 hadi 4 Aprili 1081 | Nikeforo III | alimwoa mke wa Mikaeli VII wakati ndoa haijatengwa |
Nasaba ya akina Komnenos
haririMiaka ya Utawala | Jina la Kaizari | Maelezo |
---|---|---|
4 Aprili 1081 hadi 15 Agosti 1118 | Aleksi I | Mpwa wa Isaak I |
15 Agosti 1118 hadi 8 Aprili 1143 | Yohane II | mwana wa Aleksi I |
8 Aprili 1143 hadi 24 Septemba 1180 | Manuel I | mwana wa Yohane II |
24 Septemba 1180 hadi Novemba 1183 | Aleksi II | mwana wa Manuel I |
Septemba 1183 hadi 12 Agosti 1185 | Androniko I | mpwa wa Yohane II |
Nasaba ya akina Angelos
haririMiaka ya Utawala | Jina la Kaizari | Maelezo |
---|---|---|
12 Agosti 1185 hadi 8 Aprili 1195 | Isaka II | |
8 Aprili 1195 hadi 1 Agosti 1203 | Aleksi III | kaka wa Isaak II |
1 Agosti 1203 hadi Januari 1204 | Isaka II | awamu yake ya pili; Kaizari-Mshiriki na mwana wake |
1 Agosti 1203 hadi Januari 1204 | Aleksi IV | mwana wa Isaka II |
Januari 1204 hadi 12 Aprili 1204 | Aleksi V | alimwoa binti Aleksi III |
Nasaba ya akina Laskaris
haririMiaka ya Utawala | Jina la Kaizari | Maelezo |
---|---|---|
Aprili 1204 hadi 1205 | Konstantino Laskaris | hakuvishwa taji, kwa hiyo hahesabiwi kama Konstantino XI |
1205 hadi Novemba 1222 | Theodori I | kaka wa Konstantino Laskaris |
Novemba 1222 hadi 3 Novemba 1254 | Yohane III | mkwe mwana wa Theodori I |
3 Novemba 1254 hadi Agosti 1258 | Theodori II | mwana wa Yohane III |
Agosti 1258 hadi Agosti 1261 | Yohane IV | mwana wa Theodori II |
Nasaba ya akina Palaiologos
haririMiaka ya Utawala | Jina la Kaizari | Maelezo |
---|---|---|
1259 hadi 11 Desemba 1282 | Mikaeli VIII | |
11 Desemba 1282 hadi Mei 1328 | Androniko II | mwana wa Mikaeli VIII |
Mei 1328 hadi 15 Juni 1341 | Androniko III | mjukuu wa Andronikos II |
15 Juni 1341 hadi Mei 1347 | Yohane V | mwana wa Androniko III |
Mei 1347 hadi 1354 | Yohane VI | baba mkwe wa Yohane V |
1354 hadi 12 Agosti 1376 | Yohane V | awamu yake ya pili |
12 Agosti 1376 hadi 1379 | Androniko IV | mwana wa Yohane V |
18 Oktoba 1377 hadi 1379 | Yohane VII | Kaizari-Mshiriki na Androniko IV |
1379 hadi 1390 | Yohane V | awamu yake ya tatu |
miezi michache 1390 | Yohane VII | awamu yake ya pili |
1390 hadi 16 Februari 1391 | Yohane V | awamu yake ya nne |
16 Februari 1391 hadi 21 Julai 1425 | Manuel II | mwana wa John V; Kaizari-Mshiriki tangu 1373 |
1399 hadi 1402 | Yohane VII | awamu yake ya tatu; alimtawalia Manuel II |
21 Julai 1325 hadi 31 Oktoba 1448 | Yohane VIII | mwana wa Manuel II |
Januari 1449 hadi 29 Mei 1453 | Konstantino XI | mwana wa Manuel II |