Chile
Chile ni nchi ya Amerika Kusini.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: "Por la razón o la fuerza" (Kwa akili au nguvu) | |||||
Wimbo wa taifa: Puro, Chile, es tu cielo azulado "Safi ee Chile ni anga lako ya buluu"' | |||||
Mji mkuu | Santiago de Chile1 | ||||
Mji mkubwa nchini | Santiago de Chile | ||||
Lugha rasmi | Kihispania | ||||
Serikali | Jamhuri Gabriel Boric | ||||
Uhuru Serikali ya kwanza ya uhuru Ilitangazwa Ilitambuliwa |
18 Septemba 1810 12 Februari 1818 25 Aprili 1844 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
756,096.3 km² (ya 38) 1.07%2 | ||||
Idadi ya watu - 2021 kadirio - 2017 sensa - Msongamano wa watu |
19,678,310 (ya 62) 17,574,003 26/km² (ya 198) | ||||
Fedha | Peso (CLP )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
— (UTC-4) — (UTC-3) | ||||
Intaneti TLD | .cl | ||||
Kodi ya simu | +56
- | ||||
1 The legislative body operates in Valparaíso 2 Includes Easter Island and Isla Sala y Gómez; does not include 1,250,000 km² of claimed territory in Antarctica |
Eneo lake ni kama kanda ndefu nyembamba kati ya safu za milima ya Andes na Bahari ya Pasifiki.
Imepakana na Peru, Bolivia na Argentina.
Ni sehemu za Chile pia maeneo ya Kisiwa cha Pasaka (Rapa Nui), Kisiwa cha Salas y Gómez, Visiwa vya Juan Fernández (pamoja na kisiwa cha Robinson Crusoe), visiwa vya Desventuradas, Visiwa vya Ildefonso na visiwa vya Diego Ramirez.
Chile inadai ya kuwa sehemu ya bara la Antaktika ni eneo lake.
Mji mkuu ni Santiago, yaani Mtakatifu Yakobo.
Jiografia
haririChile ina urefu wa kilomita 4,200 kufuata pwani ya Pasifiki na milima ya Andes. Umbali huu ni kama kutoka Cape Town kwenda Dar es Salaam. Lakini upana wa wastani wa eneo lake ni kilomita 180 tu: sehemu nyembamba ya nchi ina upana wa kilomita 90, sehemu pana zaidi ina kilomita 240.
Nje ya maeneo yenye uwanja mwembamba wa pwani, nchi yote ni ya milima na mabonde. Sehemu kubwa ya nchi ina safu mbili za milima:
- Andes katika mashariki na
- Cordillera de la Costa (safu ya pwani) katika magharibi.
Katikati ya safu hizo mbili kuna bonde la kati (Valle Central) lenye makazi ya idadi kubwa ya wananchi na ardhi yenye rutuba kwa kilimo.
Kuelekea kusini kimo cha nchi hushuka hadi kufikia chini ya uwiano wa bahari. Milima ya safu ya pwani huonekana sasa kama visiwa.
Kaskazini mwa nchi hakuna bonde kubwa la kati. Nchi inapanda juu kutoka mwambao wa bahari hadi kuwa tambarare yenye kimo cha mita 1,000 - 1,500 inayoendelea mpaka mwanzo wa safu ya Andes.
Milima
haririAndes za Chile ni kati ya milima ya juu duniani: kuna vilele kadhaa juu ya mita 6,000.
- Volkeno ya Nevado Ojos del Salado, mita 6,880 (Región de Atacama)
- Cerro Tupungato, mita 6,800 (Región Metropolitana)
- Volkeno ya Llullaillaco, mita 6,739 (Región de Antofagasta)
- Volkeno ya Parinacota, mita 6,342 (Región de Tarapacá)
- Volkeno ya Licancábur, mita 5,916 (Región de Antofagasta)
- Descabezado Grande, mita 3,830 (Región del Maule)
- Torres del Paine, mita 2,800 (Región de Magallanes y de la Antártica Chilena)
- Volkeno ya Villarrica, mita 2,840 (Región de la Araucanía)
- Volkeno ya Osorno, mita 2,652 (Región de Los Lagos)
- Volkeno ya Cerro Hudson, mita 1,905 (Región de Aisén)
Watu
haririWakazi wengi (85%) wanaishi mijini. Utafiti juu ya DNA yao unaonyesha kwa asilimia 52% hivi ina asili ya Ulaya, 43% ni ya Kiindio na 5% ni kutoka Afrika. Kwa jumla, wengi wana mchanganyiko wa damu.
Lugha rasmi na ya kawaida ni Kihispania.
Upande wa dini, 66.6% ni Wakatoliki na 17% ni Waprotestanti. Asilimia 12.4 haina dini yoyote.
Tazama pia
haririViungo vya nje
hariri- (Kihispania) Serikali ya Chile tovuti rasmi
Nchi na maeneo ya Amerika Kusini |
Argentina | Bolivia | Brazil | Chile | Ekuador | Guyana | Guyani ya Kifaransa | Kolombia | Paraguay | Peru | Surinam | Uruguay | Venezuela |
Makala hii kuhusu maeneo ya Chile bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Chile kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |